Uchaguzi 2020 Baada ya Dkt. Kigwangalla kujibizana na Mo Dewji Twitter. Dkt. Bashiru amshukia Kigwangalla, amtaka am-tweet Dkt. Magufuli

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla kumzungumzia Mgombea wa Urais wa CCM, Dkt. Magufuli badala ya kuendelea na malumbano yake yanayohusu mpira dhidi ya Mmiliki wa Simba SC, Mohammed Dewji.

Dkt. Bashiru amaema“Naona Hamis Kigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na Mohammed Dewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda.”

Ameongeza, “Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM".

Dkt. Kigwangalla na Mo Dewji walianza kujibishana mtandaoni baada ya Kigwangalla kuhoji namna alivyopatikana CEO mpya wa Simba ambaye anaelewa kuwa PA wa Mo Dewji.

Katika kujibu hoja hiyo Mo aliendelea hadi kumuomba msamaha Waziri Kigwangalla kutokana na mkopo wa pikipiki kutofanikiwa (hali iliyotafrisiwa kuwa Mo anadhani Kigwangalla anafanya hivyo kutokana na kunyimwa mkopo).

Hata hivyo, Kigwangalla aliendelea na kusema mkopo hauhusianj bali tu yeye anahoji kama Mwanachama wa Klabu ya Simba. Aliweka bayana barua pepe aliyoombea mkopo wa pikipiki na pia alionesha tweet zake za nyuma ambazo pia alikuwa a ahoji mambo kadhaa ndani ya Simba.


85964FB6-F44E-4AB7-9794-81654EC0BA7D.jpeg
 
"Naona Ndg HKigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na @moodewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda.Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM"NdgBashiru https://t.co/Ftf8f0WpdF
Rangi hizo zinaonekana katika uhalisia wake sasa
 
"Naona Ndg HKigwangalla yupo mitandaoni kujibizana na @moodewji mambo ya mipira, tupo kwenye uchaguzi. Nataka nione ana-tweet na wafuasi wake namna Mwenyekiti na Mgombea Urais wetu atakavyoshinda.Siingilii maisha binafsi, hakuna maisha binafsi unapokuwa mgombea wa CCM"NdgBashiru https://t.co/Ftf8f0WpdF
Dr Kigwangalla yuko sahihi Mo Dewji alipe sh bilioni 20 za Simba.

Maendeleo hayana vyama!
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Bashiru Ally mchana wa leo ametoa maelekezo kwa wagombea wa Ubunge kubaki katika maeneo yao ya jimbo na kufuata maelekezo na taratibu zilizopangwa na Kamati za Siasa za Wilaya husika.

Katibu Mkuu amewataka wabunge kuzingatia ratiba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ratiba za Kamati za Siasa za Wilaya kuungana na Viongozi wengine kuwatafutia Kura wagombea Udiwani pamoja na kumuombea Kura mgombea Urais wa CCM Ndugu John Pombe Magufuli.

Sambamba na maelekezo hayo, amewataka wabunge kutumia mitandao ya kijamii katika kutafuta kura za Chama Cha Mapinduzi kwa kufafanua ilani yetu ya Chama kwa mwaka 2020- 2025 kwa kuwaeleza wananchi kipi kimetekelezwa na kipi tunatarajia kukitekeleza pamoja na kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura siku ya tarehe 28 Oktoba 2020.

Nidhamu ya Chama inatuongoza kusikiliza maelekezo ya Viongozi wetu na bila kinyongo kuyatii na kujisahihisha.

Tunasema tumesikia na tumetii...!

WhatsApp Image 2020-09-06 at 15.51.26.jpeg
WhatsApp Image 2020-09-06 at 15.51.26.jpeg
WhatsApp Image 2020-09-06 at 15.52.43.jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2020-09-06 at 15.51.29.jpeg
    WhatsApp Image 2020-09-06 at 15.51.29.jpeg
    24.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom