Baada ya ACP Kingai kuonja joto la kutoa ushahidi, tutegemee nini toka kwa ushahidi wa IGP Sirro?

Jana 15/9/2021, Tulishuhudia ACP Ramadhan Kingai akitoa ushahidi mahakani juu ya kesi ya kigaidi inayomkabili Mbowe na wenzake, Tuliona namna alivyowashiwa Moto wa mahojiano na mawakili wa utetezi kiasi kwamba akaanza kujichanganya na kupelekea watu hapa jukwaani kuhoji CV yake!

Ikumbukwe kuwa, wakili msomi, Peter Kibatala, aliiomba mahakama kuwa IGP Sirro awe shahidi upande wa utetezi na ijumaa alitajwa rasmi kuwa mmoja Kati ya mashahidi upande wa utetezi!

Tutegemee nini kutoka kwa IGP Sirro?

Atahimili na kustahimili joto la kizimba, au naye atajichanganya
Sirro ni kukaza mzuri sana
 
Kuna watu wengi wameingia jeshini ni vipanga darasani na matokeo yao yalikuwa mazuri wengine ni hob
Siasa gani inayohitaji 'kichwa' kuwa mtu mkubwa?

Tunajua sifa za kujiunga na jeshi la polisi, na sababu za wengi kuingia huko…. hakuna mtu 'anayewaburuza' darasani akakimbilia jeshini.
 
Sirro anahold phd ya sheria udsm
Tangu lini mkuu?Unamaana anaitwa Dr.Sirro ,acha utani
Sirro kuanzia olevel hadi advance alikuwa anawaburuza watu kile ni kichwa hatari angeamua kuingia kwenye siasa angekua mtu mkubwa sana
Weeeeeee!Humjui hata kidogo amesoma na Baba yangu mdogo Kilaza tu !Degree zenyewe amesoma akiwa kazini.Tangu lini PT watanzania wakawa na akili darasani,Tena enzi zao walikuwa wanachukua waliofeli tu.
 
Kuna watu wengi wameingia jeshini ni vipanga darasani na matokeo yao yalikuwa mazuri wengine ni hob
Siyo Jeshi la polisi!!!Lakini pia siyo Jeshi la enzi hizo.Kwa sababu ya ukosefu wa ajira ni kweli Kwa Sasa kuna Polisi wasomi wazuri.Lakini za kina IGP Polisi waliingia wakiwa vihiyo.Hata huyo unaye mtetea aliingia akiwa na kidato cha sita Wala hakuwa na degree
 
Back
Top Bottom