Ama kweli mwenzenu nimethibitisha laivu zile semi za wahenga
"baada ya dhiki ni faraja, pesa sabuni ya roho, pesa mwana haram!, mipango siyo matumizi, pata pesa tujue tabia zako"
mimi kama mfanya biashara tangu niliposkia MTWARA NA LINDI KUCHERE! niliwahi fasta kutafta fursa.
Baada ya kufika huku nimejifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wakulima wa korosho...........
kikubwa nilichogundua wakulima wengi wana mashamba ya kurithi kwa maana hiyo hawana uchungu na faida ya zao hili, wanafanya tu almradi, heka moja ya korosho wanaambulia 1M, shamba zuri kidogo wanavuna hadi 1.5M,....
Kwa wachache wenye mashamba makubwa ya hekali zaidi ya 30 ndiyo wanaambulia hadi 35mil.
Kwa maana hiyo zoezi la kuwatambua wauza korosho Limerahisishwa, mkulima anaeonekana anauza korosho za 5MIL na kuendelea inabidi waonyeshe kwanza mashamba yao ili kuepuka WALANGUAJI, kiufupi walanguaji wamedhibitiwa ingawa wengine wanafanikiwa kibishi, lakini wanaokamatwa na mzigo wa korosho bila kuonesha mashamba yanayoendana na mzigo wao yanataifishwa mara moja.
TOFAUTI NA MATARAJIO YA WALIOWENGI
Ni kwamba tofauti na matarajio;

- baada ya kulipwa pesa za korosho wengine wameongeza wake,
- Baada ya kuuza korosho wengine wametapeliwa na vimada,
- Baada ya kuuza korosho wengine hawajarudi makwao hadi hivi sasa,
- Baada ya kuuza korosho wachache wamekumbuka kufanya maendeleo,
- Baada ya kuuza korosho wengi wameparamia kununua RADIO KUBWA zile PANASONIC na sambufa wakicheza na kuruka,
- Baada ya kuuza korosho wananywesha SODA hadi mbuzi na kuwavisha miwani kama ishara ya U-doni,
- Baada ya kuuza korosho wananunua hadi madela ya kuvalisha mbuzi wao.
- Baada ya kuuza korosho mabasi kama BUTI LA ZUNGU,MANING NICE yanaendelea kushusha warembo wa kila aina kuja kuhakikisha mkulima wa korosho anarudi shambani mapema iwezekanvyo...