Baada Ya Charles Taylor, Zamu Ya Kikwete Na Karume Inakuja - Maalim Seif | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada Ya Charles Taylor, Zamu Ya Kikwete Na Karume Inakuja - Maalim Seif

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jul 19, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sasa kuna kila dalili kwamba zoezi la uandikishaji wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) ndio litakaloiingiza nchi katika machafuko makubwa kutokana na kuzuiwa kwa watu wengi kuingizwa kwenye Daftari hilo.

  Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, alipokuwa akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kiwanja cha Herous Mkwajuni Kibeni,Mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Katika mkutano huo uliokusudiwa kuhitimisha ziara za Katibu Mkuu huyo katika wilaya ya Kaskazini ‘A’, Maalim Seif aliwaambia wananchi kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ikishirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na Idara ya Vitambulisho imeandaa mpango maalumu unaokusudiwa kuwaengua katika zoezi la uandikishaji kiasi ya Wazanzibari 80,000 kufikia mwakani ambapo zoezi hilo litakuwa limekamilika.

  “Hawa jamaa wana mpango maalum wa kuwanyima Wazanzibari haki yao ya kupiga kura. Wanajuwa kwamba bila ya kufanya hivyo, hawana uwezo wa kushinda Zanzibar. Lakini tunasema kwamba, mara hii hatukubali, hatukubali, hatukubali. Wanavyotaka tunataka. Wakitaka iwe noma, itakuwa noma kwenye nchi hii mara hii,” Alisema Maalim Seif kwa hasira huku akishangiliwa na wafuasi wake.

  Bila ya kusema ni hatua gani ambayo chama chake itachukuwa kukabiliana na tatizo hili, Maalim Seif aliwataka Rais Jakaya Kikwete na Rais Amani Karume kukumbuka kwamba siku hizi dunia ni ndogo sana na akawataka wakumbuke mfano wa mwenzao wa Sudan, Rais Omar Al-Bashir, ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu Dhidi ya Ubinaadamu.

  “Kama (Rais Karume na Rais Kikwete) wameamua kwamba nchi hii iingie kwenye vurugu, basi sawa itaingia. Lakini wajue tu kwamba ni wao ndio watakaochukuwa dhamana ya lolote litakalotokezea. Wamtizame mwenzao Bashir. Wamtazame Taylor (Charles Taylor aliyekuwa Rais wa Liberia).”

  Akifafanua mpango uliopangwa na SMZ, Maalim Seif alisema kwamba Serikali inawatumia masheha kuwanyima wananchi barua zinazowatambulisha kuwa wakaazi halali wa maeneo yao, na kwa kufanya hivyo, Idara ya Vitambulisho haitoi kitambulisho cha Uzanzibari Mkaazi kwa mtu ambaye hana barua ya sheha na mwisho ZEC haimuandikishi mtu ambaye hana kitambulisho.

  Alisema kwa kutumia mpango huo wa pande tatu, yaani Masheha, ZEC na Idara ya Vitambulisho, tayari SMZ imeshawazuia watu wapatao 3000 kuandikishwa katika majimbo ya Konde na Mgogoni peke yake katika wakati ambapo zoezi hilo linaendelea katika wilaya ya Micheweni.

  “Wanachotaka kufanya hawa jamaa ni kwamba, ikifika siku ya upiga kura kuwe hakuna sababu tena kwao kuleta majeshi na vifaru kama walivyokuwa wakifanya katia chaguzi nyingine. Wanataka waibe kabisa kura ili ukifika upigaji kura waseme kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki. Kama walivyofanya kwenye uchaguzi wa Magogoni.” Alisema Maalim Seif.

  Katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Magogoni uliofanyika mwezi Mei mwaka huu, watu walioripotiwa kukosa haki ya kuandikishwa kuwa wapiga kura ni 1,684. hata hivyo, matokeo ya uchaguzi huo ambayo yalimpa ushindi wa zaidi ya asilimia 50 mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi Asha Hilal, hayakulalamikiwa na CUF.

  Ikiwa hesabu hii ni sawa na itaendelea kuwa hivyo kwa majimbo mengine yaliyobakia, basi kuna wastani wa kukatwa wananchi 1,500 kwa kila jimbo na kwa kuwa Zanzibar ina majimbo 50 ya uchaguzi, basi watu watakaoshindwa kupiga kura mwaka 2010 watafikia 75,000, kiwango ambacho ni kikubwa sana katika uchaguzi wa Zanzibar, ambayo kwa ujumla ina wapiga kura wasiotimia 500,000.

  Akizungumzia kuingizwa kwa sharti la kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi kama kigezo cha mtu kuandikishwa kuwa mpiga kura, Maalim Seif alisema hilo limefanywa kwa makusudi ili kuhakikisha kwamba watu hawaandikishwi kwani aliyepewa mamlaka ya kuthibitisha ukaazi wa mtu ni sheha, ambaye hutumia nafasi yake kutokutoa uthibitisho huo kwa wale watu anaoamini kuwa si wafuasi wa CCM.

