DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,212
- 4,517
Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.
Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.
Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.
Je, tunafanyeje kisheria hapa??
Ni halali hiyo?
Mzee aliyekuwa msimamizi wa mali ya familia kwa faida ya wote ameshatangulia. Kuepuka uhuni na uhasama usokuwa wa lazima, gawaneni mali kwa mama zenu.
Wake za wazee wapewe chao kila mmoja ajipange.
Watoto wa mama mdogo wana haki kabisa kudai sehemu ya mali maana hamtachelewa kuwageuka huko mbleleni.