Salamu za pongezi zaendelea kumiminika
Tarehe: 8th November 2010 @ 21:15 HabariLeo
SALAMU za pongezi kutoka ndani na nje ya Tanzania, zimeendelea kutolewa kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, awamu ya saba.
Salamu hizo zinatoka kwa jumuiya, vyama vya siasa, vikosi vya ulinzi na usalama, mashirika, wizara, taasisi za serikali na zisizo za serikali, ofisi za ubalozi wa Tanzania zilizopo nje na ndani ya nchi pamoja na wananchi mbalimbali.
Miongoni mwa salamu hizo ni kutoka Ofisi ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Devis Mwamunyange ambaye ametoa salamu kwa niaba ya maofisa, askari, watumishi wa umma wanaofanya kazi jeshini na kwa niaba yake binafsi.
Salamu hizo zilieleza kuwa ushindi wa Dk. Shein umeonesha dhahiri imani kubwa waliyonayo wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla juu ya uadilifu alionao, uzalendo, uvumilivu, unyenyekevu na kwamba yeye ndiye atakayewaletea maendeleo ya kweli chini ya mfumo mpya wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Nayo Jumuiya ya Al-Youseif, imetoa salamu za pongezi na kueleza kuwa Wazanzibar wamefanya uchaguzi mzuri wa kumchagua Dk. Shein kutokana na uongozi wake bora. Jumuiya hiyo, imemhakikishia Dk. Shein kuendelea kutoa ushirikiano wake na misaada yake kwa Zanzibar.
Naye Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba kwa niaba yake na watendaji wa Idara yake ameeleza kwamba kuchaguliwa kwa Dk. Shein sio kwa bahati, bali ni kutokana na juhudi zake katika kuchapa kazi.