Baada ya CCM kuzidi kukimbiwa, Nape atoa kauli hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya CCM kuzidi kukimbiwa, Nape atoa kauli hii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dullo, Apr 20, 2012.

 1. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  By Nape Moses Nnauye

  UZALENDO NI UPENDO KWA TAIFA

  Kwa muda sasa nimekuwa nikipokea meseji mbalimbali kutoka kwa vijana mbalimbali wakitaka kujua hali halisi juu ya yanayoendelea sasa huko Arusha,Mwanza na Tandahimba lakini pia wanaonesha kushtushwa kwao pale wanaposoma magazeti na kusikiliza baadhi ya radio. Wanahoji kuhusu hali ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi lakini pia hili wanatoa maoni juu msimamo wa vijana na nafasi yao katika Chama.

  Labda kwa upande wangu niseme haya yafuatayo;
  Kwanza si kweli kuwa vijana wote wamepoteza mvuto na chama cha Mapinduzi na kujiunga upinzani, bali hii ni propaganda ya upinzani kupitia vyombo vya habari vilivyo tayari kutumika katika kujipatia umaarufu na kuudanganya umma wa watanzania.

  Mimi ninao ushahidi wa kimazingira kwani nimefanya ziara nchi nzima na sehemu zote nilipokelewa na makundi ya vijana ambao ni wanachama wa CCM, lakini hata ushahidi wa takwimu unaonyesha hilo kwani katika wanachama takriban milioni sita (6,000,000) tulionao idadi ya vijana ni kubwa ukilinganisha na makundi-rika mengine.

  (i) Mimi nikiwa kama msimamizi mkuu wa shughuli za uenezi wa itikadi, siasa na sera za CCM. Ninalo jukumu ndani ya Idara yangu, kutafakari kwa kina juu ya hali ya sasa ya siasa ndani na nje ya chama lakini pia ni katika majukumu yangu kuwaeleza na kuwajibu maswali mnayoniuliza juu ya upepo wa sasa wa siasa ndani ya chama.

  Ni wazi kuwa upo mgongano wa mawazo na utofauti wa mitazamo juu ya namna ya uendeshaji wa shughuli za chama lakini pia juu ya maamuzi na mahusiano ya chama na wanachama wake na wananchi kwa ujumla hususani kundi la vijana ambalo ni kundi kubwa.

  Napenda niwatoe wasiwasi kuwa mgangano huu wa mawazo ni Afya kwa chama na ni kitu kinachodhihirisha uhai wa chama cha Mapinduzi, ni ushahidi kuwa CCM inatoa nafasi kwa wanachama wake kuhoji, kushauri, kupendekeza na kukosoa. Lakini pia ni kuonesha bayana kuwa wanachama wa CCM ni makini na wenye mawazo huru muda wote. Ila inapotokea kuwa njia za kukosoa ama kushauri ni potofu huwa tunasahihisha juu ya njia iliyotumika lakini tunachukua ushauri na mapendekezo hayo.

  Baadhi ya walioniandikia wanahoji ikiwa hili la Milya na madiwani linahusiana na hali hii ya migongano ya mawazo nami nawajibu kuwa ,hili la Milya linahusiana zaidi na maamuzi ya vikao vya chama vya kamati ya maadili, ambayo ilimuona Milya kuwa ni miongoni mwa wanachama wanaohitajika kupewa karipio na kuonywa juu ya mwenendo wake lakini pia kujitafakari na ikibidi "ajivue gamba" na naamini kuwa alifanya hivyo na kukiri kwa utashi wake kuwa namna ya matendo yake na hulka zake haziendani na mwanachama muadilifu wa CCM na hivyo kwa kuwa hawezi kubadilika aliamua kujivua gamba, uamuzi ambao si tu kuwa tumeuheshimu lakini pia tumeukubali. Pia kuhusu madiwani ambao nao wanaungana na milya ni watu ambao wameshindwa kuwaza sawasawa na wanaofuata mkumbo, wameshindwa kutumia fursa kama viongozi ndani ya chama, wameshindwa kujielewa hivyo wameshindwa kuelewesha wengine.

  (ii) Hata hivyo, Muundo wa Chama cha Mapinduzi kikatiba unawapa vijana fursa na nafasi ya kujipanga na kufanya kazi za chama kwa kiwango cha uelewa wao na uwezo wao. Chama kimeweka jumuiya ya vijana, ambako huko vijana wanakuwa recruited, nurtured na utilized kwa manufaa ya chama. Jumuiya hii inayo wajibu wa kuhakikisha kuwa kundi la vijana wa Tanzania linakuwa ni kundi la vijana wa CCM.
  Na ikasemwa wazi kuwa ‘kutakuwa na jumuiya ya vijana ambamo kutakuwepo vijana wote WANAOKUBALI IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI YA CCM.


