B.O.T, kuanzisha noti ya sh.20,000, nini madhara yake?

Leonard Robert

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
11,059
7,189
kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea nchini bila ufumbuzi wa tatizo hili,imepelekea thamani ya fedha za ndani kushuka..ni wazi sasa ukienda na sh.elfu kumi sokoni haitoshi kwa mahitaji ya nyumbani kwa siku.
Ni tofauti na miaka ya nyuma,kwani hadi mwaka 1993 shiling ya Tanzania ilikua na thamani kubwa angalau.
Kutokana na tatizo hili BOT yaweza kuanzisha noti mpya ya sh.elfu ishirini (20,000) kwenye mzunguko ili kupunguza hadha ya kubebelea noti nyingi kununua vitu vichache.
Je nini madhara yake(hasara na faida kama zipo) kiuchumi na kijamii?
 
wataalamu wa uchumi pia mchango wao ni muhimu,ili sisi wananchi wa kawaida tujue implication ya hili.karibu.
 
Mie nilikuwa najua BOT wameanzisha kumbe ni wazo lako!
 
Ndio maana kuna mtu (jina kapuni) aliwahi kuyaita mamilioni ni "vijisenti"> Nadhani wakati ule hakusomeka vizuri, Maana yake ndio hiyo, unakwenda Sokoni na T/Shs. elfu kumi unaishia kununua mboga tu.
 
ukiiweka hiyo 20000 kwenye mzunguko dola itabadilishwa kwa 2000 za kibongo maana wao wameshindwa kucontrol mfumuko wa bei wanataka kuleta mambo ya ajabu na kitu kibovu kupita vyote ni kuchanganya siasa na taaluma za watu sijui prof beno anafanya nini hapo majengo pacha..
 
kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea nchini bila ufumbuzi wa tatizo hili,imepelekea thamani ya fedha za ndani kushuka..ni wazi sasa ukienda na sh.elfu kumi sokoni haitoshi kwa mahitaji ya nyumbani kwa siku.
Ni tofauti na miaka ya nyuma,kwani hadi mwaka 1993 shiling ya Tanzania ilikua na thamani kubwa angalau.
Kutokana na tatizo hili BOT yaweza kuanzisha noti mpya ya sh.elfu ishirini (20,000) kwenye mzunguko ili kupunguza hadha ya kubebelea noti nyingi kununua vitu vichache.
Je nini madhara yake(hasara na faida kama zipo) kiuchumi na kijamii?

Kuchapisha noti kubwa siyo suluhisho la kupunguza mfumuko wa bei; BoT na serikali inatakiwa isimamie/ifanye mambo yafuatayo:

1. Iongeze kodi kwenye bidhaa zinazoagizwa toka nje ili kuwafanya watanzania wapende bidhaa za ndani (kutokana na unafuu wa bei) na hivyo kuchochea ukuaji wa uzalishaji mali;

2. Iweke marufuku ya uagizaji wa bidhaa tunazoweza kuzalisha wenyewe kama za vyakula, ngozi, mbao nk. Ni aibu mahoteli yote kujazana juice za Afrika kusini hata kwa yale matunda yanayopatikana hapa nchini. Kenya wao wananunua mananasi yetu na kutuletea juice za mananasi.

3. Itumie vema fursa tulizonazo za kuuza bidhaa nje ya nchi kama vile mkataba wa AGOA nk. Ni bahati mbaya sana hizi fursa wanaozitumia ni jamii ya kiasia watanzania wengi hawazijui wala hakuna jitihada za kuwafungua macho kuzielewa.

4. Ijengee wananchi wake uwezo wa kuzalisha bidhaa mbalimbali mfano kupitia SIDO na VETA, kuwepo na viwanda vidogo vidogo kwenye miji midogo kwa ajili ya kusindika mazao yanayopatikana sehemu ile tayari kuuzika kama bidhaa kamili. Mfano bei ya kuuza vitunguu kwa gunia ni toafauti na ukifungasha uzazo wa kilo moja moja na kuuza kwenye maduka makubwa

kutokana na mfumuko wa bei unaoendelea nchini bila ufumbuzi wa tatizo hili,imepelekea thamani ya fedha za ndani kushuka..ni wazi sasa ukienda na sh.elfu kumi sokoni haitoshi kwa mahitaji ya nyumbani kwa siku.
Ni tofauti na miaka ya nyuma,kwani hadi mwaka 1993 shiling ya Tanzania ilikua na thamani kubwa angalau.
Kutokana na tatizo hili BOT yaweza kuanzisha noti mpya ya sh.elfu ishirini (20,000) kwenye mzunguko ili kupunguza hadha ya kubebelea noti nyingi kununua vitu vichache.
Je nini madhara yake(hasara na faida kama zipo) kiuchumi na kijamii?

hicho mkuu kuna kitu kinaitwa inflation kwanza kabisa pesa yetu itashuka thamani mara mbili ya hiyo na pia kutakuwa na mfumuko wa bei sana kwa hiyo tujiaandae hasa kwani inatakiwa tuzalishe sana na pia kuuza sana nje kuliko kuagiza (favorable balance of payment).
 
Kabla ya hii nilisikia itatengenezwa not ya 50000, bt nothing...leo noti ya 20000....hivi kwanini hamuweki source ya hizi info zenu..?? yaani nyie mnalala mkiamka tu mnakuja na vitu vya kufikirika?? Leo nimemsikia gavana B. Ndulu akitoa sababu kwanini fedha yetu inashuka thamani...na sababu kubwa alisema fedha za kigeni zimepungua na akainisha hizo fedha za kigeni zinaingia kwa njia gani...akasema
1. Kutokana na migodi ya dhahabu na madini mengine(sekta ya madini) na akataja amount per yr inayopata serikali yetu
2. Njia ya Utalii kutokana na mbuga zetu
3. Akasema njia ya Uchukuzi mizigo bandarini na sehemu nyingine
4. Akasema ni Kwenye mazao ya chakula na biashara zitokazo ndani ya nchi yetu
5. Sikumbuki vizuri alisema nini...

Lakini hakusema kwamba eti tatizo hili inabidi iundwe noti ya 20000 ili kukabiliana na deflation/inflation iliyopo!! Toeni source kwa taarifa zenu JF!!
 
Na wale wanaoagiza noti zichapishwe wtapata 10% yao toka kwa printer watakae mpa tenda
 
unajua hata mimi nilidhani ni hivyo! duh, vichwa vingine bwana! ila sidhani kama tumeshafika kwenye hatua hiyo, nadhani bado!
Mie nilikuwa najua BOT wameanzisha kumbe ni wazo lako!
 
hicho mkuu kuna kitu kinaitwa inflation kwanza kabisa pesa yetu itashuka thamani mara mbili ya hiyo na pia kutakuwa na mfumuko wa bei sana kwa hiyo tujiaandae hasa kwani inatakiwa tuzalishe sana na pia kuuza sana nje kuliko kuagiza (favorable balance of payment).

kuuza mbona tunauza tena sana,labda kuhusu kununua maana vitu vingi tunaagiza,hivi wenzetu wa kenya wao wanafanyaje wajameni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom