Baada ya haya, CHADEMA 2015 hakuna kizuizi kuingia ikulu!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Watanzania wapenda mabadiliko asalamu aleikum!

Baada ya kukutana na makamanda wenyeviti na makatibu wote wa Tanzania bara na visiwani (CDM) na kubadilishana nao mawazo, hapa nitaweka mawazo yangu na yale ya baadhi ya makamanda.

1. Kwa sura na uwezo wa wajumbe toka Zanzibar nimepata picha kuwa chama chetu ni dhaifu kuliko hata nilivyofikria kabla kwa upande wa Zanzibar.

2.Chama chetu hakina wananawake imara sana kwa nafasi za kwa nafasi za wenyeviti na makatbu wa mikoa, hapa nazungumzia akina mama kama Suzani Kiwanga ( Moro) na Chiku Abwao (Iringa). Unahitajika mkakati maalum wa kuwshirikisha wanawake katika harakati za chama.

3.Katika moja ya vikao vya ndani ilithibitika kuwa kuna wagombea majimboni ambao tayari wameonyesha nia na sehemu nyingine wameanza harakati za kutoa chochote kukamata majimbo hayo na kuhatarisha umoja wa chama.
Dr Slaa akasema acha waendelee ila muda ukifika wasije kulaumu! Tutafute dawa mapema.

3.M4C ndiyo siraha muhimu kuipeleka CDM madarakani. Operesheni ndogo kama ya Karagwe nilimuona Dr Slaa amesimama kwa zaidi ya saa moja baada ya mkutano kusaini kadi za wanachama wapya. Walipopita makamanda mpaka leo bado bendera zinapepea, hamasa ni kubwa sana . Utengenenezwe mkakati wa haraka wa kupita mikoa yote ambapo m4c haijapita. Muda hauko upande wetu!

4. Mkakati maalum wa watu kujiandikisha katika daftari la kudumu na vitambulisho vya taifa uandaliwe mapema sana na usambazwe nchi nzima na ikibidi uwe wa siri maana kuna hajuma inaandaliwa kutuhujumu kwenye vitambulisho vya taifa.

Nikipata nafasi nitakuja na mapendekezo mengine.

Nawashilisha!
 
Kichwa cha habari, content na mtiririko ni kama umechukua mlenda, nyama ukachanganya na maharage, ukila ni ushuzi tu. Kajipange kutiririka dogo siyo unakula njugu zako na kuja kutujambia humu.
 
Kichwa cha habari, content na mtiririko ni kama umechukua mlenda, nyama ukachanganya na maharage, ukila ni ushuzi tu. Kajipange kutiririka dogo siyo unakula njugu zako na kuja kutujambia humu.
Sasa unam-attack mleta mada kwa lipi? ' A silent fool counted wise'
 
Naunga mkono hoja. Chama chetu bado ni dhaifu sana kwa upande wa Zanzibar although Zanzibar sio ya muhimu sana kwetu kisiasa kutokana na kuwa na population ndogo. Pia future ya muungano wetu haijulikani. Jimbo la Ubungo lina umuhimu mkubwa sana kwetu kisiasa kuliko Zanzibar. So let Zanzibar Go. Kwa upande wa akina mama ni kweli chama chetu bado hakina akina makamanda hodari kama Mdee, Abwao, Kiwanga, Esther Wassira, etc. Pia bado hatujapata support ya kutosha kutoka kwa wanawake. Jitihada za makusudi zinahitajika katika hili. Pia chama kiendelee kuwatumia viongozi wa maeneo husika katika M4C.
 
mpk Kwenye namba hapo ndipo uwezo mkubwa wa Kinana ulipo hapo kujiandaa na wizi wa kura na kuwanyima watanzania vitambulisho .Patachimbika Tanzania ni ya wote
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkono hoja. Chama chetu bado ni dhaifu sana kwa upande wa Zanzibar although Zanzibar sio ya muhimu sana kwetu kisiasa kutokana na kuwa na population ndogo. Pia future ya muungano wetu haijulikani. Jimbo la Ubungo lina umuhimu mkubwa sana kwetu kisiasa kuliko Zanzibar. So let Zanzibar Go. Kwa upande wa akina mama ni kweli chama chetu bado hakina akina makamanda hodari kama Mdee, Abwao, Kiwanga, Esther Wassira, etc. Pia bado hatujapata support ya kutosha kutoka kwa wanawake. Jitihada za makusudi zinahitajika katika hili. Pia chama kiendelee kuwatumia viongozi wa maeneo husika katika M4C.
ni kweli kabisa
 
1. wanawake walio na uongozi ndani ya CHADEMA wabebe jukumu la kuhamasisha wanawake hasa walio vijijini. Wakati wa ziara/ mikutanoya MC4 viongozi wanawake wa wilaya/ mkoa wakishirirkiana na wale wa taifa wao waelekeze nguvu zaidi kukutana na wanawake huko mtaani/ katika vitongoji na kuwaeleza kuhusu CHADEMA (katiba ya CHADEMA inasema nini na mkakati wake katika kuhakikisha haki za raia zinatimizwa). Ikiwezekana viwe ni vikao/ mikutano midogo midogo na huku watakaofanya kazi hii watumie lugha rahisi kueleweka. Hili lifanyike kwa nguvu kubwa maana ukweli ni kuwa wanawake ndio wapiga kura katika nchi hii. Aidha CHADEMA itanmbue kuwa baraza la wanawake wa CHADEMA halijafanya kazi ya kutosha kama ilivyo BAVICHA

