Baada ya CCM kuzidi kukimbiwa, Nape atoa kauli hii

lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.
hapa bwana nape umefuka, mmeshindwa kutekeleza uvuaji gamba na gamba linawavuka ninyi!
sijui hawa viongozi waccm wanafikilia nini??
Gamba mlilosema lazima mlitoe hamlitoi matokeo yake ndo haya mnayoyapata!
 
Naona anani hesabia na mimi nilipokwenda uingereza kusoma miaka hiyo niliambiwa lazima ninue kadi ya CCM niwe mwana chama sijawahi kamwe kuiripia lakini nimeiweka kama sourveniour

the same with me Mkuu itakuwa nipo kwenye mahesabu yake wakati mimi moyo wangu upo kinchi zaidi na si kichama!
 
Umeua font

.
Mkuu, Tume ya Katiba

Siku nyingine ukiona font ndogo fanya hivi bonyeza (kwenye keyboard yako) na shikilia kitufe (yaani Press and Hold) cha Control na huku ukiwa umehold control ... bonyeza alama ya kujumlisha yaani (+)


Press & Hold
Ctrl and press + Kukuza

Press & Hold Ctrl and press - Kupunguza


Kwa kufanya hivyo utakuza/kupunguza maandishi (font) katika saizi yoyote upendayo
 
Katika hao wanachama milioni 6, na mimi unanihesabu? Nina kadi ya 'chama' nilipewa kule Kiwalani, lakini sijawahi na sitakuja kumpigia kura mgombea yeyote wa 'chama'. Mwaka 1995, tena nikiwa na umri chini ya miaka 18, niliipigia NCCR, mwaka 2000 TLP, 2005 CHADEMA na 2010 CHADEMA, ila nyumbani nina kadi ya 'chama'! Naamini katika hao 6M wapo wengi unaowahesabu kama ulivyonihesabu mimi!


Ni kweli mkuu, kwani hata mimi ninayo, unajuwa zamani walikuwa wanatutisha eti usipokuwa na kadi ya CCM, unaweza kukosa baadhi ya uduma/ utafanikiwa haraka zaidi......CHADEMA wamekuja kutuondolea uoga huo wa zamani
 
Kwa kuwa Nape analipwa kwa kazi hii.. Mie cimlaumu kwa sana maana kama ulivyo ule msemo wa mtumikie kafiri upate mradi wako.. Sema tu napenda kumkumbusha Nape ule msemo mwingine wa Winston Churchill "The truth is incontrovertible. Malice may attack it, ignorance may deride it, money may corrupt it but in the end, there it is".. Baada ya yote CCM waliojaribu kuyafanya.. Ukweli unaanza kuonekana kwa rangi yake..
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa afukuzwe kazi, na Mwenyekiti awe mwinginne ili Raisi awajibike pia kwa chama chake katika kuteleza manifesto ya chama.Utawala wa namna hii mwenyekiti wa chama kuwa rais ni kukosa cheks and balance na wameweza china tu.
 
hii yote ni sehemu ya demokrasia lakini mimi ninachomsikitikia kijana mwenzangu nape ni kwamba CCM inakufa ikiwa chini ya uognozi wao. Kama kijana makini angechukua maamuzi magumu!!!!!

CHADEMA :help::help::help::help:CCM we are DYING!!!!!!
 
Nape kweli ni mtu wa ajabu; eti anasema ameshtushwa na taarifa ya CAG; duhh huo kweli ni usanii, taarifa za CAG for the past 10 years zinatoa uchafu kama huo leo unasema umeshtushwa.
Nape ; aliyelala hana sababu ya kuamshwa, wewe endelea kuamini CCM ina vijana wengi, kichapo kwenye chaguzi zijazo ndio kitakuamsha usingizi wako wa pono.
 
Hii inadhiirisha kuwa ccm ilishashidwa na imeshindwa kuongoza nchi!!!! Mimi ni mwana ccm kwa dhati kabisa lkn nape kubali tu! Sio vyombo vya habari au wanasiasa uchwara wanaofanya vijana wajiunge na upinzani bali ni huo uliomalizia hapo mwisho, yaani utendaji mbovu wa serikali ya ccm!!! Ccm na ife!!!!
 
Chadema hamjui? CCM ni mafia kwa taarifa yenu, kwa sasa CCM wanajipanga kuivunja CHADEMA kwa gharama zozote zile na hata damu ikimwagika. Chamsingi Mungu awekwe mbele. Hapa sina chama ( naamini katika haki na utendaji uliotukuk ) ila navutwa na peoples P.
 
