Elections 2010 Baada ya hatihati, Chadema yapendekeza wagombea viti maalum

Hatimaye Chadema imepitisha majina ya wabunge 105 wa viti maalumu huku ikiwaacha
wanachama wake 42 walioshindwa kukidhi vigezo vya chama hicho.

Majina ya wabunge hao hayakuwekwa hadharani na badala yake yatapelekwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kabla ya Septemba 30 mwaka huu.

Uteuzi wa majina hayo ulifanywa na mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Mkumbo Kitila, ambaye ni mwanachama wa chama hicho na kuthibitishwa na Kamati Kuu katika kikao chake cha Septemba 25 na 26 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, alisema baada ya matokeo ya wabunge hao ya Julai kufutwa kutokana na mizengwe, Baraza Kuu lilikasimu madaraka kwa Kamati Kuu kufanya uteuzi huo.

“Kamati Kuu ikaunda Kamati Ndogo ambayo ilimtumia mshauri kufanya uteuzi huo akizingatia vigezo vya elimu, uzoefu wa uongozi kisiasa, uzoefu wa uongozi nje ya siasa; ugombea jimboni mwaka huu; mchango katika operesheni za chama na kampeni zinazoendelea na umri ndani ya chama,” alisema Slaa.

Katika vigezo hivyo, aliyeongoza alipata asilimia 94 na wa mwisho 16 ambapo moja ya sababu za kutumika utaratibu huo ambao Dk. Slaa aliuita wa kisayansi, ni kuondoa uswahiba, wagombea kutoka kanda moja na urafiki.

“Tumeondoa dhana ya mtu kuchagua ‘girlfriend (rafiki wa kike)’ wake, na majina haya hatutayatoa hadharani, kwani wengine waliopitishwa wanagombea majimboni,
hivyo kunaweza kuwachanganya wapiga kura,”
alifafanua.

Dk. Kitila alisema katika uandaaji wa vigezo, waliangalia suala la umahiri wa mgombea na kwambambunge atakuwa anawakilisha nchi na kupanua wigo wa ushiriki wa wanawake.

Katika Bunge lililopita, wabunge wa Chadema walikuwa 11 wakiwamo wa majimbo na viti
maalumu na mwaka huu imesimamisha wabunge wa majimbo 185.

wa ndima,tupe basi hata baadhi najua wajua.
 
Where is transparency? halafu wanataka kutawala nchi huku nepotism inawatafuna! Mnaotaka majina ni Mdee, Lucy Ndesamburo, Suzan Lyimo, Mushi, Massawe, Kimaro, Lauwo, Mlaki, Mlay, Swai, Mallya Temu, Mrema et al.

Hawawezi kutangaza sasa wana jua backslash yake wanasubiri muwape kura halafu imetoka hiyo! typical Chaga Democratic Manifesto!
 
Mzee kuwa objective acha ukabila usiokuwa na msingi! wewe nadhani kama sio mtusi basi ni mhutu! usituletea hayo mambo yenu ya kitoto aiseeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
wa ndima,tupe basi hata baadhi najua wajua.

"Tumeondoa dhana ya mtu kuchagua ‘girlfriend (rafiki wa kike)' wake, na majina haya hatutayatoa hadharani, kwani wengine waliopitishwa wanagombea majimboni,
hivyo kunaweza kuwachanganya wapiga kura,"
alifafanua.
 
Where is transparency? halafu wanataka kutawala nchi huku nepotism inawatafuna! Mnaotaka majina ni Mdee, Lucy Ndesamburo, Suzan Lyimo, Mushi, Massawe, Kimaro, Lauwo, Mlaki, Mlay, Swai, Mallya Temu, Mrema et al.

Hawawezi kutangaza sasa wana jua backslash yake wanasubiri muwape kura halafu imetoka hiyo! typical Chaga Democratic Manifesto!

Una umri gani?
 
Transparency does't mean naming the names on public is the way/methods (formula) used to get them.
 
Yuko form five.
Kwa hiyo piga hesabu uone anaweza kuwa na umri gani maana hoja zake ni za daraja hilo!
 
Hapo kama ungekuwa karibu umeshaklula za macho ambazo hazina idadi, unawagusa wasotaka kuguswa hata kama wanagusika kaka.Watakwambia deni halifungi.

Kama ni hivyo itabidi wamvalishe kondom ya ovaroli kwani kuguswa lazima ataguswa. :becky:
 
Chadema kinajulikana ni chama cha kikabila na kina harufu ya udini!!!! Na sasa ndio kifo chake kinakaribia maana kimevamiwa na mambwa waliotajwa na mwalimu nyerere(akina mabere marando) walioimaliza na kuiua nccr-mageuzi ona sasa chadema wameshaanza kugombania madaraka ktk uteuzi wa wabunge na muda si mrefu utasikia wanaanza kupigana makonde!!! Hawa hawana uwezo na nia ya kuleta mabadiliko ni njaa tu inawasumbua!!!!
 
nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri
 
Where is transparency? halafu wanataka kutawala nchi huku nepotism inawatafuna! Mnaotaka majina ni Mdee, Lucy Ndesamburo, Suzan Lyimo, Mushi, Massawe, Kimaro, Lauwo, Mlaki, Mlay, Swai, Mallya Temu, Mrema et al.

Hawawezi kutangaza sasa wana jua backslash yake wanasubiri muwape kura halafu imetoka hiyo! typical Chaga Democratic Manifesto!

Transparency ... my foot!

Hivi kama CCM wangekuwa wako transparent, CC na NEC wangekata majina ya walioshinda kwenye kura za maoni? Muulize Bashe, Prof. Kahigi, Mwakalebela, Mzee Nyimbo na wengineo kibao ambao hiyo transparent yako ilifanya kazi. Haina maana yoyote kuruhusu watu wapige kura za maoni, halafu CC na NEC iende kuchakachua matokeo.

Transparency ingeanza na kujadili majina ya waliojitokeza kugombea, wenye kasoro zao wakatwe mapema au waambiwe matatizo yao na kama wanaweza kuya-fix waya-fix mapema. Once mtu akishashinda kwenye kura za maoni inakuwa imetoka. Sasa unaacha watu wapige kura za maoni, halafu baada ya hapo unaenda na hoja nyepesi ku-justify kufyeka majina ya washindi. Hiyo ndio transparency?
 
Chadema kinajulikana ni chama cha kikabila na kina harufu ya udini!!!! Na sasa ndio kifo chake kinakaribia maana kimevamiwa na mambwa waliotajwa na mwalimu nyerere(akina mabere marando) walioimaliza na kuiua nccr-mageuzi ona sasa chadema wameshaanza kugombania madaraka ktk uteuzi wa wabunge na muda si mrefu utasikia wanaanza kupigana makonde!!! Hawa hawana uwezo na nia ya kuleta mabadiliko ni njaa tu inawasumbua!!!!

CHADEMA ingekuwa inakaribia kufa wala wasingeteua majina 105 ya wagombea wa Viti Maalum. Sasa hivi wagombea wa viti maalum kupitia CCM na hasa wale walioshika nafasi ya pili kwenye mikoa yao, matumbo yako moto, maana hawajui kama watauona mjengo mwaka huu.
 
Nccr ilikufa kwa vile lyatonga nae alikuwa ccm, pia alikuwa mkiti dhaifu. Marando mmoja ni nani hadi awe na uwezo wa kuhujumu chadema?
 
Back
Top Bottom