  (iii) Nikiachana na hayo; Mimi binafsi nimeshtushwa na taarifa zilizotolewa bungeni na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) lakini pia kamati za Mh; Cheyo, Mrema na Zito,.ambazo zinaonesha kuwepo kwa ufisadi na matumizi ya hovyo katika mamlaka,taasisi na halmashauri mbalimbali ndani ya serikali. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na kutafakari juu ya hali hii. Nikiwa kama mwanaCCM ambaye naamini katika imani ya CCM, imani yangu inayotokana na CCM ni kuwa "rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa" lakini kama mwanaCCM nimekula kiapo kuwa "Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko. Taarifa hizi za mkaguzi wa serikali zinaonyesha kuwepo kwa rushwa, ufisadi na utendaji mbovu wa waajiriwa wa serikali, lakini pia zinaonyesha kwa kiasi gani tatizo la ufisadi lilivyokithiri katika jamii ya watanzania na hasa wataalam ambao kwa sehemu kubwa ndiyo watumishi wa umma. Kwani pamoja na kuwepo vyombo mbalimbali vya kushughulikia rushwa na ufisadi bado ufisadi wa kiasi hiki unaendelea, naamini kuwa kupambana na rushwa ni suala la zaidi ya uwepo wa taasisi. Ufisadi na utendaji mbovu ni tabia inayojengeka kwenye jamii yetu, namna ya kukabiliana na hali hii ni wazi kuwa jamii yote inatakiwa kubadili namna ya kujilea, ni lazima utamaduni wa kupinga ufisadi na kufatilia na kutenda haki uimarishwe katika level ya familia, lazima tujilazimishe kusema ukweli hata kama ukweli huo ni mchungu kwetu, lazima tujenge msingi wa maadili katika mfumo wetu wa elimu na ajira, na lazima azimio la kuyafanya haya lianzie kwenye mioyo yetu.

  Tufanye maamuzi, maamuzi haya hayatalenga mtu wala koo wala kanda bali yawe maamuzi ya watanzania wote, leo Nape anapopiga kelele na kupinga ufisadi asipingwe kwa kuwa ni Nape-katibu wa itikadi CCM lakini aungwe mkono kama mtanzania mwenye nia ya kuona watanzania wote wanaishi maisha bora, Katika hili lazima jamii iungane, nimefuraishwa na wabunge hasa wa CCM walipokuwa wakichangia taarifa za kamati za bunge, waliungana na wabunge wengine katika kulielezea hili na kupendekeza namna ya kulishughulikia.

  Mimi binafsi nimesikitishwa lakini pia ni changamoto inayohitaji kushughulikiwa na kutolewa maamuzi. Katika level ya Chama tutafanya yale ambayo yapo katika wigo wetu lakini pia tutashauri serikali kupitia vyombo vyake vya haki kulifuatilia hili kwa umakini mkubwa na kulitolea maamuzi, lakini pia tutawaomba wananchi watuunge mkono na kutuamini katika utekelezaji wa maamuzi na ushauri wetu.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Umeua font
   
 3. l

  london JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 12, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ajabu ajabu wewe Nape si ndiye unatamba siku zote nyie ndo serikali sasa hapa unaongea upuuzi gani SEMA mmeshindwa wewe chama chako cha magamba na serikali yako. Viongozi karibia wote wa serikali wako kwenye kamati kuu na NEC sasa mnashindwa wapi kuwapasha ukweli au kuwashinikiza watekeleze majukumu yao iwapasavyo.

  CCM hamna nia thabiti kwa taifa na wananchi wake, hapa nakunukuru km ndo kauli yako kweli
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Taarifa yake naifananisha na VUVUZELa linalopigwa na mtu dhaifu, asiyeweza kupuliza sawasawa!!

  Siye yetu macho tu:A S shade:
   
 5. I

  Idofi JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,541
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  Vuvuzela huyo hajui anachokiongea
   
 6. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,638
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Katika hao wanachama milioni 6, na mimi unanihesabu? Nina kadi ya 'chama' nilipewa kule Kiwalani, lakini sijawahi na sitakuja kumpigia kura mgombea yeyote wa 'chama'. Mwaka 1995, tena nikiwa na umri chini ya miaka 18, niliipigia NCCR, mwaka 2000 TLP, 2005 CHADEMA na 2010 CHADEMA, ila nyumbani nina kadi ya 'chama'! Naamini katika hao 6M wapo wengi unaowahesabu kama ulivyonihesabu mimi!
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kama ndivyo, Nape unakubali kuwa utawala wa CCM umeshindwa kusimamia mambo? Huoni ipo haja ya kupisha ili wengine waongoze jahazi?
   
