Baada ya anayejiita Wakala wake Kulikoroga Mchezaji Meddie Kagere amtuma msemaji wa Simba SC Manara kuusema ukweli wake huu kwa Wanasimba

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
"Kama Mchezaji wa Simba SC nimesikitishwa sana na Kauli za huyu Patrick Gakumba kuhusu Mimi na Uhusiano wangu na Kocha Gomez "

"Nikiri tu kwamba namjua Patrick Gakumba ila nashangaa ni kwanini kila mara anajitokeza kudai ni Wakala wangu "

"Ukweli ni kwamba Patrick Gakumba si Wakala wangu bali nilimtumia tu Kufanikisha Kusajiliwa Kwangu Simba SC "

"Sina kawaida ya kuwa na Wakala wa Kudumu na huyu nilimalizana nae Siku ile ile najjunga na Simba SC "

"Nawaomba Radhi sana Wana Simba SC wote kwa Usumbufu huo ila Patrick Gakumba si Wakala wangu kabisa "

"Namheshimu Kocha Gomez na sina tatizo nae na ni Rafiki yangu kabla ya Kukutana hapa Simba SC na namkubali mno "

"Nimeshawasiliana na Patrick Gakumba na kumtaka asiniharibie hapa Simba SC kwani ananishushia Heshima pia "

Maneno yote haya nimemkariri Msemaji wa Simba SC Haji Manara ( alias ) BUGATTI alipokuwa akifanya Mazungumzo na Kipindi cha Michezo cha Ufm ( Uhai FM ) na Mtangazaji Mussa Kawambwa Jr kutoka Azam Media Jioni hii ya leo kuelekea Mechi ya ASFC ya Kesho kati ya Mnyama ( Simba SC ) na Dodoma Jiji FC kutoka Mkoani Dodoma.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa Media Kubwa nchini Tanzania hebu ziwe zinaacha Kuhoji ' Wahuni ' kama huyu anayejiita Wakala wa Meddie Kagere aitwae Patrick Gakumba badala yake kukitokea ' sintofahamu ' yoyote ziwe ama zinamtafuta Mchezaji husika au Watafute Official Agents wao ili Kulinda ' Credibility ' ya Chombo husika na hata Mtangazaji ( Mwandishi ) Mwenyewe.
 
Kagere anamkataa wakala kwa kupenda au kashawishiwa?

Naona ni rahisi zaidi kwake kumkataa wakala kuliko kumkataa kocha, "undue influence" kwa wanasheria watakuwa wananielewa hapa.
 
Kagere ni mtu mzima na anachofanya ni kuweka sawa kwakua uyo wakala amezungumza ukweli na yeye Kagere anajua msg imefika, anacho kifanya kwa kauli yake ni kucheza na akili ya mbumbumbu fc ili ionekane yeye Kagere hana tatizo lolote ata akiwekwa bench.
Ki uhalisia Kagere na uyo wakala uwa wanaongea tena yanayo husu maendeleo yake ya mpira, kilicho ongelewa na wakala ndio msimamo halisi wa Kagere. Kitacho fuata ni mchezaji kuomba kisitisha mkataba Kama akipata dili linalo eleweka. Umri wa Kagere ni mkubwa hawezi kukubali kuozea bench wakati ndio anamalizia mpira wake.
 
Back
Top Bottom