Baada ya afya yake kuimarika, Mama Janeth Magufuli aibukia kanisani

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
2,000
[HASHTAG]#HABARI[/HASHTAG] Baada ya afya yake kuimarika, Mama Janeth Magufuli aibukia kanisani.

====

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitaliMke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam

Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.

"Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.

"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa

Chanzo: EATV

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,680
2,000
Picha zinaongea mambo mengi sana.
Picha ya juu nimependa mshono wa huyo Mama mwingine aliyeshika "Misale ya Waumini" na tabasamu kubwa.Naona kashona Wax kwa mshono maridadi wa "kiutu uzima".Nafikiri alikuwa ana hamu ya kumshika First Lady lkn itifaki ikamkatiza

Lakini "suit" ya huyo mlinzi wa Mama wa kwanza nayo nzuri,na kwa kweli imekaa mwilini vizuri kiasi kikubwa.

Lakini nimetaka kujua,wale waliokaa juu ya uzio kule pembeni ni walinzi?Ndio wanalinda usalama wa hawa Wamama wawili?Naona wananing'inia kwenye uzio.

Hii picha ya chini na mke wa PM...(Hivi Mama Tunu Pinda yupo?)...Lkn nilitaka kupata ufafanuzi,PM mkewe ni mkatoliki na PM ni muislam?

Ni hayo tu kutoka katika picha hizo mbili
image.jpeg
image.jpeg
 
Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,116

View attachment 447716 View attachment 447717
To be holly honest:nimependa tabasamu la huyo mama,very free,liko wazi,dah
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
75,858
2,000
Picha zinaongea mambo mengi sana.
Picha ya juu nimependa mshono wa huyo Mama mwingine aliyeshika "Misale ya Waumini" na tabasamu kubwa.Naona kashona Wax kwa mshono maridadi wa "kiutu uzima".Nafikiri alikuwa ana hamu ya kumshika First Lady lkn itifaki ikamkatiza

Lakini "suit" ya huyo mlinzi wa Mama wa kwanza nayo nzuri,na kwa kweli imekaa mwilini vizuri kiasi kikubwa.

Lakini nimetaka kujua,wale waliokaa juu ya uzio kule pembeni ni walinzi?Ndio wanalinda usalama wa hawa Wamama wawili?Naona wananing'inia kwenye uzio.

Hii picha ya chini na mke wa PM...(Hivi Mama Tunu Pinda yupo?)...Lkn nilitaka kupata ufafanuzi,PM mkewe ni mkatoliki na PM ni muislam?

Ni hayo tu kutoka katika picha hizo mbili
View attachment 447716 View attachment 447717
Majibu kuhusu mke wa PM kuwa mkatoliki anayo THE BOSS.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom