Baada ya ACP Kingai kuonja joto la kutoa ushahidi, tutegemee nini toka kwa ushahidi wa IGP Sirro?

Jana 15/9/2021, Tulishuhudia ACP Ramadhan Kingai akitoa ushahidi mahakani juu ya kesi ya kigaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, Tuliona namna alivyowashiwa Moto wa mahojiano na mawakili wa utetezi kiasi kwamba akaanza kujichanganya na kupelekea watu hapa jukwaani kuhoji CV yake!

Ikumbukwe kuwa, wakili msomi, Peter Kibatala, aliiomba mahakama kuwa IGP Sirro awe shahidi upande wa utetezi na ijumaa alitajwa rasmi kuwa mmoja Kati ya mashahidi upande wa utetezi!

Tutegemee nini kutoka kwa IGP Sirro?

Atahimili na kustahimili joto la kizimba, au naye atajichanganya?

___________________________________

NB: Kesi itaendelea Leo saa 4:00 asbuhi, ACP kingai akiendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.
Tuwekeeni hayo mahojiano tuone.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kusoma sheria hakuhusiani chochote na cross examination, pale wakili anakuwa uwanja wa nyumbani, Sirro ajiandae.
Nilichogundua humu watu wanafanya ushabiki kwenye masuala ya kitaaluma. Sheria ni taaluma siyo ushabiki wa mpira. Kuna Mawakili Mahakamani huwa wanawahoji mashahidi mambo ya kipumbavu ambayo hata hayahusiani na kesi ya msingi. Mwisho wa siku mteja wao akishindwa kesi, wanadai Jaji hakua fair.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Kuna uwezekano kwa 99% Sirro asitokee mahakamani, ili kukwepa kuaibika.
Kwa jinsi mwenzake alivyopelekeshwa jana, Sirro huenda akaachia Samadi mbichi pale mahakamani.
Kibatala :unachanja au huchanjiii???

RPC wa Simon Sirro : sijachnachannasijachijnnjjj

Kibatala:ha
 
Hatapata tabu yoyote kwa sababu ni shahidi upande wa utetezi, yaani atalazimika kumtetea Mbowe na wenzake...

Vivyo hivyo yule gaidi halisi aliyekuwa DC wa Hai Ole Lengai Sabaya ataitwa kumtetea Freeman Mbowe...!

Ukiwa upande wa utetezi hupati shida. Upande wa shida ni ule wa kubumba mashtaka halafu ulazimishwe na circumstance kuutetea uongo....
 
Tanzania nchi ya ajabu sana
Huku Hangaya anatangaza kuogombea 2025
Huku Mbowe mahakamani uhujumu uchumi na ugaidi
Huku Gwajima na chanjo
Huku baraza la mawaziri limefanyiwa marekebisho
Jua linazama na kiza kitafunika anga huku tukitegemea mapambazuko
 
Jana 15/9/2021, Tulishuhudia ACP Ramadhan Kingai akitoa ushahidi mahakani juu ya kesi ya kigaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, Tuliona namna alivyowashiwa Moto wa mahojiano na mawakili wa utetezi kiasi kwamba akaanza kujichanganya na kupelekea watu hapa jukwaani kuhoji CV yake!

Ikumbukwe kuwa, wakili msomi, Peter Kibatala, aliiomba mahakama kuwa IGP Sirro awe shahidi upande wa utetezi na ijumaa alitajwa rasmi kuwa mmoja Kati ya mashahidi upande wa utetezi!

Tutegemee nini kutoka kwa IGP Sirro?

Atahimili na kustahimili joto la kizimba, au naye atajichanganya?

___________________________________

NB: Kesi itaendelea Leo saa 4:00 asbuhi, ACP kingai akiendelea kuhojiwa na upande wa utetezi.
Tuombe ulinzi kwa mhe kibatala na wenzake

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini watuhumiwa walikutwa na madawa ya kulevya lakini maelezo hayo hayapo kwenye hati ya mashitaka? Au madawa ya kulevya yamehalalishwa siku hizi?
Kesi ya madawa ilo inarejea itatajwa soon ,kumbuka hii ni kesi mama vipo vikesi vidogo vidogo vya kutosha hadi mbowe afungwe

USSR
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom