Baada ya hotuba ya Rais, nimepima mkojo wa binadamu kwa kutumia Kipimo cha Malaria, na Kipimo kimesoma "Negative"

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Baada ya kupima mkojo wa binadamu kwa kutumia MRDT ambacho Ni kipimo kinachotumika kupima Malaria, nilitegemea majibu yangekuwa Invalid au undetermined lakini Cha kushangaza kipimo kimeonyesha negative kwa sababu kipimo hiki hutumika kupima damu.

Je kwa majibu haya Kuna uwezekano hata vipimo vya CORONA viko sahihi kwa kutoa majibu ya papai kuwa positive.

NB: yeyote yule anaweza kununua kipimo hiki na kufanya jaribio hili Nyumbani kwake ili ajiridhishe
Screenshot_20200503-183304.png
 
Du!! Hii ni hatari, naona control line imesoma. Huyo magonjwa alileta mkojo Kwa clinical complains gani?! Isije kua mkojo ulikua na mchanganyiko wa damu.

Hata hivo Fanya majaribio, unaweza ukawa umefanya ugunduzi muhim, huenda malaria inaweza pimwa kwenye mkojo badala ya Damu ambayo ni inversive

Asante
 
Ninachohisi kama kuna conflict kati ya wataalamu na wanasiasa hasa Mh. Rais.

Wataalamu wanajaribu kusema ukweli na uhalisia kulingana na taaluma zao.

Mheshimiwa anapinga,hataki kusikia ukweli ili kulinda maslahi yake binafsi ya uongozi wake usiporomoke kiuchumi ambacho yeye anadhani kuwa ndio kipimo Cha ubora wake!

Then? Anasabotage taarifa,mikakati,mbinu na ushauri wa wataalamu ili watu wafanye kazi na kodi iendelee kukusanywa!

Anyway mkuu hongera kwa utafiti mdogo.
 
Hahaha kila kitu kinapima what was intended kupimwa. Nadhani alikuwa anafanya validation kwa kutumia unknown unknown, sijui kwanini alitegemea apate majibu aliyokuwa akiyataka.
 
Back
Top Bottom