Baada ya Alikiba sasa ni Nandy alalamika kushushiwa views Youtube

That is very stupid to accuse Diamond for such rubbish! Mwambieni aandike email support@youtube.com awaulize kwa nini views zinashuka, au aingie kwenye help forum a post topic au malalamiko yake hapo:

YouTube Community

But also, kitu ambacho hawa wasanii wenye magroup ya whatsapp wanaowatuma wafuasi wao waende ku watch videos kwa lengo la kuongeza views, sasa wao wana replay over and over kila baada ya few seconds then views zote zinakua nullified.

Kwa kawaida YouTube wanahesabu VIEW iwapo mtu una watch video for more than 30 seconds, chini ya hapo, inakua 0 hata kama ume watch mara 100, so usishangae ukawa na video ina views 1m then after 48 hours ikawa na 800k
Asante sana Mkuu, hii elimu bora sana kwa watu ambao huwa wanalalamika bila kuelewa kuwa help desk au youtube Mgt! ndio controller wa viewers na credits!!
Pia hawa wasanii wanapaswa kuelewa policies za youtube Mgt hasa katika suala la viewers, hii itaondoa malalamiko!!
 
Lawama zitaenda kwa diamond na crew yake..

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu waliofeli na masikini wa akili siku zote matatizo yao uwalalamikia wengine.Kuna clip moja niliona mtandaoni Kuna jamaa fulani akihojiwa baada ya kufeli mtihani wa kidato Cha nne wa mwaka Jana akaulizwa kwanini umefeli? akajibu serikali imesababisha nifeli akaulizwa Tena kwasababu gani?

Akajibu walimu wameshindwa kulipwa mishahara yao akaulizwa Tena shule yenu wamefaulu wangapi akataja 87 Kati ya 150 akaulizwa Tena Kama tatizo ni waalimu kutolipwa mishahara yao hao 87 wamefauluje? akashindwa kujibu
 
Watu waliofeli na masikini wa akili siku zote matatizo yao uwalalamikia wengine.Kuna clip moja niliona mtandaoni Kuna jamaa fulani akihojiwa baada ya kufeli mtihani wa kidato Cha nne wa mwaka Jana akaulizwa kwanini umefeli? akajibu serikali imesababisha nifeli akaulizwa Tena kwasababu gani? Akajibu walimu wameshindwa kulipwa mishahara yao akaulizwa Tena shule yenu wamefaulu wangapi akataja 87 Kati ya 150 akaulizwa Tena Kama tatizo ni waalimu kutolipwa mishahara yao hao 87 wamefauluje? akashindwa kujibu
WaTz tuna shida sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si awaulize Youtube mbona wana-respond faster sana wale jamaa. Asitulaumu sie tunaomsupport.
 
Uzuri ni kwamba You tube haisimamiwi na Wabongo, hivyo hawana sababu ya kuhujumu Mtu, tena Mbongo.

Nijuavyo mimi kuna utaratibu wa hizi hesabu, na sio you tube tu bali hata kwenye FACE BOOK, unaweza kuwa na marafiki 400 leo na baada ya siku chache unakuta wapo 340.

Kuna sababu kadhaa miongoni mwao ni UONGO, ambapo huenda imegundulika hao Marafiki 60 sio wenye akaunti HAI.

Pia hali yaweza kuwa mbaya zaidi kama akaunti yako imesha wekwa alama kama ina mambo yanayoendelea yasiyo ya kweli tofauti na Mwenzako asiye na alama...kwamba yaweza kuwa wote mna kasoro lakini wewe ukaumia zaidi.
 
Nimevumilia hii siku ya nne sasa... Uko youtube vinatokea vitu vya ajabu sana! Ni nini tatizo ni nini kwanini nikifikisha laki 9 viwers wanarudishwa nyuma mpaka laki 8 au 7 hii siku ya nne naona miujiza tu kwenyeaccount yangu.

Nilikuwa 934k now bimerudishwa asubuhi hadi laki 8 ni nini sitak kuhukumu watu naomba watu wa it mnisaidie kuna nini? Why huu mchezo unatokea wa ajabu tatizo ni nini? Na kama ni michezo mibaya ya fitna basi hewalaaaa.

Nandy alisha waandikia You tube na kuwauliza?
Kwanini ana kimbilia kuhujumiwa?
Nani amuhujumu? Kwa sababu zipi?
 
Kuna kila dalili hili lalamiko limeelekezwa mahali fulani kama wahujumu wa viewers. basi sawaah! Ngoja tukajazilize Jeje kwanza angalau ifike 6M ndani ya week 1 tutakuja kujibu tuhuma.

Ni kweli kabisa hapa ni wazi wanaelekezewa shutuma timu ya Diamond maana wao ndio huonekana ni watu wabaya sana kuliko wote hapa tanzania?
Huu ni ujinga ambao sikutegemea toka kwa Nandi
 
Ni kweli kabisa hapa ni wazi wanaelekezewa shutuma timu ya Diamond maana wao ndio huonekana ni watu wabaya sana kuliko wote hapa tanzania?
Huu ni ujinga ambao sikutegemea toka kwa Nandi
Hii itasababisha pia mashabiki wengi wa diamond kumchukia anaanza kujitengenezea nyufa mwenyewe na mashabiki wa diamond washaanza teyali kumuattack kwenye Instagram yake.
 
Watu wangine bwana wao wanajuwa Views You tube unaweza ukaongeza au kupunguza kama sauti ya Redio.
 
Back
Top Bottom