comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 8,222
- 5,946
Simu yake iliita kwa Bahati mbaya wakati wa ibada akiwa kanisani.
Mchungaji alimfokea.
Waumini walimzonga baada ya maombi ya ibada Wakati anarudi nyumbani, njia nzima mkewe aliendelea kumsema kwa kutokuwa makini Akajisikia vibaya sana, huzuni, na aibu juu. Hakutia miguu tena kanisani . Jioni yake, ili kupoteza mawazo, alikwenda bar.
Aliagiza bia, akaiweka mezani. Kwa kuwa alikuwa na mawazo mengi, akaigusa pombe ikamwagika .
Muhudumu alikuja, akampa pole kwa unyenyekevu, na akafuta meza kiustaarabu, kisha akamfuta jamaa ilipommwagikia kiunyenyekevu. Meneja wa bar ile alimpa jamaa bia ya ofa kufidia iliyomwagika, Muhudumu wa kaunta alipomletea alim'busu akim'bembeleza, "USIJALI HAKUNA AMBAYE HANA MAKOSA”
Jamaa hajawahi kukosa 'ibada' katika bar hiyo tangu siku ile.
SOMO:Unavyowatendea watu kunaweza kujenga au kuwabomoa, hasa wanapokosea.