  “Sharti la kutumia kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi ni kinyume na Katiba ya Zanzibar. Hata Mkurugenzi wa ZEC amenukuliwa akisema hivyo na vyombo vya habari. Lakini hata kama ingelikuwa ni sawa, serikali ilipaswa kuhakikisha kuwa kila mtu aliyetimia umri anapata. Mkurugenzi wa Usajili wa Vitambulisho Zanzibar anasema idara yake imetoa vitambulisho 500,000 lakini imempa nani? Imewapa watoto mpaka wa miaka 14 lakini inawanyima wazee wa miaka 80. Imewapa watu ambao hata si Wazanzibari, kutoka Bagamoyo, Mkuranga na Kigamboni, lakini haiwapi Wazanzibari wanaokaa Micheweni. Yaani serikali ndiyo inayosimamia ubaguzi katika nchi hii. Na sisi hilo hatutalikubali hata kidogo.”

  Taarifa kutoka Pemba ambako uandikishwaji unaendelea katika wilaya ya Micheweni zinasema kwamba Masheha (Viongozi wa serikali za mitaa) wa huko wanawaambia wananchi wanaokwenda kuchukua barua za uthibitisho kutoka kwao kwamba wao hawana barua hizo na au serikali imesitisha kabisa zoezi la kutoa vitambulisho vipya mpaka hapo zoezi la uandikishaji litakapokamilika.

  Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho, Mohammed Ame, alikanusha kwamba ofisi yake imezuia zoezi la kutoa vitambulisho kama inavyodaiwa na masheha hao na kusema kwamba iwapo masheha wanatoa kauli hiyo basi huo ni mpango wenyewe na sio agizo kutokla serikalini.

  “Serikali haijasitisha kutoa vitambulisho. Kama kuna sheha anasema hivyo, anasema kwa lengo lake mwenyewe, lakini si maagizo ya serikali.” Alisema Mkurugenzi huyo.

  Mkurugenzi huyo alisema ni kweli katika zoezi la utoaji wa vitambulisho awali kulihitajika kupatikana barua za sheha wa shehia husika ili kumtambua mkaazi wa sehemu anayoishi lakini sasa wameongeza sharti la kupatikana kwa cheti cha kuzaliwa cha mhusika anayetaka kupewa kitambulisho cha mzanzibari mkaazi.

  Hata hivyo malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi mbali mbali wamnalalmikia zoezi zima la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linaonekana kuwa na vikwazo kadhaa ikiwemo masharti ya kuwa na vitambulusho vya mzanzibari mkaazi ambapo vitambulisho hivyo vinaelezwa hutolewa kwa misingi ya kiitikadi ya kisiasa.


  SOURCE:
  ZANZIBAR YETU BLOG.

  N.B Msisitizo ni wangu.
   
 2. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lini CUF wamenduka kuhusiana na hili ?
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapo lazima CUF na wananchi kwa ujumla kuwa ngangari, hawa jamaa (CCM) ukicheka nao watu kibao hawataandikishwa na pia wameshapandikiza wana Usalama kibao ambao wao huandikishwa. Na sasa wanajipanga kuchukua majimbo ya Pemba.
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo WaTanzania wote wanawaona WaPemba kuwa ni mashuja wao ,sasa ikiwa wengine mnasubiri WaPemba watafanya nini basi mtatawaliwa milele ,maana hamjiwezi miguu wala mikono ,WaPemba tu ndio mashujaa ndio wanaoweza kupambana na majeshi na mapolisi na mauslama wa Tanzania ,WaTanzania wengine wote ni viwete,mabubu,viziwi kila gumu linawezekana Pemba tu,siku hizi wakuu wote wameshughulika wanapanga mikakati ya vipi wataidhibiti Pemba , maana kwa Tanzania nzima Pemba peke yao ndio wanaume na ndio wanaoweza kupambana mpaka mpaka wanaisababishia CCM mbali ya kusaidiwa na majeshi na mapolisi basi husalim amri.

  WaTanzania wengine hawana lolote isipokuwa maneno mengi tu na kujifanya ni wapinzani wakubwa wa serikali ya CCM na vyombo vyake ,CCM na vyombo vyao vya dola wamegalagizwa chini ,Pemba ni kisiwa kidogo sana sana ,lakini wameweza kuitikisa Tanzania nzima na dunia kupata habari kuwa kuna wanaume wa kazi hapa Pemba.

  Hata serikali ya Kikwete ikisema Pemba waachiwe wajitawale wenyewe basi naona haitokuwa wamefanya kosa zaidi ya kuona wanastahili kupewa ,tofauti na sehemu zingine za Tanzania ambako watu ni woga kupita kiasi ,ila nakumbuka kitendo kimoja ambacho polisi alivuliwa nguo na kubakishwa na chupi tu sehemu za manzese na kuambia atoke mbio au na chupi itavuliwa ,hapa nilijipa moyo na kusema kuwa ikiwa watu watavinjari basi si polisi wala usalama wa Taifa atakaeweza kutokeza pua ,lakini wapi wakitimia polisi wawili tu basi huna la kuwambia WaTanganyika ,watakimbia na urafiki utakufa siku hiyo.

  Hongera WaPemba Inshaallah Mwenyezi Mungu atakuwa nanyi.
   
Loading...