Baada ya hisia kuwa kali juu yake nimeamua kumrudia

Lager

JF-Expert Member
Mar 4, 2019
389
1,071
Ndio mimi nilieleta uzi humu ya kuwa nilimuacha lkn hisia juu yake zikiwa bado ni kali sana

Nilijutia kumuacha na nikaona ya nini niumie angali badonampenda!, nimemrudia na mapenzi hivi Sasa ni motomoto. Nimeamua nimkubali hivyo alivyo hisia za kumpenda huyu manzi ni kali sana kumuacha ni sawa na kujitia dosari mwenyewe

Nilichojifunza kwenye mapenzi kabla hujafikia uamuzi wa kumuacha mpenzio jiulize kwanza utaweza kuhimili hisia? Au ndo kabla ya kuruka uagane na nyonga

Kingine usijaribu kuacha unachokipenda bali ishi nacho kwa akili fata unachotaka kwa akili mengine yapo tu. Mwisho kiasi cha utamu wa mapenzi ulichonacho ndo hichohicho kiasi cha maumivu ulichonacho kama mambo yataenda kombo

Niwatakie siku njema ila kupanga ni kuchagua.

Soma mada iliyotangulia: Usijaribu kuacha usichoweza kukiacha, mapenzi yanauma
 
Uweke huo uzi hapa. USIKURUPUKE kuvunja penzi kisha ukaja kujuta baadaye. Tafakari kwa kina.
 
Uweke huo uzi hapa. USIKURUPUKE kuvunja penzi kisha ukaja kujuta baadaye. Tafakari kwa kina.
Itakuwa ni huu wa Grace kuomba msamaha kwa njia ya kumpa mchezo

Shukrani sana 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Itakuwa ni huu wa Grace kuomba msamaha kwa njia ya kumpa mchezo

Tatizo ni kuachana bila sababu za msingi. Kukiwa na sababu za msingi huwezi kujitoa kuachana. Unakuta matatizo madogo ya kawaida mnaamua kuachana badala ya kutafuta ufumbuzi.
 
Hilo bomu la kienyeji linasubiri wanamgambo wa kipalestina walibutue Ndio utajua hujui.
 
Ukichomwa na msumali utahisi maumivu makali sana.......lakini tiba pekee ni kuutoa huo msumali ili upate uponyaji wa kudumu vinginevyo utakusababishia madhara.......lakini kuutoa msumali ulioingia mwilini utapitia maumivu makali sana ambayo yatakufanya ujutie kuutoa huo mwiba.....lakini ukivumilia maumivu ya kuutoa mwiba huo utaishi maisha mazuri na yenye amani tele.......

NB;
Umeanguka kwenye mtihani muhimu kwenye kipimo cha uanaume wako.......huo ni mtihani ambao ungevua kutoka kwenye shati la uvulana na kuvaa koti la UANAMUME........
 
Mwanamke yoyote ukiachana nae halafu ukamrudia, heshima yake kwako inashuka kwa asilimia 70. Muda si mrefu lazima huyo mwanamke atakupiga chini!
 
Tatizo ni kuachana bila sababu za msingi. Kukiwa na sababu za msingi huwezi kujitoa kuachana. Unakuta matatizo madogo ya kawaida mnaamua kuachana badala ya kutafuta ufumbuzi.
Mkuu nimeandika nimemaliza mengine nayajua bianafsi.
 
Ukichomwa na msumali utahisi maumivu makali sana.......lakini tiba pekee ni kuutoa huo msumali ili upate uponyaji wa kudumu vinginevyo utakusababishia madhara.......lakini kuutoa msumali ulioingia mwilini utapitia maumivu makali sana ambayo yatakufanya ujutie kuutoa huo mwiba.....lakini ukivumilia maumivu ya kuutoa mwiba huo utaishi maisha mazuri na yenye amani tele.......

NB;
Umeanguka kwenye mtihani muhimu kwenye kipimo cha uanaume wako.......huo ni mtihani ambao ungevua kutoka kwenye shati la uvulana na kuvaa koti la UANAMUME........
Ni sehemu ya funzo tu Mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom