Baada ya ''honeymoon'' ya kisiasa, utawala wa Rais Samia utatetewa sana na makundi matatu

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
2,000
Katika siasa kuna muda ambao kiongozi anayeingia madarakani huwa anapata uungwaji mkono mkubwa na kuna muda ambao kukubalika kwake hupungua sana. Kwa kutumia mantiki hii ndio maana wataalam wa masuala ya soshologia na uchumi walikubalia ni vizuri kwa kiongozi wa juu ambaye ni mtendaji katika nchi/taifa akawa madarakani kwa muda si zaidi ya miaka 10. Miaka mitano ya kutunga sera na sheria halafu miaka mingine mitano ni kutekeleza sera na sheria.

Kwa mantiki hiyo, kuna muda utawala wa Rais Samia utaanza kukosa uungwaji mkubwa na hapo ndipo tegemeo lake litakuwa kwa makundi ambayo mahusiano yake na yeye ni zaidi ya siasa.

Ninadhani uungwaji mkubwa utapungua kwa haraka sana kama atataka kuridhisha kwa pamoja kila kundi au kuanza siasa za kinafiki!

Kwa kadri muda ulivyoanza kutoa majawabu inaonyesha utawala wa Rais Samia utatetewa sana na makundi makuu matatu nchini ukiondoa ''diehard CCM''. Makundi hayo ni Wazanzibari, Wanawake na Waislam. Haya makundi hayataweza kuona mapungufu ya Rais Samia bali yatatumia dhana iliyojengeka katika fikra zao ya ''kudharauliwa, kutengwa na kubaguliwa'' kama ndio kinga pale Rais Samia atakapokosolewa.

Ni ukweli ulio wazi kuwa Rais Samia 'anatiki' katika mabox haya matatu (Uzanzibari, Uanamke na Uislam) ambayo katika siasa za Tanzania yanahisi hayapewi nafasi ya kuongoza taifa kwa kwa sababu ''yanadharauliwa'', ''yanatengwa'' na ''kubaguliwa''.

Hisia za ''kudharauliwa'', ''kutengwa'' na ''kubaguliwa'' zinayafanya haya makundi kuwa wamoja katika kupambana kwa pamoja na ''adui'' ambaye wanaamini ''anawadharau'', ''anawatenga'' na ''kuwabagua''.

Ukiangalia kwa sasa Wazanzibari wengi kama sio wote wako nyuma ya Rais Samia. Hii sio kwa sababu ni Rais mzuri bali ni kwa sababu ametoka Zanzibar ambako kuna ''hisia'' kuwa Wazanzibari hawatendewi haki kwenye Muungano. Kwa sasa ukimpinga Rais Samia unakuwa kama unawapinga Wazanzibari au unaendeleza dhana ya ''kuwadharau'' ''kuwatenga'' na ''kuwabagua''. Kwa sasa ukichunguza utagundua kuwa, Wazanzibari wengi kama sio wote bila kujali Itikadi zao wako nyuma ya Rais Samia na hawatadiriki kumkosoa hata kama yatajitokeza mapungufu ya kiutendaji.

Kundi la wanawake hasa wanaharakati pia litahakikisha linamtetea Rais Samia kwa nguvu zote huku likitumia silaha iliyotengenezwa na ''hisia ya kudharauliwa kwa kuwa ni wanawake''. Hili kundi halitaona madhaifu ya Rais Samia bali litahakikisha linajenga hoja kuwa wanaomkosoa wanafanya hivyo kwa sababu ni Rais mwanamke ambaye wakosoaji hawaamini kama mwanamke anaweza kuwa ni kiongozi wa juu wa Taifa. Haishangazi kumuona Rais Samia akirudia rudia dhana ya uanamke na madaraka ya juu kwenye mikutano yake ili kujenga picha kuwa kuna watu wanamuona ni dhaifu na hawezi kuongoza nchi kwa sababu ni mwanamke. Hoja hii inajenga dhana ya kichaka cha kuficha mapungufu ya kiuongozi kabla ya kuanza kukosolewa (pre-emptive defence strategy)

Kundi la Waislam hasa wenye kuelekea kuwa na msimamo wa itikadi kali nalo halitabaki nyuma na kama mwanaJamiiforums unataka kujua kwa haraka, utaona kuna ID zitaanza kuibuka sio muda mrefu ili kumtetea Rais Samia sio kwa sababu ni Rais wa Tanzania bali ni mmoja wao kiimani kwa sababu sio kafir! Hili ni kundi ambalo litamtetea sana Rais Samia kwa sababu linaamini kwa imani yake ya kidini atawapa kile ambacho watawala wengine wa nyuma hawakukitoa. Hili ni kundi ambalo halimuoni Rais Samia kama ni Rais wa Tanzania bali ni sehemu ya imani yao katika kutimiza malengo yao.

Wahenga walisema, ''Muda ni mwalimu mzuri''. Muda umeanza kutoa majawabu halisi.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,914
2,000
Huyu mama kachemka mapema sana baada ya kuanza na mifumo ya haki na sheria yeye anaanza na kuhonga Benz.


Mpaka sasahivi miezi 2 ajazindua mradi wowote wa maendeleo

Hata mawaziri wake hawajazindua chochote

Magenge ya ujambazi yameanza watu wapo busy na urais 2025.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,967
2,000
Huyu mama kachemka mapema sana baada ya kuanza na mifumo ya haki na sheria yeye anaanza na kuhongaga Benz.


Mpaka sasahivi miezi 2 ajazindua mradi wowote wa maendeleo

Hata mawaziri wake hawajazindua chochote

Magenge ya ujambazi yameanza watu wapo busy na urais 2025.


Miradi siyo kipaumbele kwa Bi Mkubwa; alimradi masponsa wake wameshiba, yeye anaridhika. Awamu hii ni ya kuwahadaa wananchi kama ilivyofanyika jana kuleee uwanjani. Hivi mwizi wa sokoni na yule wa jana kuna tofauti gani!??? Sanasana huyu wa serikali ni mbaya zaidi maana anatumia cheo alichopewa na rai kuwaibia na kuwahujumu.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,965
2,000
Miradi siyo kipaumbele kwa Bi Mkubwa; alimradi masponsa wake wameshiba, yeye anaridhika. Awamu hii ni ya kuwahadaa wananchi kama ilivyofanyika jana kuleee uwanjani. Hivi mwizi wa sokoni na yule wa jana kuna tofauti gani!??? Sanasana huyu wa serikali ni mbaya zaidi maana anatumia cheo alichopewa na rai kuwaibia na kuwahujumu.
sorry amewaibia akina nani?
 

christeve88

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
1,322
2,000
Nilifurahi sana waziri mkuu akitembelea miradi siku chache zilizopita. Hii miradi inatymia. fedha nyingi inahitaji viongoz wa juu kuwa karibu nayo wakijisahau eidha itachelewa kukamilika au itajengwa chini ya kiwango.
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,143
2,000
Pamoja na article kuwa ndefu ila imejaa "assumptions" na mleta mada bado anasumbuliwa na kivuli cha Magufuli, huenda mleta mada kwa "nature" ya jina lake ni wale ambao wamegoma kuamini kuwa Magu hatuko nae tena!

Tumpe muda, akikosea atakosolewa tu, kama hatukufa kwenye utawala ule basi Mungu ataendelea kusimama nasi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom