Baada ya CCM kuzidi kukimbiwa, Nape atoa kauli hii

By Nape Moses Nnauye

UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA

Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko Arusha,Mwanza na Tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika Chama.

Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.

Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa CCM, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.

(i) Mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za CCM. Ninalo jukumu ndani ya Idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.

Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.

Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha Mapinduzi, ni ushahidi kuwa CCM inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa CCM ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.

Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la Milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la Milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona Milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi “ajivue gamba” na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa CCM na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.

(ii) Hata hivyo, Muundo wa Chama cha Mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa Tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa CCM.
Na ikasemwa wazi kuwa ‘kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote WANAOKUBALI IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM.


(iii) Nikiachana na hayo; Mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) lakini pia kamati za Mh; Cheyo, Mrema na Zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaCCM ambaye naamini katika imani ya CCM, imani yangu inayotokana na CCM ni kuwa “rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa” lakini kama mwanaCCM nimekula kiapo kuwa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ufisadi na utendaji mbovu ni tabia inayojengeka kwenye jamii yetu, namna ya kukabiliana na hali hii ni wazi kuwa jamii yote inatakiwa kubadili namna ya kujilea, ni lazima utamaduni wa kupinga ufisadi na kufatilia na kutenda haki uimarishwe katika level ya familia, lazima tujilazimishe kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kwetu, lazima tujenge msingi wa maadili katika mfumo wetu wa elimu na ajira, na lazima azimio la kuyafanya haya lianzie kwenye mioyo yetu.

Tufanye maamuzi, maamuzi haya hayatalenga mtu wala koo wala kanda bali yawe maamuzi ya watanzania wote, leo Nape anapopiga kelele na kupinga ufisadi asipingwe kwa kuwa ni Nape-katibu wa itikadi CCM lakini aungwe mkono kama mtanzania mwenye nia ya kuona watanzania wote wanaishi maisha bora, Katika hili lazima jamii iungane, nimefuraishwa na wabunge hasa wa CCM walipokuwa wakichangia taarifa za kamati za bunge, waliungana na wabunge wengine katika kulielezea hili na kupendekeza namna ya kulishughulikia.

Mimi binafsi nimesikitishwa lakini pia ni changamoto inayohitaji kushughulikiwa na kutolewa maamuzi. Katika level ya Chama tutafanya yale ambayo yapo katika wigo wetu lakini pia tutashauri serikali kupitia vyombo vyake vya haki kulifuatilia hili kwa umakini mkubwa na kulitolea maamuzi, lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.

kama bwana nape unafuatilia michango ktk hii mada uliyoweka humu jamvini, utagundua kuwa woote waliochangia wako against wewe. natumaini wengi ni vijana, ndio inajulikana vijana ndio wachangiaji wakuu humu jamvini japo wapo wazee wachache. ushauri kaa chini tafakari kwa kina jiulize kwa nini wote wamekuponda? je wanakudharau wewe kama nape au wanaidharau ccm? je baada ya miaka 3 au 13 hali itakuwaje kwako na kwa ccm? naaaaape!!!!!!!! what are you doing naaape..... huwezi kushindana na nguvu ya uma nape huwezi..........utasubiri hadi lini???
 
Ha ha ha Nape Leo umejitetea ha ha ninauhakika, Mapepe yako yataisha karibuni..
SAMAKI MMOJA AKIOZA? NAPE JIBU..
 
Nape hana akili timamu kabsaaa. Hivi enzi hizi unaleta hoja ya kisiasa tena isiyokuwa na mashiko kwa maisha ya watu! Yaani anakuja kutupotezea muda kwa porojo za hovyo tu. Nape anasema amekula kiapo kuwa atasema kweli daima fitina kwake mwiko, sasa ni kitu gani ameongea cha maana kwenye maelezo yake? Sisi trunataka ukweli wa pasupasu, mambo ya kuzunguka na misamiati hatuna haja nayo. Hivyo viapo CCM wote wamekula lkn nani anazingatia ukweli. Nape sema wazi kuwa sasa CCM ilipofikia haiwezi kuongoza nchi tena. Huo ndo utakuwa ukweli wa kutolewa na mwanaume aliyekula kiapo cha uzalendo. Mara ngapi Nape anatoa taarifa za uongo? Hata ktk uchaguzi mdogo Arumeru Mash, Nape aliongea uwongo mwingi. Kama hana la maana la kusema akae kimya. Kama ana uchungu na Taifa hili, atoke CCM sasa hivi. Labda ndo tutaona kweli anaumia kwa nchi kudorora. Nape hana nguvu yoyote ya kubadili chochote ktk CCM. Ni bora akajivua gamba mapema.
 
Nape umetoa heading nzuri kuwa UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA. Lakini umeharibu hiyo heading kwa kuendelea kutetea CCM. Watu wenye uzalendo na upendo kwa Taifa hawako CCM. Ungekuwa mkweli kabisa bila fitina, ungetamka kabisa kuwa Wana-CCM hawana uzalendo wala upendo kwa taifa, hapo tungekuelewa. Wenye uzalendo na upendo kwa taifa ni akina Millya waliohamia upinzani, ingawa wewe unawachafua. Mbona hujamsema Mgombea ubunge wenu wa Afrika Mash aliyepewa karipio pamoja na Millya? Mtu amekuwa mzigo halafu mnampa nafasi ya kugombea uwakilishi wa taifa. Nape una fitina nyingi, wewe sio mzalendo, na sio mkweli na kweli haimo ndani yako wala ndani ya chama chako.
 
Nape haelew na wala hajielew' kwake yeye kila mtu anayeona chama hakifai na kuamua kuondoka anamwona alikuwa 'MZIGO' au 'GAMBA' hataki kuheshimu mawazo yao, namhakikishia ipo siku atakubali wamekufa na siku zenyewe si nyingi.Hao watu mil6 anaosema amewasahau waliowapinga kule Igunga?ambapo walishinda lakin kwa kura tofaut na alizopata Rostam, hakumbuki wanachama wake walioikataa hiyo CCM yake mchana huku Arumeru' nao anawajumlisha kuwa wanachama wake? Namwambia ajitafakari upya na awe na akili timam.
 
Mjifunze kutafakar mnapoongea mambo ya msingi na wtu wenye AKIL TIMAM NA WANAOJITAMBUA! Mwanacham anpochukua jukmu la kujitoa mnaita mzigo na hii inathihirisha ni jinsi gani chama chenu kimekua ZIGO KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU!!!! Nape, tusomapo hatusomi uliyoyandika,tunasoma yaliyo ndani ya kile uchoandika na TZ ya sas ni ya wenye AKILI WENGI si enzi zileeeeeeeeeee!! Tazama Taifa sio chama. ulichokiongea ni kwa chama kimaslahi na msipokuwa makini mtafia kwenye kidonda.:yield:
upo sahihi
 
Kijana Nape, naomba kabla ya kujivunia idadi ya wananchama wa CCM utafakari yafuatayo;
  • Nchi ya Marekani ina idadi ya watu zaidi ya 300 milioni, Tanzania ina watu chini ya 50 milioni.
  • Nchi ya Marekani ina idadi ya wapiga kura zaidi ya 100 milioni, tanzania ina wapiga kura chini ya 20 milioni.
  • Democratic Party (DP) ya Marekani ina umri wa miaka zaidi ya 200, CCM ya Tanzania ina miaka chini ya 40.
Lakini;
  • DP ya Marekani ina wanachama (wenye kadi) wasiofika milioni moja, CCM inadai ina wanachama zaidi ya milioni 6!
  • Katika uchaguzi wa 2008, DP ilipata kura milioni 70, CCM mwaka 2010 ilipata kura milioni 5!
  • Hivi sasa wapenzi wa DP ya Marekani zaidi ya milioni 50, je wapenzi wa CCM ni wamebaki wangapi?
 
Ni kweli mkuu, kwani hata mimi ninayo, unajuwa zamani walikuwa wanatutisha eti usipokuwa na kadi ya CCM, unaweza kukosa baadhi ya uduma/ utafanikiwa haraka zaidi......CHADEMA wamekuja kutuondolea uoga huo wa zamani

Mi nilipewa tshirt nikaliweka, tukapata mfanyakazi mpya wa ng'ombe akawa hajaja na nguo. Nikaambiwa nimpe za kujisitiri kwa muda, la kwanza nikampa lile la ccm ndo nikachagua nguo mbaya nikampa.
 
Haya tena, yale yale; maneno maneno maneno maneno, bila chochote cha maana. Mtaendelea na maneno hivyo hivyo mpaka chama kitakapowafia ndo mtalijua jiji.
 
Kazana Napee, hukubali hadi ufe na tai shingoni.
Hizo takwimu za wanachama wa ccm mnazo danganya watu kwa konyesha mna wanachama wengi mnazitoa wapi?
Mnahesabu idadi ya kadi ambazo zilisha toka, bila kujua kwamba hizo zilizotoka ziko kwa akina nani.
Kwa mfano sisi tulipokuwa jeshini tulichukua kadi za ccm kutoka makao makuu tena kwa kuandikishwa majina. Wengi tumejenga mtandao tunaowasiliana mara kwa mara, ccm tunaiona kama kinyesi kwa jinsi inavyotesa wana wanchi kiasi ambacho hakivumiliki. Je, na sisi bado tupo kwenye hizo takwimu zenu?
 
kaka NAPE pole sana unaupendo na chama chako lakini huwezi kufukuza upepo.sio siri kila kitu unakiona kilivyokaa vibaya lakini kwa kuwa upo kazini lazma utetee unga wako.lakini kumbuka unajijengea mazingira ya kuchukiwa kila kukicha na kama bado una ndoto na kuwa mwana siasa unahtaji kutafuta uwezekano wa kulinda sifa yako.ww bado kijana na hata kama chama kimekulea lakin kimemomonyoka huna namna ya kukikwamua kilipofikia ni sawa na MV BUKOBA.Tabia ya kufukiafukia mambo na kudhani watanzania watasahau ina mwisho wake.ww unapolala kaka ni pazuri hujui kilichopo mtaani.Hali inatisha akina ADELA wanateseka,watu wamekata tamaa ya kuishi badilika kaka.muda haukusubiri
 
Kati ya hao wanachama m6 arumeru wako wangapi? Kwanza nitoe mimi kwenye hiyo list yako. Sikitaki tena hicho chama.
 
Mjomba umeangukia shimo la siafu bro unawezaje kujitamba na kusimama kifua mbele kwamba "chama kiko imara" hata haya huna mnakamatana ugoni wenyewe kwa uongo still na wewe hapa unaendelea kudanganya takwimu na idadi una tupa ya enzi za azimio we ni punguani kaa hapo kama jinga man subiri heshima za mwisho tukazike chama kwenye mikoa iliyobaki Arusha tulisha wazika pembeni ya Sumary.
 
Nape jiandae kuwa mpinzani 2015. CDM OYEEEEEEEE!

Hawezi hata kuwa mpinzani huyu boya nepi,hana ubongo wa kuwa mpinzai kwa Chama tawala CDM, Nape kwa sababu ya uvuvuzela wako sasa ccm inakufia, zile safari zako zakuzunguka mikoani ukisema mnavua gamba zikowapi? anza upya kuzunguka watz wanahamu upite wakupopoe na mawe.
 
Hivi hao wanachama milioni 6 huwa hawaongezeki wala kupungua? Mimi naamini wamepungua sana na wamebaki kwenye matakwimu tu, pole Nape ila ukweli wztu wameichoka ccm wanatska kutawaliwa na chama kingine, achieni nchi tu mkajipange!
 
Nape nitoe mimi kwenye orodha yako. Nilichukua kadi ya CCM ili kijiji kiniuzie shamba maana kijiji chote ni CCM. Sasa nimepata shamba na shati langu la kijani nimepatia mtendaji wa kijiji. Nimerudi kwetu Peopleeeeeeeeeeeez!
 
Nina mashaka na elimu ya Nape...

Mbona cimuelewi alichoandika??? Ni kulia, kuimba au ni nini.....

All craps
 
Back
Top Bottom