Baada ya baba kufariki, watoto wa mke mdogo wanataka mali, tufanyeje?

Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.

Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.

Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.

Je, tunafanyeje kisheria hapa??

Ni halali hiyo?

Mzee aliyekuwa msimamizi wa mali ya familia kwa faida ya wote ameshatangulia. Kuepuka uhuni na uhasama usokuwa wa lazima, gawaneni mali kwa mama zenu.

Wake za wazee wapewe chao kila mmoja ajipange.

Watoto wa mama mdogo wana haki kabisa kudai sehemu ya mali maana hamtachelewa kuwageuka huko mbleleni.
 
"Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake"

Labda ame edit lakini kusudio lake ndio hilo maana haiingii akilini kama watoto wazaliwe na baba mmoja halafu wawashangae wenzao kudai mirathi.
Anachoshangaa mleta uzi ni wao kudai mirathi ya mama yao ambaye ni marehemu. Yaani kwa maana nyingine ni kuwa wanadai haki ya marehemu mama yao kurithi mali kutoka kwa marehemu mume wake.

Ingekuwa wanadai mirathi yao wao kama watoto naamini mleta uzi asingeshangaa maana ni haki yao iyo hai.

Ishu hapo ni marehemu anadai vipi mirathi ya marehemu mwingine?, ambapo sheria ipo wazi kuwa marehemu hufa na urithi wakw kwenye mirathi yoyote aliyokuwa na haki nayo.

Mleta uzi ana swali zuri sana.
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,

Watoto kama ni wa huyo Baba yao kwanini wadai Mali ya marehemu Mama yao kwa Marehemu Mumewe na isiwe wao wadai Mali ya Marehemu Baba yao?

Yaani wao wanataka Mali mara mbili? Ya Baba kwa Watoto na Mama kwa mumewe?
Exactly, hapa ni kama vile wanataka mara mbili.

Nakubaliana na wazo lako, mwenye uzi kuna mambo anatakiwa kuyaeleza zaidi ili asaidike vizuri
 
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,

Watoto kama ni wa huyo Baba yao kwanini wadai Mali ya marehemu Mama yao kwa Marehemu Mumewe na isiwe wao wadai Mali ya Marehemu Baba yao?

Yaani wao wanataka Mali mara mbili? Ya Baba kwa Watoto na Mama kwa mumewe?
Kumbuka kama baba ni muislamu anapokufa mali hurithiwa na watoto, mke/wake, wazazi. Hivyo, iwapo hao watoto wamezaliwa na baba mmoja, watoto hao watapata urithi wao na mama yao atapata urithi wake. Na wao watoto wana haki ya kurithi mali za mama yao iwapo amekufa. Kwa msingi huo, iwapo mali haikugawanywa baba yao alipofariki definitely watoto watapata mali kwa awamu mbili (au urithi mara mbili kutoka kwa warithiwa wawili tofauti). Watapata mali ya urithi wa baba yao halafu watachukua mali ya urithi wa mama yao aliyopaswa kupata kutoka kwa mumuwe.

Kama watoto si wa baba huyo, wao wana haki ya kupata mali za urithi kutoka kwa mama yao pekee na only ikiwa mume wa mama yao alianza kufa kabla ya mama yao. Kama mama yao alianza kufa na wao si watoto wa baba huyo then hawana urithi zaidi ya kuomba kufanyiwa ihsani tu.
 
Inategemea marehemu alikua anaishi katika misingi gani ya kiiamani na taratibu,mfano ni ya kiristo,uislamu au mila nk mfano waislamu watoto nje hawarithi ila pia Uislamu ina uhalalisha ndoa za mitaala , hawarithi kabisa ila kama marehemu alikua ni mkristo ina maana watoto wa njee wanarithi yani watoto wote wana haki kasoro mke wa njee ambapo dini ya kikristo hairuhusu maana ni ndoa ya mke mmoja na mume mmoja,
 
Anachoshangaa mleta uzi ni wao kudai mirathi ya mama yao ambaye ni marehemu. Yaani kwa maana nyingine ni kuwa wanadai haki ya marehemu mama yao kurithi mali kutoka kwa marehemu mume wake.

