Baada ya CHADEMA kula ruzuku peke yake bila kuvigawia vyama shirika uchaguzi wa 2015 Msajili abadili kanuni na kuweka masharti magumu!

Hivi Ukawa ilikuwa bado ipo?
Je, vyama vilivyoshirikiana na ukawa vilikuwa vinafaidi matokeo ya ukawa?

Ukawa haikuwa kisheria bali ni ushirikiano ambao haukuwa rasmi. Kufaidi matokeo ya ukawa ulitaka iwe kwa dalili zipi au kwenye nyanja zipi labda? Ninachojua kila chama kilipata kilichopata, kutokana na kukubalika kwake kwa wananchi kama chama.
 
Ccm imepeleka michango ya wafanyakazi wake mifuko ya hifadhi ya jamii?Kazi kudandia yasiyowahusu ya kwenu yanawashinda.
 
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 vyama vitakavyotaka kushirikiana ni lazima viingie mkataba wa kisheria na kuweka wazi maeneo ya ushirikiano wao.

Msajili msaidizi mh Nyahuza amesema uchaguzi wa mwaka 2015 uliacha vidonda baada ya chama kimoja kilichoungwa mkono kupitia UKAWA kuvisahau vyama vingine kiruzuku baada ya uchaguzi.

Msajili amesema baadhi ya vyama vililalamika kuwa chama kikuu cha upinzani kilipata wabunge wengi na kura nyingi za urais kutokana na uungwaji mkono na vyama vilivyounda UKAWA na hivyo kupokea mgao mkubwa wa ruzuku kutoka serikalini

Katika utaratibu mpya ni lazima ielezwe vyama shirika vitanufaikaje na ushirikiano huo na lazima iwekwe kisheria, amesisitiza msajili Nyahuza.

Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
Mlikipa tlp sh ngapi kwa kumuunga mkono magufuli.
 
Sisi ccm tumeungana na tlp na UDP watamuunga mkono jiwe lkn kwenye ruzuku hawalambi hata mia na msajili wa vyama hatutafanya chochote make kateuliwa na mwenyekiti wetu, hiyo sheria ni kwa ajili ya chadema na ACT make wametukalia kooni hatupumui

Mlema na baadhi ya wajumbe watapewa nafasi za uongozi katika serikari
 
Mimi najiuliza tu CDM itaishi vipi bila ruzuku baada ya uchaguzi na ile michango ya asilimia kumi itakoma maana wa kurudi bungeni sijui ni nani
 
Matajiri anapoteza muda. CDM tunapinga hesabu za kushinda uchaguzi na Siyo kupata wabunge wengi.
 
Hivi nyie hamfanyi Kazi
Au kupigia chapuo watu fulani ndy Kazi yenu

Ova
 
Hivi kuna maandishi yoyote yaliyowekwa kuhusiana na ndoa ya CCM na NCCR- MAGEUZI?
 
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 vyama vitakavyotaka kushirikiana ni lazima viingie mkataba wa kisheria na kuweka wazi maeneo ya ushirikiano wao.

Msajili msaidizi mh Nyahuza amesema uchaguzi wa mwaka 2015 uliacha vidonda baada ya chama kimoja kilichoungwa mkono kupitia UKAWA kuvisahau vyama vingine kiruzuku baada ya uchaguzi.

Msajili amesema baadhi ya vyama vililalamika kuwa chama kikuu cha upinzani kilipata wabunge wengi na kura nyingi za urais kutokana na uungwaji mkono na vyama vilivyounda UKAWA na hivyo kupokea mgao mkubwa wa ruzuku kutoka serikalini

Katika utaratibu mpya ni lazima ielezwe vyama shirika vitanufaikaje na ushirikiano huo na lazima iwekwe kisheria, amesisitiza msajili Nyahuza.

Source ITV

Maendeleo hayana vyama!
Tlp, udp, inabidi wanufaike na ushirika wao na ccm, wadhulumiwa sana na ccm kwenye ruzuku
 
Back
Top Bottom