Baada ya ''honeymoon'' ya kisiasa, utawala wa Rais Samia utatetewa sana na makundi matatu

Miradi siyo kipaumbele kwa Bi Mkubwa; alimradi masponsa wake wameshiba, yeye anaridhika. Awamu hii ni ya kuwahadaa wananchi kama ilivyofanyika jana kuleee uwanjani. Hivi mwizi wa sokoni na yule wa jana kuna tofauti gani!??? Sanasana huyu wa serikali ni mbaya zaidi maana anatumia cheo alichopewa na rai kuwaibia na kuwahujumu.
Tunawajua sukuma gang hamna jema
 
Haya ni mawazo yako Mkuu.

Tatizo tunachanganya Mambo ya serikali na hasira za mipira na wivu kwa Mzee Mwinyi kuzawadiwa gari.

Nikuombe utulie muda ukingali bado, mawazo yako yanafaa sana wakati wa uchaguzi ili yatumike kama mizania ya hoja.
Kwa sasa unachofanya ni kama kupiga ramli chonganishi.
 
Katika siasa kuna muda ambao kiongozi anayeingia madarakani huwa anapata uungwaji mkono mkubwa na kuna muda ambao kukubalika kwake hupungua sana.
...
Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia 'anatiki' katika mabox haya matatu (Uzanzibari, Uanamke na Uislam) ambayo katika siasa za Tanzania yanahisi hayapewi nafasi ya kuongoza taifa kwa kwa sababu ''yanadharauliwa'', ''yanatengwa'' na ''kubaguliwa''.
...
Wahenga walisema, ''Muda ni mwalimu mzuri''. Muda umeanza kutoa majawabu halisi!

Hayo makundi matatu yatakayo mtetea, na yameanza, ni falsafa hiyo hiyo inaongoza maamuzi yake kwamba:

√ Yeye ni Mzanzibari hivyo rasmali za Tanzania bara (Tanganyika) hana uchungu nazo na ikiwezekana zitumike kwa ajili ya nchi anakotoka;

√ Kama Mwanamke anahisi kudharauliwa kwa sababu kwa dini yake (Uislam) wanawake hawapewi nafasi ya kutosha ya kujitokeza. Na hili la yeye kuwa ni Rais mwenye maumbile ya kike hupenda kulirudia mara kwa mara;

√ Ili kutimiza matakwa ya imani yake ya Uislam aweze kutekeleza majukumu yake ya uongozi, inabidi wasaidizi wake wa karibu wawe pia wa dini hiyo. Hii ni dhahiri katika uteuzi wake wa hivi karibuni na utakaokuja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom