Baada ya CWT kushidwa kutatua matatizo ya walimu, walimu wa sayansi kuunda chama chao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya CWT kushidwa kutatua matatizo ya walimu, walimu wa sayansi kuunda chama chao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jun 29, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  baada ya cwt kuonekana dhahiri kushidwa kutetea maslahi ya walimu, kuna harakati zinaendelea hasa kwa upande wa walimu wa sayansi kuunda chama chao kitakacho tetea maslahi yao hasa ukizingatia wao wamekuwa wakifanya shughuli nyingi hasa za kuandaa practical bila malipo yeyote huku wakihatarisha maisha yao kwa kemikali kali zilizoko maabara bila kinga yeyote.
   
 2. H

  HOJA YANGU Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno.
   
 3. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Wafanye haraka. Hii CWT ina harufu ya u-CCM.
   
 4. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kila kundi la waalimu likianza kujitoa na kujiangalia lenyewe basi itakuwa ni furaha sana kwa serikali kwani itaendelea kuwanyanyasa kirahisi tu kwa kuwa tayari mko divided.Njia bora ya kudai haki za walimu ni kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuuondoa uongozi mzima wa CWT na kuweka uongozi mpya ambao unaendana na mabadiliko yanayokusudiwa kufanywa.Mkianza kutengana hivyo huku hao akina mkoba wakaendelea kuwa viongozi wenu wala hamtofanikiwa.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280

  Wacha Uongo!
   
 6. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Uongo gani?
   
 7. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,787
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  walimu wa sekondari vidiploma vinawasumbua
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,879
  Trophy Points: 280
  I trust scientist wakisema kitu wamesema!!!
   
 9. f

  frontline1 Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  jamani walimu wetu chonde chonde msiunde chama kipya, mwajikaanga kwa mafuta yenu, madaktari kwa sasa wana umoja kwa kuwa wako wamoja serikali kwa kuona huo ni mwiba kwa sasa wanaharakisha kusajili chama cha assistant medical officers na wengine kuuwa umoja wao, naomba mfikirie mara mbili nakuazimia kuwangoa viongozi wenu wa cwt muweke vijana mambo yatakwenda matakavyo na sio watakavyo watawala.
   
 10. W

  Welu JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Na sisi chama cha Umoja wa Maafisa Elimu UMET Tanzania kipo njiani kusajiliwa. CWT ni usanii tu ife kama CCM.
   
 11. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Kuwa wakijitenga watashindwa, si kweli, kwa sasa hali ilivyo ni ngumu sana kuondoa uongozi wa CWT - CCM, kwani magmba wamejizatiti huko na kuwaibia walimu.

  Huelewei nini hapo?
   
 12. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Vipi cha WAHUGUZI unakijua? cha MANESI JE? Hukijuhi?
  Kwanini walimu wote wa Chekechea hadi sekondari wawe na chama kimoja?
  Ni bora kila mtu aende kivyake ili iwe rahisi kufanya maamuzi, hivi unafikiri manesi wangekuwa pamoja na madokta hii migomo ingewezekana?
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  jamani sisi waalim wa sayansi tulishataka chama chetu siku nyingi sana na hili lipo hata kama cwt itaendelea kuwepo. hivi cwt imeweza au iliwah kutetea lini mwalim wasayansi zaid ya kusema waalim?

  nakumbuka mwaka jana ndipo cwt walipoweka swala la teaching allowance kwa waalim iwe 55% ya mshahara wake. lakin napo pia haikuweza kuishinikiza serikali huku sisi waalimu tukiumia kila siku kwa maacid huko maabara. ikumbukwe kuwa mwalim wa sayansi hana security zaid ya bima ya afya tena brown card upatapo ajali maabara hakuna anayejali zaid ya huruma ya mkuu wa shule tu tell me what is this? haya ikumbukwe kuwa mwl huyu wa sayansi anafanya kazi za watu wawili yaani as lab technician na kama mwl wa somo lakin mshahara anapokea wa mtu mmoja. tuliwah kudai tuongezewe mshahara waalimwa sayansi ili kufidia hili lakin nalo likabaki stori tu.

  cwt imekumbatiwa na waalim wa primary, na ambao ni ccm oriented siye tunawaangalia tu sasa tumechoka na litakalo kuwa na liwe manake tumechoka.

  kwataarifa yenu this time hata kama waalim wote watashindwa kugoma lkin wa sayansi lazima tutagoma tu. tunanyanyasika na inatia uchungu sana pale wenzetu wanapopata ajali maabara wanapoteza maisha kwa kemikali na hata kuwa walemavu and yet no body cares.
   
