Baada ya Dr. Slaa kufunua nyongeza; Sheria ya "mbwembwe" ni batili?

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
BAADA ya Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kuibana serikali kuhusu vipengele vilivyoongezwa kinyemela katika muswada uliosaniwa na Rais Jakaya Kikwete kwa mbwembwe wiki iliyopita, taarifa mpya zinasema Rais amefura, akitaka maelezo ya kina ya walioingiza vipengele hivyo.

Tanzania Daima lilipozungumza na mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete kuhusu sakata hilo jana, alidokeza kwa maneno machache, na kwa msisitizo, akisema: "Rais amefura."

Kwa habari zaidi, Soma Tanzania Daima.
 
Nimependa ulivyoweka habari! Tumezoea wale wenzetu wanakopi gazeti zima na kumwaga hapa! Hivi JMK huwa anamuda wa kusoma anachosign? ama mwenzetu ni ceremonial president?

attachment.php
 
Hizo ni dalili mbaya sana kwa uongozi mzima na Idara ya usalama wa Taifa, hivi hawa jamaa wa UWT wanakubali vipi kitu ambacho raisi keshakisaini kije kugushiwa na kiingie kwenye Public bila wao kujua, ina maana kuna wanasiasa wana ujanja na uwezo kuliko wao?
 
BAADA ya Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kuibana serikali kuhusu vipengele vilivyoongezwa kinyemela katika muswada uliosaniwa na Rais Jakaya Kikwete kwa mbwembwe wiki iliyopita, taarifa mpya zinasema Rais amefura, akitaka maelezo ya kina ya walioingiza vipengele hivyo.
Tanzania Daima lilipozungumza na mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete kuhusu sakata hilo jana, alidokeza kwa maneno machache, na kwa msisitizo, akisema: “Rais amefura.”
Kwa habari zaidi, Soma Tanzania Daima.
Janja ya uchaguzi...............
 
Nachelea kuamini siku moja watamchomekea a sign kwa mbwembwe, urais wangu nimemwachia Lowa Saa
 
Siku muswada unajadiliwa bungeni, Werema (AG) aliwaonya wabunge kuwa yeye alikuwa jaji. Hivi naye hakupata nafasi ya kuusoma kabla ya kuuwasilisha kwa rais? Rais anatakiwa kuonyesha njia kwa kumwajibisha aliyehusika na si kuishia kufura tu!
 
Nimependa ulivyoweka habari! Tumezoea wale wenzetu wanakopi gazeti zima na kumwaga hapa! Hivi JMK huwa anamuda wa kusoma anachosign? ama mwenzetu ni ceremonial president?

attachment.php
I love this post! Hiyo Chaque kwa maneno imeandikwa Two Hundred Thousand lakini kwa mahesabu 300,000! Kama sio doctored hii itakua ya mwaka! Manake muungwana anafurahia bila hata kusoma! Hii kali!!!
 
I love this post! Hiyo Chaque kwa maneno imeandikwa Two Hundred Thousand lakini kwa mahesabu 300,000! Kama sio doctored hii itakua ya mwaka! Manake muungwana anafurahia bila hata kusoma! Hii kali!!!
nimeipenda pia hiyo picha, hiki kilikua kielelezo cha Rais asiemwangalifu na aliezungukwa na wasaidizi wenye mwenendo wa maisha usio wa kawaida.....kuna wakati lakini naona huwa wanamuacha aumbuke kwa sababu labda mkuu nae ana simple mind, ama simuelewa wa mambo ama akili yake ni nzito.
 
I love this post! Hiyo Chaque kwa maneno imeandikwa Two Hundred Thousand lakini kwa mahesabu 300,000! Kama sio doctored hii itakua ya mwaka! Manake muungwana anafurahia bila hata kusoma! Hii kali!!!

Mwanetu huyu Dr. Muungwana hana muda wa kusoma. Ndio maana masaibu haya yanamfika. Kusign sheria kwa mbwembwe na kupokea cheki kwa mbwembwe ndio zake.
 
Guys, this is hilarious... naona mkuu wameshamgeuza bibi!!! Someone or some people have to go!!! Yaani na mbwembwe zote zile?
 
i love this post! Hiyo chaque kwa maneno imeandikwa two hundred thousand lakini kwa mahesabu 300,000! kama sio doctored hii itakua ya mwaka! Manake muungwana anafurahia bila hata kusoma! Hii kali!!!

uzuri hakusign yeye hiyo cheque...otherwise zingekuwa zile za bot!!!!!!!
 
Unajua nini, maofisa wa Ikulu kila siku humuweka Dr Jakaya kwenye matatizo alwayz husema mambo yote yako safi kumbe wameshafanya usanii kibao.Mnakumbuka ambulance, mtu akitwa kuchukua gari wakati sio mhusika.Hiii real ni aibu kubwa sana kwa Taifa.Tuwe makini jamani na kila jambo lina taratibu zake.
 
BAADA ya Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa kuibana serikali kuhusu vipengele vilivyoongezwa kinyemela katika muswada uliosaniwa na Rais Jakaya Kikwete kwa mbwembwe wiki iliyopita, taarifa mpya zinasema Rais amefura, akitaka maelezo ya kina ya walioingiza vipengele hivyo.
Tanzania Daima lilipozungumza na mmoja wa wasaidizi wa Rais Kikwete kuhusu sakata hilo jana, alidokeza kwa maneno machache, na kwa msisitizo, akisema: “Rais amefura.”
Kwa habari zaidi, Soma Tanzania Daima.
katika Yoote, Dr Slaa anasoma sana, ni makini mno, ....binafsi na muheshimu sana.
 
Hiyo habari ya cheki ilishajadiliwa sana hapa JF mwaka 2008 na Ikulu nafikiri walikubali hilo kosa. Hiyo thread ipo hapa hapa JF na ilikuwa vituko kweli kweli. Hata magazeti yaliinasa na kuiandika.
 
Back
Top Bottom