Baada ya dirisha la usajili barani Ulaya kufungwa haya ndiyo niliyoyaona

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kufuli la chuma, ufunguo wa Chuma na Dirisha la chuma. Kila kitu kimefungwa tayari tangu ile mida ya usiku wa saa sita na dakika sifuri usiku wa kuamkia leo. Dirisha kubwa la usajili lilifungwa hapo jana, kila mtu alivuna alichopanda.

Aaah! mara nyingi huwa nakosaga amani ikifikaga siku ya mwisho ya usajili, kuna mambo ya ajabu huwa yanafanyika hadi kubakia mdomo wazi, mara nyingi huwa kuna vimbwanga pale.

Unataka habari gani ucheke? Eric Choupo-Moting kujiunga Bayern Munich siku ya mwisho? ana bahati sana yule, kutoka Schalke O4, Stoke City, PSG mpaka Bayern Munich. Miujiza. Douglas Costa amerudi kwa mkopo pale.

Alex Telles, mbrazil mmoja mhuni anapiga kazi sana, ni mwekundu kwanzia sasa anaungana na Edinson Cavani pale kwenda kufanya kazi moja tu, kumtoa Luke Shaw kibonge pale mbavu ya kushoto na kuingia yeye.

Yule Michael Cuisance ambaye Leeds walimtaka kwa hali na mali kutoka FC Bayern Munich amekwenda Olympique de Marseille kwa Manuel Macron kule.

Ruben Loftus-Cheek. Mnakumbuka Hat-trick yake Europa League lakini? alikuwa bora sana yule, akaenda kuumia kule Marekani, wanachelsea wakawa wananiambia yule mwamba akipona, Mason Mount atafute chaka lake la kujificha.

Aliporudi. Hatukujua anacheza nini? jana amepelekwa Fulham pale kwa mkopo, Lampard anapunguza waingereza, hii ni baada ya Ross Barkley kwenda Aston Villa pale na kuhusika katika kifo cha jogoo la Merseyside.

Matteo Guendouzi unamkumbuka? kijana mdogo sana, amekwenda pale Hertha Berlin, nimefurahishwa na usajili huu, akapige shughuli ya maana pale kwa wajerumani akirudi apige mzigo kama kawaida, amepewa jezi ya uhakika. Namba 8.

Unamjua Thomas? Unamfahamu Partey? wana gunners wanakwambia No Thomas no Partey! wana sifa sana majamaa wa London, Guendouzi kampisha pale huyu mtu wa kazi, wanakwambia bado yule Houssem Aouar bado watamchukua Januari pale Olympique Lyon.

Theobald Walcott. Unamkumbuka vizuri? kijana mmoja aliyekuwa ananyoa low cut kama T.I pale Arsenal, tulimtabiria makubwa sana na jezi ya Thierry Henry namba 14. Umemkumbuka vizuri? yupo Southampton pale kwa sasa kutoka Everton.

Ukoo wa mzee Sarr naona unafuata mkumbo wa ukoo wa mzee Mendy pale Ulaya ambao umewajaza vijana kama Nampalys Mendy pale Leicester City, Benjamin Mendy pale City of Manchester, Edouard Mendy pale Chelsea na Ferland Mendy pale Bernabeu.

Kuna Sarr mwingine amejiunga pale Bayern, anaitwa Bouna Sarr anautangaza ukoo wa mzee Sarr baada ya Malang Sarr na kipenzi cha wana Liverpool, Ismaila Sarr.

Hivi ndivyo komeo la usajili lilivyofungwa kibabe, unaweza kulala maskini ukaamka tajiri. Maisha ni kuchagua, tukutane uwanjani.
 
Hii ndo reality ya gemu , Historia inaonyesha man u tukipigwa Gori sita lazima tunyenyue kwapa
Duh hivi una uhakika gani na hyo miujiza yako kutokea?.... Kwa kawaida bingwa wa EPL anafungwa mechi 3 au 4 ..Manchester mmeshafungwa mechi 2 mpk sasa bado hamjakutana na Leeds ya yule babu bielsa na timu zingine tishio unaona unaweza kuzuia usifungwe mechi 2 hapo? Acha mawazo uchwara
 
Mechi mbili sio nyingi
 
Wewe ndy unamawazo uchwara,aliyekuambia bingwa wa EPL huwa anafungwa mechi mbili Nani?? Ferguson kachukua EPL Mara kibao akiwa kafungwa mechi 5 the same to Pep msimu wa mwaka juzi kabeba EPL akiwa kapoteza mechi 5 so usitudanganye
 
Nani kasema mechi 2 ...umeelewa nilichoandika...nimesema 3 au 4 ...na hyo km average. Tu ..we jipe matumaini eti mechi 5 uchukue ubingwa...pale man u hamna timu ya kuchukua EPL
 
Pep msimu wa mwaka juzi kabeba EPL akiwa kapoteza mechi 5 so usitudanganye

Pep amechukua ubingwa 2017/18 akiwa na points 100 out of 114.

Pep amechukua ubingwa 2018/19 akiwa na 98 points out of 114.

Kupoteza game 5 ni 15 points, ukiweza na draws...!

Unazungumzia msimu upi?
 
Pep amechukua ubingwa 2017/18 akiwa na points 100 out of 114.

Pep amechukua ubingwa 2018/19 akiwa na 98 points out of 114.

Kupoteza game 5 ni 15 points, ukiweza na draws...!

Unazungumzia msimu upi?
Msimu ambao pep alipoteza mechi 5 alichukua ubingwa pia
 
Back
Top Bottom