Baada ya baba kufariki, watoto wa mke mdogo wanataka mali, tufanyeje?

DALA

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
2,083
4,057
Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake.

Sasa huyo mke mdogo alishafariki muda mrefu amebaki huyu mkubwa ambaye ni mama yetu sisi. Muda si mrefu mzee naye kafariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu.

Tumefanya msiba na mazishi tayari. Sasa hawa watoto wa mke mdogo wa mzee wanataka sehemu ya urithi kwa upande wa mama yao wakati mke wa marehemu(mke mkubwa ambaye ni mama yetu sisi) bado yupo.

Je, tunafanyeje kisheria hapa??

Ni halali hiyo?

Mzee aliyekuwa msimamizi wa mali ya familia kwa faida ya wote ameshatangulia. Kuepuka uhuni na uhasama usokuwa wa lazima, gawaneni mali kwa mama zenu.

Wake za wazee wapewe chao kila mmoja ajipange.

Watoto wa mama mdogo wana haki kabisa kudai sehemu ya mali maana hamtachelewa kuwageuka huko mbleleni.
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
5,443
7,013
"Ipo hivi mzee wetu alikuwa na wake wawili mkubwa ndio mama yetu sisi na mdogo alikuwa ana watoto wake"

Labda ame edit lakini kusudio lake ndio hilo maana haiingii akilini kama watoto wazaliwe na baba mmoja halafu wawashangae wenzao kudai mirathi.
Anachoshangaa mleta uzi ni wao kudai mirathi ya mama yao ambaye ni marehemu. Yaani kwa maana nyingine ni kuwa wanadai haki ya marehemu mama yao kurithi mali kutoka kwa marehemu mume wake.

Ingekuwa wanadai mirathi yao wao kama watoto naamini mleta uzi asingeshangaa maana ni haki yao iyo hai.

Ishu hapo ni marehemu anadai vipi mirathi ya marehemu mwingine?, ambapo sheria ipo wazi kuwa marehemu hufa na urithi wakw kwenye mirathi yoyote aliyokuwa na haki nayo.

Mleta uzi ana swali zuri sana.
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,

Watoto kama ni wa huyo Baba yao kwanini wadai Mali ya marehemu Mama yao kwa Marehemu Mumewe na isiwe wao wadai Mali ya Marehemu Baba yao?

Yaani wao wanataka Mali mara mbili? Ya Baba kwa Watoto na Mama kwa mumewe?
Exactly, hapa ni kama vile wanataka mara mbili.

Nakubaliana na wazo lako, mwenye uzi kuna mambo anatakiwa kuyaeleza zaidi ili asaidike vizuri
 

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
3,932
5,090
Nadhani mwenyewe angekuja aliweke hili jambo vizuri maana linachanganya,

Watoto kama ni wa huyo Baba yao kwanini wadai Mali ya marehemu Mama yao kwa Marehemu Mumewe na isiwe wao wadai Mali ya Marehemu Baba yao?

Yaani wao wanataka Mali mara mbili? Ya Baba kwa Watoto na Mama kwa mumewe?
Kumbuka kama baba ni muislamu anapokufa mali hurithiwa na watoto, mke/wake, wazazi. Hivyo, iwapo hao watoto wamezaliwa na baba mmoja, watoto hao watapata urithi wao na mama yao atapata urithi wake. Na wao watoto wana haki ya kurithi mali za mama yao iwapo amekufa. Kwa msingi huo, iwapo mali haikugawanywa baba yao alipofariki definitely watoto watapata mali kwa awamu mbili (au urithi mara mbili kutoka kwa warithiwa wawili tofauti). Watapata mali ya urithi wa baba yao halafu watachukua mali ya urithi wa mama yao aliyopaswa kupata kutoka kwa mumuwe.

Kama watoto si wa baba huyo, wao wana haki ya kupata mali za urithi kutoka kwa mama yao pekee na only ikiwa mume wa mama yao alianza kufa kabla ya mama yao. Kama mama yao alianza kufa na wao si watoto wa baba huyo then hawana urithi zaidi ya kuomba kufanyiwa ihsani tu.
 

Iceberg9

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
22,609
42,577
Inategemea marehemu alikua anaishi katika misingi gani ya kiiamani na taratibu,mfano ni ya kiristo,uislamu au mila nk mfano waislamu watoto nje hawarithi ila pia Uislamu ina uhalalisha ndoa za mitaala , hawarithi kabisa ila kama marehemu alikua ni mkristo ina maana watoto wa njee wanarithi yani watoto wote wana haki kasoro mke wa njee ambapo dini ya kikristo hairuhusu maana ni ndoa ya mke mmoja na mume mmoja,
 
4 Reactions
Reply
Top Bottom