Baada ya DSTV kujichanganya kwa bei kubwa ya World Cup, AzamTv ni nafasi yenu hii kututangazia World Cup bei chee

Azam anatuonyesha ligi ya France League 1 tunaiona PsG ya kina Neymar&Messi, azam anatuonyesha Bundesliga tunaiona Bayern Munich ya kina Sadio Mane, Dortmund na mechi kibao kila wiki, bado azam anaonyesha ligi ya ndani NBC bado azam anaonyesha mechi moja ya Epl bure kila jumamosi, lakini bado Pia tunayaona mashindano ya CAF
Huyo ndo mshindani halisi wa Dstv hapa Tz startimes ni takataka mbele ya azam, mtu mwenye akili timam hawezi kwenda kununua startimes kwa matarajio ya kupata burudani zaid ya burudani inayotolewa azam
Fact...

Labda kama sio mtumiaji wa StarTimes Tanzania ndo huwezi kuelewa maumivu tunayopata wateja wake ambao ni wapenda soka....
 
DStv jana wamezindua ofa yao ya kombe la dunia ambapo ili uone mechi zote 64 mubashara utahitaji ulipe kifurushi cha Compact ambacho ni shilingi 56,000.

Ndugu zetu, wazalendo wenzetu AzamTv huu ndiyo muda wenu wa kuibuka na kututangazia Watanzania kuwa mtaonesha kombe la dunia kwa bei nafuu.

AzamTv amkeni kutoka kwenye usingizi mzito, njooni mjichukulie alama 3 muhimu
Mkuu, usihangsike na hao kasuku wa EPL. TBC1 ndo tulizo la moyo wako kombe la dunia la FIFA, tena bure kabisa.
 
Wewe ni arrogant na huna uelewa wa aina yoyote katika exclusive rights za kurusha matangazo ya televisheni. Unajua haki utolewa kwa masharti gani? Nikikuuliza kwanini StarTimes na Dstv hawaonyeshi ligi kuu Tanzania sijui utajibu nini

Star times ama dstv wananunua content zinazoleta faida kwao. Ligi ya Tanzania kwao haina faida. Maana inafatiliwa na wa Tanzania tu. Huku wao wanarusha nchi nyingii content zao
 
Azam Tv alivyo mkuda,hata channels za taifa zitakazoonesha mechi kwa uchache ataziondoa.

56K ni reasonable kama ni mechi zote,mchawi abaki Makamba tu.

Sio mkuda.. sheria ya maudhui inambana kurusha kitu ambacho hana haki nacho. World cup sio mali ya azam.. haruhusiwi kurusha mpaka anunue haki ya kurusha
 

Attachments

  • 1666634610347.jpg
    1666634610347.jpg
    88.5 KB · Views: 11
DStv jana wamezindua ofa yao ya kombe la dunia ambapo ili uone mechi zote 64 mubashara utahitaji ulipe kifurushi cha Compact ambacho ni shilingi 56,000.

Ndugu zetu, wazalendo wenzetu AzamTv huu ndiyo muda wenu wa kuibuka na kututangazia Watanzania kuwa mtaonesha kombe la dunia kwa bei nafuu.

AzamTv amkeni kutoka kwenye usingizi mzito, njooni mjichukulie alama 3 muhimu
Litaonekana TBC bureee
 
Yaani unamaanisha TBC ina pesa kuliko Azam, company yenye brand nyingi Tanzania?
Fifa Wametoa Idhini ya Kila serikali ambayo nchi yake ni Mwanachama wa Fifa kwamba watapewa Ofa ya Local channel moja kurusha mechi zisizozidi 32 (Nusu ya idadi ya mechi zote)
Sasa hapa kwetu ni TBC ndiyo Kituo cha serikali kwa hyo imebahatika...
 
TBC wanawezaje kuonyesha world cup?
Unafahamu hakuna TV company hata moja yenye thamani hiyo hapa Africa?
Unapaswa kufahamu Kwamba kila nchi mwanachama wa FIFA imepewa ofa ya Local Channel 1 ya kuonesha angalau nusu ya idadi ya mechi kwa gharama nafuu TBC ndiyo wameponea hapo.
 
Back
Top Bottom