 8. Mauntana

  Mauntana Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hao milioni 6 naomba usinihesabu maana nlipewa kadi kwakulazimishwa. Sisiemu ni wapuuzi sana eti wakatugaia viongozi wa chuo kadi zao jamani sijawahi hata kuifungua naona kama inahitaji sahihi pia mliniwekea. Chadema oyeeeeeeeeeeee
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nape ni gamba!
   
 10. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Mkuu tune kazi yako isomeke vizuri, yaani ni mtihani mkubwa kuisoma kama ilivyo sasa
   
 11. T

  Twaa Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka hapo kwenye ufisadi umepotea njia! Kwanini ulinyimwa kugombea ubunge? Je ilikua sahihi wewe kunjimwa ndio ukapewa ukuu wa wilaya? Ufisadi ndani ya CCM sio jambo la kushangaza! Je kuna mwanaCCM yeyote ambae alishawahi kuwajibishwa kwa ufisadi? Mwenyekiti wa CCM mwenyewe ni fisadi katika sakata la RICHMOND NA DOWANS, je una uhakika na misemo uliyoitoa ni applicable ndani ya CCM? MIAKA 50 ndani ya uongozi halafu unataka kutudanganya kirahisi!?

  Kuwa mkweli, je unakumbuka twiga waliotoroshwa kwenda ulaya na maofisa wa serikali sasa unataka jamii izuieje wakati CCM walitumia wingi wao bungeni kuipotezea ile ya wanyama kuuzwa? Je walichukuliwa hatua ile hali wapo ndani ya CCM mpaka sasa? Kwanini unakua mwongo kiasi hicho? Au unataka kutuaminisha kwamba sisi raia ndio tunalea ufisadi?

  Ufisadi ulianzishwa na wanaCCM na kutunzwa na wanaCCM! je unataka utuambie wanaCCM wakiona ufisadi ndani ya vyama vya upinzani watakaa kimya!? CCM haina tofauti na chama cha matajiri, je ulishawahi kuona mkulima akithaminiwa ndani ya CCM? Bwana nape acha kutapatapa kwani CCM mmeshaifilisi nchi!
   
 12. A

  Apeche Alolo Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vuvuzela hlooo huna sera babu jipange kwanza co unabwa2ka jipange tena sanaaa
   
 13. Z

  Zyamchani Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Takwimu ya idadi ya wanachama anayotumia Nape ina mapungufu makubwa kwani ktk idadi hiyo anayotaja kuna wanachama waliingizwa na wagombea wa kura za maoni ili kupata waungaji mkono wao (wagombea kulipia kadi watu) ambao kimsingi ni wanachama maslahi tu. Vile vile wanachama wengine si hai tena na kwa sasa si mashabiki wa CCM.

  Hoja za wabunge wa CCM azipime vizuri, kama hao ni wabunge wanaofaidi wanasema hivyo je wanachama wengine wapo au wana mtazamo gani?
   
 14. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM update idadi yenu ya wanachama, hasa kwa kuangalia waliolipia ada mwaka 2011 tu mtapata idadi kamili msijidanganye na hiyo idadi ya wanachama na kama wana 6m why rais kikwete alipata kura zile?
   
 15. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 742
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Huna jpya. Jivue unyoka mkuu nape
   
 16. M

  Musyokaa Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjifunze kutafakar mnapoongea mambo ya msingi na wtu wenye AKIL TIMAM NA WANAOJITAMBUA! Mwanacham anpochukua jukmu la kujitoa mnaita mzigo na hii inathihirisha ni jinsi gani chama chenu kimekua ZIGO KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU!!!! Nape, tusomapo hatusomi uliyoyandika,tunasoma yaliyo ndani ya kile uchoandika na TZ ya sas ni ya wenye AKILI WENGI si enzi zileeeeeeeeeee!! Tazama Taifa sio chama. ulichokiongea ni kwa chama kimaslahi na msipokuwa makini mtafia kwenye kidonda.:yield:
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Naona anani hesabia na mimi nilipokwenda uingereza kusoma miaka hiyo niliambiwa lazima ninue kadi ya CCM niwe mwana chama sijawahi kamwe kuiripia lakini nimeiweka kama sourveniour
   
 18. S

  SJUMAA26 JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 611
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi kwanini huyu asipigwe BAN hadi pale atakapohamia CDM? Mods, kwanini unaruhusu watu kama hawa ku-post uongo na maneno ya kipumbavu kama haya ilhali wanaosoma ni great thinkers? Nashauri muanzishe Fisadi Forum, iwe the home of great sinkers kama Nape. Mpuuzi kweli huyu!

   
 19. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hii yote ni sehemu ya demokrasia lakini mimi ninachomsikitikia kijana mwenzangu nape ni kwamba CCM inakufa ikiwa chini ya uognozi wao. Kama kijana makini angechukua maamuzi magumu!!!!!
   
 20. W

  Wangama guy Senior Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nape jiandae kuwa mpinzani 2015. CDM OYEEEEEEEE!
   
Loading...