Ingekuwa wanadai mirathi yao wao kama watoto naamini mleta uzi asingeshangaa maana ni haki yao iyo hai.

Ishu hapo ni marehemu anadai vipi mirathi ya marehemu mwingine?, ambapo sheria ipo wazi kuwa marehemu hufa na urithi wakw kwenye mirathi yoyote aliyokuwa na haki nayo.

Mleta uzi ana swali zuri sana.
Wakuu naomba kuuliza, hivi ikatokea mzee(muislam) alikuwa na wake watatu kati ya hao wamekufa wawili na kubaki mke mdogo wa mwisho alafu, je mirathi inagawa kufuata idadi ya wake alioa(nyumba) au kulingana na idadi ya wanufaika.
 
Wanufaika Mkuu, hapo kwa haraka haraka ikifika muda huyo mzee akafariki basi mirathi itaenda kwa watoto zake pamoja na huyo mke aliye hai.

Kanuni ni kuwa marehemu hana urithi au tuseme marehemu hapewi urithi, hivyo hao wake waliofariki hawatakuwa na urithi wowote.
 
Watagawana kwa idadi yao hao watoto au kwa mafungu matatu kulingana alivyooa mama yao?
 
Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.

Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.

Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.

Je, tunafanyeje kisheria hapa??

Ni halali hiyo?
Ikiwa ni muislamu basi anayerithi ni huyo mama aliyebaki hai tu. kwa upande wa mke. Hata watoto waliokwisha kufa kabla ya kufa mzazi hawawezi kuingizwa kwenye mirathi.

Ama watoto wote watarithi (kama wamezaliwa ndani ya ndoa) kama ilivyoainishwa kwenye dini.
 
Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.

Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.

Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.

Je, tunafanyeje kisheria hapa??

Ni halali hiyo?
nashindwa kukusaidia kwasababu andishi lako halijitoshelezi
je hao watoto mama alikuwa nao kabla hajaolewa au aliwazaa na mzee wako?
je walifunga ndoa?
je walichuma mali pamoja?
 
Kwanza poleni na msiba

Twende kwenye mada, nitakupa ushauri/mwanga wa juu kuhusu wa sheria za mirathi japo hujasema nyie ni dini gani ila ipo hivi;

1. Kanuni ya kwanza kuifahamu ni kuwa, hauwezi kudai mirathi ambayo angerithi marehemu. Ufafanuzi ni kuwa mtu hawezi akadai apatiwe mali ambayo ingerithiwa na mtu mwingine kama uyo mtu angekywa hai.

Mfano, mtoto hawezi kudai urithi wa mzazi wake ambaye ni marehemu. Kama nimekuelewa vizuri hawa ndugu zenu wanadai malu ambayo kama mama yao angekuwa hai basi angerithi kutoka kwa baba yenu mara baada ya baba yenu kufariki.

Kama ni hivyo, basi hilo haliwezekani kisheria. Marehemu anakufa na haki/urithi wake.

2. Kanuni ya pili ni kila mtoto ana haki ya kurithi kutoka kwa baba yake. Sheria ya mirathi kwa sasa haibagui mtoto yeyote wa marehemu. Awe kazaliwa ndani ya ndoa au alizaluwa kutokana na baba yake kuchepuka.

Kisheria hakuna mtoto haramu, wote ni watoto wenye haki sawa.

Sasa hawa ndugu zenu wanaweza kutumia msimamo huu wa kisheria kudai urithi wao kutoka kwa baba yao ambaye ni baba yenu pia. Hii haihitaji ushauri zaidi ya kukwambia kuwa ni haki yao kisheria na wanaweza kuitekeleza.

Hapa kuna jambo muhimu sana la kufanya ilimali za marehemu zisipotee holela.
Ili kuepusha migogoro hapo baadae nawashauri mfungue mirathi katika mahakama ya mwanzo iliyopo eneo lenu. Ni rahisi sana na gharama nafuu, mtatakiwa mfanye yafuatayo kabla hamjaenda mahakamani kufungua mirathi

1. Mnatakiwa mtafute wosia aluoacha marehemu baba yenu. Kama hajaacha wosiana kabisa fuateni hatua ya pilihapo chini

2. Mnatakiwa kufanya kikao cha familia kumchagua msimamizi wa mirathi, huyu ndio atagawa mali za marehemu kama ataidhinishwa na mahakama

3. Baada ya kufanya kikao cha kumteua msimamizi wa mirathi, andaeni muhktasari muupeleke mahakama ya mwanzo ambapo mtafungua shauri la mirathi (huu sio ugomvi, ni taratibu tu).

4. Baada ya kufungua mirathi litatoka tangazo la kuomba kuwa msimamizi wa mirathi na kama hakutakuwa na pingamuzi lolote basi mahakama itamuidhinisha huyo mliyemchagua kuwa msimamizi wa mirathi, na atatakiwa kujaza fomu ya wadhamini mahakamani.

Baada ya hapo ataanza kazi ya kukusanya na kugawa mali za marehemu kwa warithi wote, hapa ni muhimu mtambue kuwa kwa sasa warithi wanaoonekana wazi ni watoto na mke aliye hai (kama ana cheti cha ndoa) yule mke aliyekwisha fariki sio mrithi.

Baada ya kukamilisha kugawa mali kwa warithi, msimamizi wa mirathi atapeleka hesabu mahakamani kwa ajili ya kufunga mirathi. Na mahakama itafanta hivyo.

NB: Kama hakuna migogoro ni zoezi la muda mfupi sana miezi mi 3, ila kama kuna migogoro linaweza likawa zoezi la hadi miaka 20, ni nyie tu mchague liwe zoezi fupi au refu

Kila la kheri, natumaini umepata mwanga. Ukiwa na swali uliza Mkuu.
Kuna kesi mke mkubwa anataka kugawa mali kwa watoto wa mke mdogo wakati mke mdogo bado yupo hai je kisheria mke mkubwa yupo sahihi?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Inategemea anataka kugawa mali ya nani na anagawa yeye kama nani. Ipo hivi;

Kama ameidhinishwa na Mahakama kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu mume wao na anagawa mali ya marehemu mume wao kwa watoto ikiwa ni pamoja na kwa watoto wa mke mdogo, yupo sahihi kabisa.

Ila kama hajaidhinishwa na Mahakama kuwa msimamizi wa mirathi na akagawa au anagawa mali za marehemu hata kama akiwapa warithi halali, kisheria hayupo sashihi.

Changamoto hapo itakuwa ni kuzitambua mali za marehemu bila kuzichanganya na mali za mke/wake zake. Sababu anaweza akachukua mali za mke mdogo akazigawa kama mali za marehemu mume wao, hapo hatakuwa sahihi na pataibuka mgogoro.

Sharti la kwanza ni msimamizi wa mirathi aweze kuzitambua na kuzikusanya mali za marehemu.

Kama bado una utata unaweza kumuona wakili aliye karibu na mahali ulipo akupe ushauri zaidi Mkuu. Naamini utakuwa umepata mwanga pia kwa ufafanuzi niliokupatia Mkuu.
 
Asante

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,

Watoto kama ni wa huyo Baba yao kwanini wadai Mali ya marehemu Mama yao kwa Marehemu Mumewe na isiwe wao wadai Mali ya Marehemu Baba yao?

Yaani wao wanataka Mali mara mbili? Ya Baba kwa Watoto na Mama kwa mumewe?
Wanachotaka Watoto wa Mke mdogo ambae pia ni Marehemu kwa Sasa,ni kugawana Mirathi ya Baba yao kwa nji ya matumbo, yaani hapo ipigwe nusu kwa nusu, Mke Mkubwa nusu yake atagawana na wanawe na Mke mdogo nusu yake atagawana na wanawe! Sasa hapo Mara nyingi wanaopunjika ni Watoto waliozaliwa wengi kutoka tumbo moja! Mfano Kama Mke Mkubwa ana Watoto watano na mke mdogo ana Watoto wawili,basi watakao pata kingi ni lile tumbo la Watoto wawili!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.

Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.

Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.

Je, tunafanyeje kisheria hapa??

Ni halali hiyo?
Hizo ndoa zilikuwa za namna gani? ie kidini,kimila au kiserekali?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom