Baada ya dhiki ni faraja; vimbwanga vya wauza korosho baada ya mauzo lindi na mtwara

Ni kwamba tofauti na matarajio;
  • baada ya kulipwa pesa za korosho wengine wameongeza wake,
  • Baada ya kuuza korosho wengine wametapeliwa na vimada,
  • Baada ya kuuza korosho wengine hawajarudi makwao hadi hivi sasa,
  • Baada ya kuuza korosho wachache wamekumbuka kufanya maendeleo,
  • Baada ya kuuza korosho wengi wameparamia kununua RADIO KUBWA zile PANASONIC na sambufa wakicheza na kuruka,
  • Baada ya kuuza korosho wananywesha SODA hadi mbuzi na kuwavisha miwani kama ishara ya U-doni,
  • Baada ya kuuza korosho wananunua hadi madela ya kuvalisha mbuzi wao.
  • Baada ya kuuza korosho mabasi kama BUTI LA ZUNGU,MANING NICE yanaendelea kushusha warembo wa kila aina kuja kuhakikisha mkulima wa korosho anarudi shambani mapema iwezekanvyo...
Ingesaidia sana kama ungeweka uthibitish wa picha kwa kila point hapo juu. La sivyo tutachukulia ni uzushi au utani
 
Ahahah,,nimecheka hapo MABASI ya buti la zungu na MANING NICE yanashusha warembo kwa wingi tokea Daresalaam ili kuhakikisha wakulima wanarudi mashambani haraka,, haahah,, kwaiyo wawapune fedha zote ili wawai mashambani
Na wanawapuna kwelikweli.
 
Miji niliyokutajia ni aghalabu sana kuona sura hizo. Wamekuja kwa malengo maalum, wakishagonga target haooooo, kuonana September/October kwenye msimu unaofuata.
 
Mkuuu Kuna Wasafi Vestival Jumamosi tarehe 24/11 kiiingilio buku 10, Mondi ataijaza Nangwanda maaana Mtonyo wa Korosho uko kibao na Wanakuchele wamepania haswaaaaa, wadangaji washajaza Lodge ni kujisevia tuuu. Ntwara hiii wanajua matanuzi we acha tuu
 
Aliyekuambia nilienda kulima korosho nani na una uhakika gani sikutumia fursa?mwenzio niliwekeza malengo ya lipo tumia nikarudi zangu mwanza kuendesha shughuli zangu
Haa sawa hawa wasukuma, wengi walienda kule kusini, hasa maeneo ya Rwangwa na Nachingwea.

Ila wakaferi madini hakuna, wengi walitumikishwa sana, wengine wakaolewa kule, Walikua wakijulikana, wakitembea vichwa huinamia chini kwa mawazo.

Nadhani kati ya miaka ya 2003 hadi 2004. Kipindi hicho nilikua nafanyia kazi zangu Nachingwea.
 
Haa sawa hawa wasukuma, wengi walienda kule kusini, hasa maeneo ya Rwangwa na Nachingwea.

Ila wakaferi madini hakuna, wengi walitumikishwa sana, wengine wakaolewa kule, Walikua wakijulikana, wakitembea vichwa huinamia chini kwa mawazo.

Nadhani kati ya miaka ya 2003 hadi 2004. Kipindi hicho nilikua nafanyia kazi zangu Nachingwea.
Kawaida sana ndiyo maisha hayana formula
 
Back
Top Bottom