Baada ya Corona kuisha sheria ndogo zipitishwe kwenye Halmashauri, maeneo yote ya biashara yawekewe vitakasa mikono

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
Yakiwemo maji yanayotiririka na sabuni au sanitilizer. Aidha iwe lazima baada ya COVID-19 kuisha maeneo yote yanayokusanya idadi kubwa ya watu yawe na mapipa madogo ya kuweka taka na iwe marufuku kubwa kwa yeyote kuonekana na taka katika eneo lake la biashara.

Maeneo kama vile
- Maduka Makubwa
- Gulio
- Maduka ya jumuiya kv Malls
- Hospitali, Zahanati na Vituo vya afya
- Shule
- Makanisa
- Misikiti nk.

Iwe ni lazima maeneo hayo na mengine yote kuwekewa mapipa madogo yenye maji na kuwepo mapipa ya taka.

UKWELI ULIVYO SASA: Ni kweli kwamba maeneo mengi yenye mkusanyiko wa watu hayana vitunza uchafu/taka kv makanisani, misikitini, ndani ya maduka, kwenye vyombo vya usafiri nakadhalika.

FAIDA YA KUWEKA VYOMBO VYA KUJITAKASIA NA KUKUSANYA TAKA KWENYE MAENEO YA UMMA

1. Tutatengeneza ajira (Wanaotengeneza vipipa/vindoo vya kunawia mikono watapata ajira,wanaouza hivyo viplastiki watapata ajira, mtengenezaji atapata oda nyingi zaidi hivyo kuongeza ajira viwandani)

2. Mamlaka za maji zitaongeza mapato kwani matumizi ya maji yataongezeka. Aidha wauza maji watapata fursa ya ajira.

3. Tutapunguza pakubwa kesi za maradhi ya mkurupuko kama vile Kipindupindu, kuhara, kichocho, vidonda vya tumbo na magonjwa ya matumbo kwa ujumla wake.

4. Miji yetu na vijiji itakuwa safi na kupendezesha maeneo hayo kwa ajili ya utalii nk

5. Tutajenga utamaduni wa nidhamu miongoni mwa wanajamii wetu.

6. Tutaongeza mapato kwa wahusika wanaokaidi kupigwa faini

7. Tutapunguza uharamu na unajisi (hii ni katika mukhtadha wa kidini. Dini ya Kiislamu inasisitiza usafi pia ya Kikristo)

8. Tutapunguza kulishana uchafu. Yaani kwa kutokunawa mikono tunalishana sana uchafu hasa huku uswahilini ambako tunakula vitu mtambuka bila kunawa mikono au hata tukinawa aliekuuzia kakishika hakunawa na alikuwa uwani.
 
Kama wakiuchukua ushauri wako tutapiga hatua kubwa sana sana kufanya miji iwe misafi na tutaepuka maradhi ya milipuko

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Itasaidia sana mkuu yaani baada ya hili janga kuondoka...nashauri wazingatie hili.
 
Back
Top Bottom