Ba Ndugu, Kweli Maisha hayana Kanuni

mbombo mte

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
707
250
Wana Jf, nimekuwa mara nyingi natafakari nichukuwe kanuni gani jinsi ya kuishi ktk maisha, lakini nimekuja kuona hakuna kanuni yoyote. Labda ba ndugu nisaidieni maana:

1. Nimeona wenye haraka haraka wamepata mafanikio,
2. Jamaa walivumilia mwishoni wakaja kula zilizooza badala ya mbivu,
3. Kuna wegine walikuwa na subira wakaja kumbulia nuksi na balaa,
4. Na ambao hawakusikia la mkuu wala hawakuvunjka guuu,
5. .................................................................
6......................................................................,


EBU NISAIDIENI WANAJF.
 

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Bahati mbaya sijaona kichani wala miguuni hiyo hata kiwiliwili nimeshindwa kukiona. Punguza haraka kidogo usomeke
 

Lolipop

JF-Expert Member
Oct 30, 2013
349
170
Usiige maisha ya wenzio na wala usikimbizane nao wakati una mwendo wa konokono
 

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,000
Life is all about choices and sacrifices. BUT timming is everything. Mfanikio na failure zote kwenye maisha yako ni matokeo ya choices, decisions na sacrifices ulizofanya. Ila la muhimu zaidi kwenye maisha ni kutambua na kuweza kusoma alama za nyakati.

Nitatoa mfano: Kulikuwa na umuhimu gani kwa zito kabwe kutangaa kugombea urais wakati hajafikisha miaka 40 na wakati chama chake chote kiko kwenye kampeni za uchaguzi kule arusha (kufuatia kifo cha sumari). AU kulikuwa na umuhimu gani kwa zito kugombea uenyekiti wakati yeye alikuwa kwenye top 4 ya chama chake (4th in command). Mazila na aibu zote anazopata zito sasa ni matokeo ya choices, decisions na sacrifices alizofanya. Ila la muhimu zaidi kushindwa kwake kutambua na kuweza kusoma alama za nyakati. Wakati wenzake wako bize na mambo ya chama yeye always yuko bize na mambo yake binafsi tu ya kutaka kuwa mwenyekiti wa chama na rais wa nchi (maana yake anadhani yeye ni bora kuliko kila mtu kwenye chama chake na ni bora kila mtu tanzania nzima (Umimi)
 

afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,149
2,000
Usifuate kanuni za wengine walizotengeneza.
Fuata ya kwako..

Ulizaliwa mwenyewe utakufa mwenyewe, basi ishi na kanuni zako mwenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom