Baada ya Bunge kufunguliwa Minyororo na Rais Samia ,Sasa naweza kutazama mjadala wa Bunge.

kavyilu

Member
Dec 14, 2019
28
53
Moja kwa moja kwenye mada.
Kwanza nipongeze kwa dhati kabisa hotuba yenye dira kwa taifa iliyotolewa na Rais wetu.

Katika hotuba yake Rais Samia alisisitiza wabunge kujadili maswala badala ya kujadili mambo madogo na ya hovyo kama alivyo wahi kusema Prof Mussa Assad.

Mh.Rais Samia alisisitiza kujikita kutetea wananchi wao badala ya kutetea serikali(kwa lugha za ntaani walikatazwa upambe)

Leo wabunge wanatema nyongo utadhani enzi za Bunge la Lissu,Zitto na Mnyika.

Video clip za wabunge zinatembea kama umeme kwenye socia media.

Hii inaonesha walau wameamshwa usingizini na Rais Samia.

Japo Rais alisema yeye na Mwendazake ni kitu kimoja.

Mimi nawaona ni watu wawili tofauti sana japo wanatokana na chama cha Mapinduzi.

Rais Samia kalifungua rasmi minyororo Bunge ,wabunge wameanza kazi ya ubunge leo huko nyuma walilipwa fedha ambazo zilikuwa haziendani na kazi waliyokuwa wakifanya.

"WALIOKULA UNGA WA NDELE SASA WAMELISHWA UNGA WA RUTUBA NA RAIS SAMIA."
 
Back
Top Bottom