Baada wa Watendaji wa Serikali za Mitaa Kawe 'Kutimka Mbio' Kuogopa 'Chatu' aliyeko katika pori la Chuo cha Tiba Lugalo msaada unahitajika

Mkuu unaniangusha bhana yaani unasema umekaa Lugalo halafu Hostel hupajui?

Hostel ni kule ambako zamani walikuwa wakiishi sana wale Askari Wahanga wa Vita ya Amini wa Uganda ( wengi wao wakiwa ni Vilema ) nyuma yake kuna Makaburi ila kwa sasa ndipo Kumejengwa Chuo Kikubwa cha Tiba cha MCMS kwa Ushirikiano na nchi ya Ujerumani ambapo kuna VIP Mortuary ambayo Hayati wa tarehe 17 Machi, 2021 alikuwa akilala na akiogeshewa hapo kabla ya kupelekwa Temeke Main Stadium Watu Kumuaga.
Hakuna alie kaa lugalo au kawe aseme hawajui hostel.
 
Taarifa ambazo GENTAMYCINE nimethibitishiwa na Mamlaka ya Ofisi za Serikali ya Mitaa Kawe na Mtendaji Mwandamizi kutoka Jeshini Kambini Lugalo kilipo Chuo chao cha Tiba cha MCMS ni kwamba kuna uwepo wa Chatu mkubwa kiasi cha Kutishia Maisha ya Watu.

Kwa takribani Siku tatu zimepita Wakazi wa Kawe (hasa eneo yalipo Makaburi) zamani kulikuwa ni Hostel na sasa Jeshi (JWTZ) limejenga Chuo chake cha Tiba Mamlaka ya Serikali ya Mitaa Kawe imekuwa ikipita Kuwatangazia Watu kuchukua Tahadhari (hasa kwa Watoto) na Watu waliokuwa na Mazoea ya Kukatisha huko Makaburini (zamani Hostel) kuelekea Coca Cola na Mwenge kutopita tena hiyo njia ili wasije kufanywa 'Kitoweo' Kitamu cha Chatu huyo.

Baada ya kupata Taarifa hii GENTAMYCINE niliamua kutembelea eneo la Makazi ya Watu ambapo nilibahatika Kukutana na Vijana Wawili ambao hupenda kupita hiyo njia ambao walinithibitishia kuwa ni Kweli Chatu huyo yupo na ni Mkubwa sana ambapo mara nyingi hupenda Kukaa juu ya Makaburi yaliyopo hapo.

Kumekuwa na Taarifa mbalimbali juu ya uwepo (ujio) wa huyo Chatu hapo ambapo wapo wanaosema kuwa alianza Kuonekana tokea mwaka juzi akiwa bado Mdogo baada ya Kutupwa huko Porini (Msituni) Lugalo na Wasukuma waliokuwa wakiwafuga wengine na kuwatumia katika Ngoma zao za Kitamaduni.

Watu wengine wanasema kuwa kuna uwezekano Chatu huyo akawa ameletwa na Maji ya Mto Mlalakuwa yanayopita hadi jirani na Kambi ya Lugalo, kule Golf Club mpaka JKT Mlalakuwa hivyo akanasa na kuamua kuanza Maisha yake eneo hilo.

Katika hali isiyokuwa ya Kawaida baada ya Watendaji wa Serikali ya Mtaa Kawe ( yenye Ofisi zake jirani na Soko jipya la Kawe ) walipotaarifiwa 'walijitutumua' kutaka kuonyesha 'Ushujaa' ambao hawana kwa kuamua kwenda 'Kavu Kavu' huko Msituni ( Porini ) Lugalo ( zamani Hostel ) ili Kumdhibiti.

Ila walipofika huko na Kumuona ndani ya dakika Moja mpaka Mbili hakuna aliyebakia hapo ambapo wote 'walitimka mbio' kwa kila Mtu kupita njia anayoijua ila Wote wakaja kukutania Ofisini huku wote wakiwa wameshika Viatu vyao Mikononi na wengine wakiomba Funguo za kwenda Msalani ( Chooni ) kujikagua kama wakati wakikimbia vile kwa Uwoga wa Kumuona Chatu labda kwa kutokujua ( Kihoro ) walijisaidia 'Kibaiolojia' vile walivyovihifadhi katika 'Vitambi' vyao.

Tafadhali naziomba Mamlaka husika hasa ya Jeshi (JWTZ) na Serikali ( kupitia Maliasili ) kulifuatilia hili upesi na Kumtoa upesi huyo Chatu hapo Porini ( Msituni ) kwani wengine ( GENTAMYCINE ) katika hayo Makaburi ( ya zamani Hostel ) nimemzika Mama yangu Mdogo na nilikuwa napanga kwenda 'Kumfagilia' na Kumsalimia 'Kimaombi' Siku za Usoni.

Lakini Taarifa hii imenishtua na Kuniogopesha kwenda huko ili Chatu asije 'Kuupiga Mwingi Kwangu' na nikawa Historia hapa JamiiForums na hata nikaikosa 'Derby' ya Jumapili ijayo huko Mkoani Kigoma ambapo najua Mugalu, Boko, Chama, Kagere na Miquissone wanaenda 'Kuninyooshea' na Kunifundishia Watu Adabu kwa Kipigo cha Mwana Ukome.

Kwa wale wenye Blogs zenu na Media zingine mbalimbali tafadhali siwazuii Kuichukua hii Taarifa yangu na Kuitumia ila nawaomba tu mkiitumia toeni 'Credit' kwa Mtandao huu wa JamiiForums na Mimi GENTAMYCINE niliyeileta ( iweka wazi ) na acheni Kudanganya kuwa mmeitafuta nyie kwani mnakuwa hamtendi Haki na Kutuvunja Moyo Watu tunaopenda Kutafuta Taarifa na Kuzianzishia hapa JamiiForums mzijue hata kama hakuna tunacholipwa ila tunajua tutalipwa vikubwa (zaidi) na Mwenyezi Mungu Siku moja atakayoipenda na kuichagua Yeye.
Utakuta chatu kesha fukua maiti na kuitafuna.
 
Back
Top Bottom