 14. k

  kasinge JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  That is what I was waiting to see. To see science teachers being respected and given special treatment. CWT has failed you guys forever. Now it's your time to wake up. Be waiting to see this happen.
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Hivi unajua nikiskia habari za cwt naona kichefuchefu, mwl leo hii akifiwa na mzazi labda asubirie huruma ya mkuu wake wa shule lakini hakuna chchote mwajiri anachotoa kama pole kwa mtumish wake. haiishii hapo kama ni mtoto uko entitled kupewa jeneza na usafiri and so forth but huwez kuamini hata hizo wanachakachua ukienda cwt kueleza majibu unayokutana nayo ni balaa.

  uje kwenye madai ya waalim sijaona field ambayo mtumish anapandishwa cheo halafu anatumikia daraja la juu kwa mshahara wa cheo cha chini kwa mwaka hadi 3 kiasi kwamba unakuta mtu anapanda vyeo mara 2 lakini hata maramoja hajapata mshahara wa hivyo vyote. leta kwenye areazi ndo usiseme utadai kila siku faili halija rudi hazina jiulize hiyo hazina inafanya nini faili miaka 3?

  huku tsd ndio usiseme ni uozo mtupu hata category ya mwl mwenye masters hakuna. yaani ukienda unauliza unataka tukueke daraja gani? e ama f sasa wewe unajiuliza hivi watumisha wa kada nyingine wanazo category kwa nini ualim hakuna? sioni haya kusema kuwa mwl wa masters anapokea mshahara wa degree holder wa kilimo is this fair? bwana acheni this time tutakufa wengi. tumechoka sana na huu unyanyasaji

  sasa hapa kweli hawa cwt wako kumtetea mwl ama kula pesa za waalim? kila salary slip ya mwl inakatwa hela kwa ajili ya cwt na ni lazima sasa hebu fikiria hizo hela kazi ni kujenga vitega uchumi tu lakin kumsaidia mwl haziwez? ama cwt ni chama cha kitega uchumi tu cha waalim na uchumi wenyewe uishie kwa mkoba na chipolopolo? serikali sijui wanawahonga nini ama ni woga wa kuuwawa manake siku zote huwa mnalalamika ukitaka kupotea basi gusa hoja yeyote inayotetea waalim.

  kwanza siongei tena manake hadi nataman kuvunja lap top kwa upuuzi wa cwt na ccm na tumeshagundua ilani na sera zote na shinikizo la kuanzisha cwt lilitoka wapi na kwanini na sasa tuko tayari kuvunja kila kitu.
   
 16. Aikasa

  Aikasa Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  jamani, mnajua kwa nn hatufanikiwi kwa hv vyama vyetu! Leo walimu wa sayansi wanaunda chama chao, kesho walimu wa sanaa nao wataunda chama chao! Cha muhimu walimu kuungana bila kuwepo makundi then kudai haki zetu! Pamoja tutashinda
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  acha wajivunie..
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nyie walimu wa sayansi mnakubali k├║tumika kama lab technician? Yaan mnakuwa madokta na manesi? Pambafu zenyu
   
 19. g

  gpluse JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 393
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 80
  Ndoto za walimu kujikomboa Tanzania ni za siku nyingi. kwa mazingira ya walimu wenyewe, elimu zao, wanavyopata hizo ajira kwa kutumia vyeti vya wajomba, shangazi n.k., hizo zitaendelea kuwa ndoto tu. Poleni walimu wenzangu. Mie nililiona mapema nikaondoka huko. Ualimu ni wito endeleeni kuchapa kazi......!
   
 20. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  kwahiyo wakianza kwa kujiita hawa wa sayansi na hawa wa arts ndo watafanikiwa?Badae waendelee hawa wa Math wengine Physics,Biology,Chemistry?Kama kuwatoa CWT ni ngumu bado kuna njia zingine za kuji"organise" kuliko hii ya kuji"disorganise".Na nani kasema kuwatoa CWT ni vigumu huku katiba ya CWT inatamka wazi kuwa kama zaidi ya nusu ya wanachama watapiga kura za kutokuwa na imani na uongozi uliopo basi uongozi huo ni batili?
   
Loading...