2. Viongozi wa wilaya na mkoa wawe na mkakati wa kwao kuimarisha chama ikiwemo kuongeza wanachama kama ilivyo kwa mkoa wa Arusha

3. Iongezwe nguvu ya kuimarisha chama huko Zanzibar na Pemba; tufahamu kuwa hata kama kuna idadi ndogo lakini tufahamu kuwa bado ni sehemu ya Tanzania na CHADEMA haipingi muungano ingawa tunahimiza kurekebisha muundo

4. Kila wilaya iwe na miradi yake ili ofisi ziweze kujiendesha. Hii itasaidia kupunguza mivutano kuwa ofisi ya taifa haigawi ruzuku. Tukumbuke kuwa CHADEMA bado ni changa sana na hatuna uwezesho kama ilivyo kwa CCM ambao wanafursa ya kutumia rasilimali za umma (zilizopo katika halmashauri). Kuwa na vyanzo vya chama vya mapato husaidia chama kuwa na nguvu; tukumbuke kuwa kutegemea wahisani pekee na fundraising events si vyanzo vya kudumu

EJL
 
Mshaurini Dr Slaa amalize shauri lake liliofunguliwa Mahakamani na aliyekuwa Mke wake Rose Kamili nje ya Mahakama kwani ni udhalilishaji kwa wanawake wote labda ndio maana wanakikwepa Chama
 
Kichwa cha habari, content na mtiririko ni kama umechukua mlenda, nyama ukachanganya na maharage, ukila ni ushuzi tu. Kajipange kutiririka dogo siyo unakula njugu zako na kuja kutujambia humu.

Lakini ukweli ndo huo - message sent!
 
Kwanza niombe radhi kwa hoja zangu chokonozi dhidi ya chama chetu pendwa cha CHADEMA.

Kabla ya kuanza likizo yangu nilijaribu kufanya japo utafiti usio rasmi kuhusu siasa za Tz na mstakabali wa CHADEMA kuelekea

2015. Hadi mwisho wa likizo yangu iliyonipisha zaidi ya mikoa minne ya kanda ya ziwa pamoja na dsm nimethibitisha bila

shaka kuwa CHADEMA wataingia ikulu kwa kishindo. Anayebisha amuulize KINANA na NAPE.

Namshukuru Mungu kwani hoja zangu chokonozi dhidi ya CHADEMA zilifanya nikoswekoswe vipigo ktk baadhi ya maeneo hasa Musoma, Bunda , Geita na Kahama.

Kwa heri CCM, karibu CHADEMA 2015!
 
Hizo ndoto ndugu,tena umeota mchana,hivi hizo wilaya 2 ulizopita ndio wana kura za kuitosha chadema kuingia ikulu,
 
Hizo ndoto ndugu,tena umeota mchana,hivi hizo wilaya 2 ulizopita ndio wana kura za kuitosha chadema kuingia ikulu,

Ni kweli hizo ni ndoto maana CCM wasingekuwa wanasaidiwa na vyombo vya dola na wasingekuwa wanaiba kura hapo tungesema ni kweli. Hata hivyo, Mungu ni mkuu anaweza kuwabadilisha Watz wanaonunuliwa kwa pilao na rushwa kukipa ushindi CCM. Kama Chadema hawatateleka (kama baadhi yao walivyoanza kufanya) ni wazi wana nafasi kubwa sana maana wana support kutoka kila sehemu.
 
Nilipoona chadema kuingia ikulu kwa kishindo kwa haraka haraka nikadhani kuna maandamano yanaelekea ikulu baada ya kusoma vizuri kumbe hamna kitu?tumeyamiss maandamano lakini!
 
CCM wanaweweseka tu, waache kila kitu kienda sawa, Tume ya uchaguzi huru nk.....hawashindi uchaguzi!!
Imekufa, sasa inataka kujihalalisha kututawala kwa uji-nga wa kadi iliyoko sandukuni ya DR Slaa!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kwanza niombe radhi kwa hoja zangu chokonozi dhidi ya chama chetu pendwa cha chadema.

Kabla ya kuanza likizo yangu nilijaribu kufanya japo utafiti usio rasmi kuhusu siasa za tz na mstakabali wa chadema kueleke

2015. Hadi mwisho wa likizo yangu iliyonipisha zaidi ya mikoa minne ya kanda ya ziwa pamoja na dsm nimethibitisha bila

shaka kuwa chadema wataingia ikulu kwa kishindo. Anayebisha amuulize kinana na nape.

Namshukuru mungu kwani hoja zangu chokonozi dhidi ya chadema zilifanya nikoswekoswe vipigo ktk baadhi ya maeneo hasa musoma, bunda , geita na kahama.

Kwa heri ccm, karibu chadema 2015!
hata mgonjwa wa ukimwi huwa anakuwa na matumaini labda kesho atapona ..lakini ndo agona agona
 
Back
Top Bottom