Baada ya Fareed kujiteka na kisha kujirudisha kwake ukweli wabainika ya Mbagala

mmh, sishangai

maana haya maanadamano hayaeleweki, mara kiwanja kirudishwe mara mtoto kakojolea nini.

Basi maruwe ruwe tupu

kuna baadhi ukiwauliza kwa nini wanaandamana hawawezi ata kukupa jibu la kueleweka,yani bora liendee kama vile bendera fuata upepo.
 
Ninachojua mimi ni kwamba sio waislam wote wanapendezwa na fujo zinazoendelea hapa nchini. Hiki ni kikundi cha wahuni wachache wanaotumia mgongo wa dini kufanya fujo kwa maslahi yao. Hii inadhihirika kutokana sababu zinazotolewa kwamba ndio chanzo.

Hapa tunatakiwa kuwa makini tusije tukaingia mtegoni. Kwani uislam umeanza leo hapa nchini? Miaka yote tumeishi kwa amani na upendo pamoja na shida zetu zinazotuzonga,iweje leo ndio waislam waone wananyanyasika. Kama ni umasikini unatuhusu wote wenye dini na wasiokuwa na dini.Neema wanayo mafisadi tu wote wenye dini na wasio na dini(kama wapo!) Tunashindwa kupigana na ufisadi tumeanza kuchukia majirani zetu ambao wote tunashindia mlo mmoja,hii ni akili kweli! Hivi wanoshabikia ujinga huu walishawahi kwenda vijijini mbali huko wakaona wananchi wanavyohangaika na ugumu wa maisha? Kule watu hawajui hata hizi dini tunazibishania hapa! Tena kama kweli kuna nia njema ya ukombozi mimi naona ingelenga kukomboa wananchi hawa, maana sasa wao anawasemea nani,huu si ndio ubinafsi wa dhahiri kabisa! Halafu kwanza sijajua hawa watu wanapambana na nani sasa. Wananapambana na wakristo au hata waio wakristo? na ikiwa ndio hivyo amani ikivujika wasiokuwa wakristo nafasi yao iko wapi. Mimi naamini haya sio mafunzo ya kiislam, na hapa waislam wanatakiwa kuwa makini, wasije wakakubali kutumika kama rubber stamp ya kuruhusu hiki kikundi cha wahuni kutuharibia hali ya hewa.

Huu ni uhuni tu ndugu zangu,tuweni macho tusije tukapotea. Tunatakiwa kujiuliza ikiwa amani itaondoka je ni wakristo tu ndio watakaopoteza,au je ni kweli kwamba ndiyo itakuwa suluhu ya shida za waislam? Tunapokwa tunafikiria kuanzisha fujo,tusisahau pia kuwa nyumbani mwetu tuna watoto wadogo wanaotegemea ulinzi wetu.Tunao akina mama wasiojiweza,wengine wajawazito wengine wagonjwa, wote hawa wanatutegemea. Tusiangalie upande mmoja tu,hebu tujaribu kuangalia na upande wa pili. Halafu tuwe na busara japo kidogo, unapodai haki unatakiwa pia kutimiza wajibu wako! Je,ulinzi wa familia zetu tunauweka wapi tunapotaka kuchafua hali ya hewa.Je,tumewaanda vipi watoto wetu na wazee wetu kujihami ikiwa amani itatoweka?Tumewaandalia wapi pa kukimbilia? Tuache masikhara jamani. Hii nchi ni yetu sote,walio na dini na wasio na dini.

Malumbano ndani ya Jamii forums yasitufanye tukapandwa na jazba na kufanya mambo ya ovyo,kwa sababu hata humu hao wahuni wanafika na kueneza propaganda zao chafu. Hata hivyo pamoja na kwamba nimechangia post hii,bado sina imani na mtoa mada. Inaonekana habari yake ina sura ya kuamsha hisia mbaya kwa waislam,ni kama imekaa kiuongo uongo maana mtoa mada hajatoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukweli wa habari yake.

Ubarikiwe ndg yangu,tutauwana tukijidai tunamtetea Mungu,halafu mwisho wa siku wote anatutupa jehanam ya moto.Binadamu hawezi kumtetea Mungu,ni yeye ndo hututea sisi.
 
kwa wanaokanusha kuwa huu ni uzushi waje na facts tu kuwa nyumbani kwa mtoto aliyekojolea kowani ni hapa, wazazi wake ni hawa hapa anatokea huku, anasoma hapa na mengine ili kujua kuwa habari hii imepikwa au ni kweli
kuishia kusema tuu ni uzushi haisaidii, ambayo siyo uzushi ni nini?
 