Nape , unatuboa, wewe umekosa mwelekeo kabisa, kwanza haijulikani kama bado unapiga vita ufisadi /mafisadi, ni wewe uliye kwenda Arumeru Mashariki ukapanda jukwaa lilelile la kifisadi pamoja na fisadi nambari wani nchini, leo uta waambia nini wenye nchi? Vijana unao zungumzia wewe ni wale ulio nao kwenye makabrasha yenu, kialisia hawapo, ccm wamebaki vijana wenye kuishi kwa matumaini kama wewe, Mungu saidia unaweza kuukwaa uwaziri, nani ajuae?
 
Dullo Niulizie Haya maswali kwa Nape:
  1. Msingi wa karipio alilopewa Millya nilikuwa linamtaka kujitoa uanachama au kubadilika?
  2. Hilo Karipio lilikuwa na deadline ya utekelezaji?Je Millya alikuwa ndani ya huo Muda?
  3. Hiyo idadi ya wanachama kuwa ni 6mil ni ya mwaka gani?Je baada ya millya kujiotoa na wengine wengi bado database yako inasoma kuwa unawachama milion sita?
  4. Katika hiyo million sita vijana ni % ngapi?na JE wapo hai?

Kujibu Maswali ni Ungwana kwa watanzania!
 
By Nape Moses Nnauye

UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA

Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko Arusha,Mwanza na Tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika Chama.

Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.

Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa CCM, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.

(i) Mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za CCM. Ninalo jukumu ndani ya Idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.

Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.

Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha Mapinduzi, ni ushahidi kuwa CCM inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa CCM ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.

Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la Milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la Milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona Milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi “ajivue gamba” na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa CCM na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.

(ii) Hata hivyo, Muundo wa Chama cha Mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa Tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa CCM.
Na ikasemwa wazi kuwa ‘kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote WANAOKUBALI IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM.


(iii) Nikiachana na hayo; Mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) lakini pia kamati za Mh; Cheyo, Mrema na Zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaCCM ambaye naamini katika imani ya CCM, imani yangu inayotokana na CCM ni kuwa “rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa” lakini kama mwanaCCM nimekula kiapo kuwa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. NAPE ACHA USANII....Walioliua azimio la Arusha lililokuwa linadhibiti Maadili ya uongozi ni nyie sisiem.Chama chenu na serikali yake vimekuwa genge la Walanguzi na Wanyang'anyi.MMETUCHOSHA SANA,PISHENI IKULU MUWAACHIE WATU WENYE FALSAFA NA DIRA MPYA WAONGOZE NCHI.
 
kaka mbona bado unahang??naomba nijue unasupport move ya Zitto au hasupport??Philosophy ya CCM kwa sas ni ipi??sababu hata hao wanachama unaojivunua unawachanganya kila siku,,ulipotoa siku 90 watu walikupa heko na imani watu walianza kuifikiria upya,,lakini kwa haya mnayoyafanya brother na uchaguzi wenu unaokuja ndo mmeisha kabisa,,,Zitto ameamua kuwarahisishia nyie kazi na ni opportunity iliyobaki kwenu kwa sasa...:censored:
 
Br. Nape mimi binafsi nakuonea huruma kwasababu katika kutengeneza Moral person ya CCM una nafasi muhimu katika chama ambacho moral credibility yake imepwaya sana. Hili wewe unalijua na linakuumiza. Na hivi kusimama na kutetea chama cha namna hii ni maumivu sana.

Hata hivyo katika mazingira ya sasa una jambo moja la kuchagua ili kulinda credibility yako kama individual person. Au unyaze kama Kikwete na uwaache watu wakuhukumu kwa ukimya, jambo ambalo ni rahisi kujitetea, au say it black and white, you are on the wrong track.

Usianze kugeneralize tatizo kwa kuanza kuzitaja sijuwi familia, mara wananchi, sema kinaume serikali ya chama chako sasa ni kaputt. Kuanza kutaja maneno mazuri kama uzalendo au sijui Demokrasia ndani ya CCM ni kama kuvutia bangi msikitini.

Na kuitetea CCM katika suala la ufisadi ni kama kujaribu kufukuza inzi kwenye choo cha shimo. Haiwezekani, humo ndimo wanamozaliwa na wapo katika hatua mbalimbali kuanzia mayai, funza na inzi midume na mijike. Dawa ni kubomoa tu hicho choo.
 
.
Mkuu, Tume ya Katiba

Siku nyingine ukiona font ndogo fanya hivi bonyeza (kwenye keyboard yako) na shikilia kitufe (yaani Press and Hold) cha Control na huku ukiwa umehold control ... bonyeza alama ya kujumlisha yaani (+)


Press & Hold
Ctrl and press + Kukuza

Press & Hold Ctrl and press - Kupunguza


Kwa kufanya hivyo utakuza/kupunguza maandishi (font) katika saizi yoyote upendayo


Asante sana kwa somo hili!
 
Back
Top Bottom