Baada ya hayati Magufuli kufariki 'mikutano ya injili' imeanza

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
2,420
4,922
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana.

mikutano hiyo huambatana na safari za kuenda nje zisizoeleweka malengo yake. pia hutokea kuingia kwa wageni wengi kuwasili nchini kwa kivuli cha kufanya matamasha ya 'injili'.

safari za wasanii wetu na wa nje kutoka na kuingia nchini pia hushamiri.

wakati huohuo mtaani visa vya matumizi ya dawa za kulevya hushamiri. ulaji wa 'bata' kwa watu wasioeleweka wanafanya kazi gani kwa kipato kipi huongezeka.

kipindi cha dokta magufuli uovu huu ulidhibitiwa sana. China adhabu ya biashara hii ni kifo tu maana ukiwa na taifa la mateja kama nchi huwezi kupiga hatua kimaendeleo. China hayupo tayari kuona anazidiwa na Marekani kiuchumi ndo maana anailinda nguvukazi ya nchi yake kwa kutoa adhabu kali kwa walanguzi wa dawa za kulevya na wahujumu-uchumi wote bila kuangalia ni nani?

enzi za dr. magufuli dawa za kulevya zilidhibitiwa sana. madalali na walanguzi walikiona cha moto.

sasa tunarudi kulekule.

Mungu aunusuru uzao wetu maana yajayo yanasikitisha.

Pumzika kwa amani Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
 
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana...
Una mawazo ya kishamba sana. Hilo ni jukumu la vyombo vya usimamizi, lakini mikutano ya injili au mihadhara haina uhusiani na hicho unachokisema.
 
Hivi ilikuwa kweli yule gwiji Bhonke aliwahi kukamatwa na powder au wivu wawanainjili tu
 
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana...
Kama kutokupiga hatua za maendeleo ni kutokana na kutumia unga, basi Afrika yote ni watumiaji wa unga. Kama unataka kumsifia yule dhalimu na jizi la kura, tumia mbinu nyingine sio hizi.
 
Kuna ukweli hapo....💉lords wamejificha kwenye dini na michezo...walikuwa wanaleta mabox ya vitabu vya dini pamoja na madawa...
 
moja ya dalili ya kuwepo kwa biashara haramu ya unga ni utitiri wa mikutano ya injili ikifanywa na watu wasiokuwa na haiba wala karama ya kuwa wachungaji wala watumishi wa Mungu. dalili zimeanza kuonekana...
Wahubiri ni wanaccm na wasanii ni wanaccm tena wapenzi wa Magufuli

List ni ndefu kwa uchache tu ni hawa

1. Mwinjilist Masanja mkandamizaji
2. Josephat Gwajima
3. Nabii Suguye
4. Nabii GeorDevi
5. Marehemu Lwakatare
6. Na maaskofu wa TAG.

Wasanii

1. Diamondi platinum
2. Alikiba
3. Etc

Unataka kusemaje? Kwamba Magufuli ndiye alikuwa anawatuma hayo madawa ya kulevya?
 
Mzee wa upako
Mwamposya
Bashite
Malekani

Lwakatare ni lango la mlingoti.
 
Mwanza mjini wapo wahubiri wazungu (siwezi kuwatenga kama ni wamarekani, Wayahudi, nk mradi ni weupe) Wanaimba mapambio na kuserebuka wenyewe, pia wanahubiri wenyewe huku wakisaidiwa na wabongo kutafsiri kutoka lugha zao kwenda kiswahili....hawana sehemu maalum ya kuhubiri kwa maana ya vile viwanja maarufu hapana wao wanahubiri stend, gereji, jirani na hospitali, jirani na shule wakati masomo yanaendele, nk. yaani zile sehemu zisizo rasmi unawakuta! Pia wanahubiri muda wowote, jtatu saa moja na dk arobaini asubuhi, niliwakuta eneo jirani gereji za sabasaba barabara ya kwenda Kiseke wakisakata gospo ya Ben Mwaitege (wazungu hao) Pia kuna siku niliwakuta mapema saa mbili asubuhi wapo stand ya Igombe mjini!
Nimejikuta nawaza au wamekimbia covid kwao au wapo wanaisambaza...anyway ujinga na upuuzi sehemu ya kutupa huwa ni Afrika
 
Back
Top Bottom