Baada ya Igunga kazi ipo Monduli

oldekenya

New Member
Oct 4, 2011
3
0
Ndugu zangu wanajamii ni matumaini makubwa kwa CDM kwa kile kilicho dhihirika Igunga licha ya kumwagwa kwa billion 10 na magamba. wito ni kwa chama chetu chakizalendo CDM kuelekeza mashambulizi Monduli. Kwa utafiti wangu Monduli inapaswa kuvaliwa buti mapema kwani watu wake wanauwelewa mfupi zidi ya haki zao kidemokrasia. Ila na matumaini makubwa sana na vijana wa kimasai ambao nimekuwa nikijadiliana nao kila mara na wanaonyesha muamko mkubwa sana kwa CDM na hasa wanahitaji kuona kiongozi kijana atakaye wania nafasi hiyo. Tatizo kubwa ni kwa wakina mama na wazee ambao huongwa pesa, tisheti za ccm na nachakula ktk sherehe mbalimbali zinazoendeshwa na mmoja wa kigogo maarufu Monduli. Kwataarifa yenu wanajamii, watu hawaipendi ccm monduli ila wanaogopa vitisho toka kwa kigogo huyo na baadhi ya mapaparazi wake wanaompelekea taarifaa kuhusu misimamo ya watu kihitikadi kwa lengo lakupewa chochote na kuonekana wa maana. Lingine wanajamii nikuwa kijana mmoja hivi majuzi alionekana kupeperusha bendera ya CDM nakuitwa na baadhi wa wapambe wa ccm na kumpa vitisho vikali mno. Jamani nchi hii ni yakidemkrasia kwa misingi ya katiba ya nchi, hivyo kila mtu anahaki ya kuwa mfuwasi wa chama chochote kwa mujibu wa sheria.
 
Sasa naanza kuwashangaa chadema na msinilazimishe niamini maneno ya kada mmoja pale makumbusho kwamba kama tumeweza kuimaliza cuf tutashindwa chadema? Acheni uppuzi tafuteni tume huru ya uchaguzi lasivyo muendeleze kutupa show na mwisho wa siku hatupigi kura maana tayari tunajua mshindi.
 
Ningewashauri Chadema waachane na hizi by-elections kwenye majimbo yaliyochukuliwa na ccm kwani inawapotezea FOCUS ya kuwekeza nguvu kwenye kupigania kuandikwa kwa KATIBA kabla ya 2015!! CCM wanataka kuwapotezea nguvu kwenye hizi by-election ili kusiwe na msukumo kwenye kugombea kuandikwa kwa katiba mpya.
 
.... lisema Mchungaji Mtikila tangu siku nyingi; tatizo ni KATIBA chakavu na Tume ya Uchaguzi nchini. Tuelekeze sasa nguvu zetu hapa tujue kimoja. Kazi iansze mara moja kote nchini ikiambatana na kufungua mashina zaidi kote nchini.
 
Sasa naanza kuwashangaa chadema na msinilazimishe niamini maneno ya kada mmoja pale makumbusho kwamba kama tumeweza kuimaliza cuf tutashindwa chadema? Acheni uppuzi tafuteni tume huru ya uchaguzi lasivyo muendeleze kutupa show na mwisho wa siku hatupigi kura maana tayari tunajua mshindi.

Unanchekesha! CUF ndio kwanza wanaongoza nchi unasema umewamaliza? Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana.
 
Unanchekesha! CUF ndio kwanza wanaongoza nchi unasema umewamaliza? Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana.

Wanaongoza nchi gani?, au danganya toto ya Zanzibar ndio yakuchanganya mamaa!, Kile ndio kifo chao CUF!, halafu CCM ndio wanatamba kuimaliza CUF na huo ndio ukweli!

2015 wanaweza wasisimamishe mgombea kama hawatajitazama upya wakastaafisha kwa nguvu Mzee Lipumba na Maalim!
 
Monduli msiguse pale mtakufa kifo cha MENDE
Wacha vitisho huko Monduli tunakuja CDM moto wake unahamia huko. Mwambie huyo kigogo aache kabisa kuteka na kutisha vijana wetu!!!!!!!!!! Yeye kwani ni nani, hata Ghadafi anaikimbia Libya!!!!!!!!!!!!
 
Ningewashauri Chadema waachane na hizi by-elections kwenye majimbo yaliyochukuliwa na ccm kwani inawapotezea FOCUS ya kuwekeza nguvu kwenye kupigania kuandikwa kwa KATIBA kabla ya 2015!! CCM wanataka kuwapotezea nguvu kwenye hizi by-election ili kusiwe na msukumo kwenye kugombea kuandikwa kwa katiba mpya.
Huo ni woga sasa kuacha kupeleka timu kwenye ligi eti mshindi amaeisha julikana. Vita ni mbele kwa mbele hapo CDM inapata uzoefu na watu wanapata uelewa pomoja na kutambua chama kilicho makini kutetea wanyonge!!!!!!!!!!!!CHADEMA songa mbele baada ya Monduli Arusha mjini!!!!!!
 
Unanchekesha! CUF ndio kwanza wanaongoza nchi unasema umewamaliza? Ama kweli asiyejuwa maana haambiwi maana.

Ni huo ushungi ndo unaonena ama ni kitu kingine baby? Lini CAFU (CUF) wameshika dola kuongoza nchi? Unataka kusema Mwalimu Seif ni Amiri Jeshi mkuu au ndiye Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ). Kushirikishwa tu basi mnaongoza nchi, je mngeshinda si ndo mnge Tawala nchi kabisa. CUF hata bungeni haiongozi, mnaongoza wapi bhana.... hebu nena kwa kinywa na kufikiri.
 
CDM si yakumwogopa mtu wala jimbo sasa hivi ila wao ndo matumbo ya kuharisha sasa hivi. Utaona wabunge watakavyoanza kuiua serikali wakijitetea kila mtu kivyake kutetea jimbo lake ili asijekupitiwa na wimbi hili lililoanzia Igunga. Hamna mbuge wa ccm mwenye ujasiri wa kushinda mbele ya cdm kwa sasa hivi. Tutaona wengi wenye uwezo hasa vijana wanaweza kukimbilia cdm ili wabaki.

Na kwa taarifa yenu 2015 ccm itapata wagombea dhaifu kwa sababu wazuri wataenda kwenye chama ambacho huhitaji gharama kupata ubunge Kama ilivyo kwa ccm. Kumbuka kwenye uchaguzi mkuu kila mgombea atakufa kivyake bila msaada wa serikali maana ccm na serikali itakuwa biz na Uraisi.

Watu wanasahau kuwa cdm kushiriki hizi chaguzi ndogo si kwa ajili ya kushinda tu bali pia ni furusa muhimu sana ya kukijenga chama kwenye maeneo hayo. Fikiria faida waliyoipata pale Igunga ingechukua muda mrefu sana kukijenga chama pale Igunga lakini leo hii Igunga tayari imeshaingia kwenye majimbo ambayo ni ngome ya chadema na potential kwa uchaguzi ujao.

Kama ccm hawana akili basi wataendelea na uvuaji wa magamba kwa faida ya cdm lakini nadhani wanawashauri pia hawatafanya hivyo tena. Kama watamvua EL wajua kuwa atapigia kampeni cdm kabisa bilA hata chenga wajaribu waone.
 
Ccm sawa mmeshinda igunga tunaomba mechi ya marudiano monduli tutamalizia na bariadi mashariki kote huko mmeshapiga "x" na wavamizi wamekataa kutoka,token tutalipia,bomoabomoa si inaendelea mazee au mnataka kusitisha ali mmesha toa notice muda umepita na mvamizi kakataaa kuondoka what next? Tuhamie monduliiiiiiii sasa vueni gamba tupige game pale!
 
Sasa naanza kuwashangaa chadema na msinilazimishe niamini maneno ya kada mmoja pale makumbusho kwamba kama tumeweza kuimaliza cuf tutashindwa chadema? Acheni uppuzi tafuteni tume huru ya uchaguzi lasivyo muendeleze kutupa show na mwisho wa siku hatupigi kura maana tayari tunajua mshindi.
we ndo mpuuzi unaongea onhea kama bata anayeharisha hapa..hujui unachoongea nenda kamsaidie mkeo kukata vitungui jikoni
 
Huo ni woga sasa kuacha kupeleka timu kwenye ligi eti mshindi amaeisha julikana. Vita ni mbele kwa mbele hapo CDM inapata uzoefu na watu wanapata uelewa pomoja na kutambua chama kilicho makini kutetea wanyonge!!!!!!!!!!!!CHADEMA songa mbele baada ya Monduli Arusha mjini!!!!!!
Mkuu kwa taarifa yako Arusha mjini ni sawa na Makao Makuu ya CDM. Inakupasa ulitambue hilo. Labda useme nguvu nyingi tuzielekeze Tanga, Dar na Zanzibar.
 
CDM inahitaji kujipanga vizuri Monduli,kule kuna ugandamizaji wa Demokrasia,ukisikika unampinga kigogo wao unapewa vitisho sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom