Keagan Paul
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 292
- 1,000
Ushauri huu unatokana na ukweli kwamba kwa Media kama Wasafi kukumbwa na Misukosuko kama hii ya kufungiwa mara mbili ni mapema mno. Media haina hata miaka 5, Media wala sio Kongwe lakini inakumbwa na adhabu kama hizi mara mbili.
Kama ni kweli wanavyosema kwamba Mke wa Kusaga (Familia ya Kusaga) ana Hisa pale Wasafi basi nadhani ni wakati wao sasa kuingilia kati. Nadhani Diamond kama CEO wa Wasafi Media ameshindwa ku perform. Diamond ameshindwa kuvaa kofia mbili. Ndio maana mpaka muda huu ameshindwa kuzungumza chochote kuhusu swala hili, Anajichukulia yeye ni Diamond, Amesahau kwamba yeye pia ni CEO. Watanzania na Watazamaji (Mashabiki/Wapenzi wao) wanataka kusikia kutoka kwenye Management yao.
Kuna ambao mtasema mbona Media za Kusaga nazo huwa zinafungiwa, ni kweli zinafungiwa. Lakini kumbuka kuwa
Media za Kusaga zina zaidi ya miaka 20, Wasafi imeanzishwa juzi tu tayari imeshafungiwa mara mbili. Hii ni Kasoro kubwa.
Binafsi namkubali Diamond kwenye upande wa WCB lakini sio kama CEO wa Wasafi Media. Upande huu ameprove failure. Bado anataka kuendesha Kampuni kwa kutafuta KIKI. KIKI zibaki WCB na sio Wasafi Media. Na ndio maana hata aina ya usajili wa wafanyakazi unaofanyika pale utasikia wengi ni Washkaji zake wa Kitambo ambao performance yao sio kubwa Kiivoo. Kuanzia wakina Baba Levo, Mshana, wote walitakiwa wakapigwe Msasa kwanza la sivyo hii itakuwa sio mara yao ya mwisho kufungiwa.
Umejiuliza kwa nini Mara baada ya Gigy Money kushuka Jukwaani Wasafi wenyewe waliomba radhi? Maana yake hata wao wenyewe waliona kuna Kosa limefanyika. Je walishindwa kumwambia Gigy kule Back Stage kuwa Vazi lake halifai kwa Maadili yetu au Pale Jukwaani walivyoona mambo yameharibika walishindwa kukata matangazo ya LIVE? Walishindwa kukata kwa sababu hawana professionals wa kutambua Makosa kwa haraka na kuwahi kukata Matangazo.
Ukweli Watu wanaitetea na kuihurumia Wasafi Media kwa Sababu wanampenda sana Diamond, wengi wao ni Mashabiki wa WCB, kwa hiyo wanajikuta Automatically wanaipenda Wasafi Media na kuitetea, Lakini Media yenyewe kama yenyewe bado inashindwa kujitetea.
Au Nasema uongo ndugu zangu?