Hii movie ya sheikh wa uamsho kujiteka na kujiachia huru inanikumbusha mbali kwenye michezo ya kitoto. Kuna mchezo ambao mtoto mmoja anajificha na wenzake wanamtafuta, wakishindwa kumpata anajitokeza mwenyewe. Dhana nzma ya yeye kujificha na wenzie kumtafuta naifananisha na mchezo huo, wahusika wote hapa ni watu wazima ila wakati mwingine umri wa mtu hauangaliwi kwa tarakimu ya miaka au wingi wa ndevu bali matendo ya mtu.
 
Ninachojua mimi ni kwamba sio waislam wote wanapendezwa na fujo zinazoendelea hapa nchini. Hiki ni kikundi cha wahuni wachache wanaotumia mgongo wa dini kufanya fujo kwa maslahi yao. Hii inadhihirika kutokana sababu zinazotolewa kwamba ndio chanzo.

Hapa tunatakiwa kuwa makini tusije tukaingia mtegoni. Kwani uislam umeanza leo hapa nchini? Miaka yote tumeishi kwa amani na upendo pamoja na shida zetu zinazotuzonga,iweje leo ndio waislam waone wananyanyasika. Kama ni umasikini unatuhusu wote wenye dini na wasiokuwa na dini.Neema wanayo mafisadi tu wote wenye dini na wasio na dini(kama wapo!) Tunashindwa kupigana na ufisadi tumeanza kuchukia majirani zetu ambao wote tunashindia mlo mmoja,hii ni akili kweli! Hivi wanoshabikia ujinga huu walishawahi kwenda vijijini mbali huko wakaona wananchi wanavyohangaika na ugumu wa maisha? Kule watu hawajui hata hizi dini tunazibishania hapa! Tena kama kweli kuna nia njema ya ukombozi mimi naona ingelenga kukomboa wananchi hawa, maana sasa wao anawasemea nani,huu si ndio ubinafsi wa dhahiri kabisa! Halafu kwanza sijajua hawa watu wanapambana na nani sasa. Wananapambana na wakristo au hata waio wakristo? na ikiwa ndio hivyo amani ikivujika wasiokuwa wakristo nafasi yao iko wapi. Mimi naamini haya sio mafunzo ya kiislam, na hapa waislam wanatakiwa kuwa makini, wasije wakakubali kutumika kama rubber stamp ya kuruhusu hiki kikundi cha wahuni kutuharibia hali ya hewa.

Huu ni uhuni tu ndugu zangu,tuweni macho tusije tukapotea. Tunatakiwa kujiuliza ikiwa amani itaondoka je ni wakristo tu ndio watakaopoteza,au je ni kweli kwamba ndiyo itakuwa suluhu ya shida za waislam? Tunapokwa tunafikiria kuanzisha fujo,tusisahau pia kuwa nyumbani mwetu tuna watoto wadogo wanaotegemea ulinzi wetu.Tunao akina mama wasiojiweza,wengine wajawazito wengine wagonjwa, wote hawa wanatutegemea. Tusiangalie upande mmoja tu,hebu tujaribu kuangalia na upande wa pili. Halafu tuwe na busara japo kidogo, unapodai haki unatakiwa pia kutimiza wajibu wako! Je,ulinzi wa familia zetu tunauweka wapi tunapotaka kuchafua hali ya hewa.Je,tumewaanda vipi watoto wetu na wazee wetu kujihami ikiwa amani itatoweka?Tumewaandalia wapi pa kukimbilia? Tuache masikhara jamani. Hii nchi ni yetu sote,walio na dini na wasio na dini.

Malumbano ndani ya Jamii forums yasitufanye tukapandwa na jazba na kufanya mambo ya ovyo,kwa sababu hata humu hao wahuni wanafika na kueneza propaganda zao chafu. Hata hivyo pamoja na kwamba nimechangia post hii,bado sina imani na mtoa mada. Inaonekana habari yake ina sura ya kuamsha hisia mbaya kwa waislam,ni kama imekaa kiuongo uongo maana mtoa mada hajatoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukweli wa habari yake.

sema nipo mobile ningegonga bonge la LIKE mi muislam ila sikubali vurugmu wala uchochezi, hata walioiba na kuchoma makanisa sina imani kama ni waislam au wahuni
 
Jamani hapa naona kuna ukweli mbona hawakuonesha hiyo quran iliyokojolewa?
Vp kwanini hawakuchoma makazi ya yule mtoto wakakimbilia makanisa?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom