Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Kada Mbowe sasa kupitia kihunzi kingine kesho jijini Mwanza baada ya gwaride na hafla ya kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika tarehe 9 Disemba 2019.
Baada ya shamrashamra hizo atakuwa kwenye usaili utakaoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole, Matokeo ya usaili huu ndio idhini ya mwisho kabla ya kwenda kwenye kupigiwa kura za ndio au hapana.
Kwa haraka haraka maswali yatajikita kwenye maeneo yafuatayo; utekelezaji wa Chadema kwa miaka mitano iliyopita,mikakati ya Chadema miaka mitano ijayo.
Ukiangalia juu juu unaweza kufikiri ni maswali rahisi lakini vipengele vidogo vidogo huenda vikaleta vigugumizi.
Yote kwa yote tunamtakia mafanikio kwani hadi sasa yeye ndiye mwenye uchungu na chama kuliko mwingine yeyote na huenda hili likambeba.