Ndugu zangu wanajamii ni matumaini makubwa kwa CDM kwa kile kilicho dhihirika Igunga licha ya kumwagwa kwa billion 10 na magamba. wito ni kwa chama chetu chakizalendo CDM kuelekeza mashambulizi Monduli. Kwa utafiti wangu Monduli inapaswa kuvaliwa buti mapema kwani watu wake wanauwelewa mfupi zidi ya haki zao kidemokrasia. Ila na matumaini makubwa sana na vijana wa kimasai ambao nimekuwa nikijadiliana nao kila mara na wanaonyesha muamko mkubwa sana kwa CDM na hasa wanahitaji kuona kiongozi kijana atakaye wania nafasi hiyo. Tatizo kubwa ni kwa wakina mama na wazee ambao huongwa pesa, tisheti za ccm na nachakula ktk sherehe mbalimbali zinazoendeshwa na mmoja wa kigogo maarufu Monduli. Kwataarifa yenu wanajamii, watu hawaipendi ccm monduli ila wanaogopa vitisho toka kwa kigogo huyo na baadhi ya mapaparazi wake wanaompelekea taarifaa kuhusu misimamo ya watu kihitikadi kwa lengo lakupewa chochote na kuonekana wa maana. Lingine wanajamii nikuwa kijana mmoja hivi majuzi alionekana kupeperusha bendera ya CDM nakuitwa na baadhi wa wapambe wa ccm na kumpa vitisho vikali mno. Jamani nchi hii ni yakidemkrasia kwa misingi ya katiba ya nchi, hivyo kila mtu anahaki ya kuwa mfuwasi wa chama chochote kwa mujibu wa sheria.