Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

Hii ni mara ya pili akitoa kauli juu ya hili. Mara ya kwanza alifanya hivyo mwaka 2016.

Soma Zungu: Miamala ya M-Pesa kwa mwaka ni trilioni 50, wananchi tulipe kodi tuache kulia

 
Badala ya kupendekeza wafutiwe posho za kukaa Bungeni ili kuipunguzia serikali mzigo, anapendekeza aina nyingine ya kodi wakati kuingia tu mtandaoni tunakuwa tumelipa kodi kupitia vifurushi!!

Binafsi niliwahi pendekeza wazo linalofanana na hili ila nilelenga liwe kwa mambo ya hiari hasa Bima ya Afya kwa kila mtanzania atakaekuwa tayari kuchangia kupitia simu yake.

Serikali kupitia simu za mkononi, inaweza kukusanya fedha na kuanzisha Mfuko(Fund) wa kugharamia Bima ya Afya na Elimu ya Juu kwa Watanzania wote

 
Amezengua kusema kodi ya uzalendo

Angesema tu serikali ipanue wigo kwa kufanya uwekezaji mpya wa makampuni mapya ya simu tena Yale shindani yaje kuongeza kodi lakini sio kodi ya simu kila siku hii napinga.

Huwezi ukamkata mtu kila siku 50/= Kuna watu hawaweki vocha kabisa ila wanawasiliana.

Labda kama unaongeza V.A.T kwenye vocha ambayo mpaka sasa ipo..
 
Mbunge wa ilala Azan Zungu amependekeza kuwepo na kodi ya UZALENDO itakayo katwa ktk mitamdao ya simu .

Amesema ikikatwa kwa kila mtanzania anayetumia simu ya mkononi kama chanzo kipya cha mapato kwa serikali.

Kwa mujibu wa mbunge huyo kiasi hicho kikikatwa kwa watanzania millioni 30 kati ya woote waliopo nchini serikali itaweza kujipatia sh billioni 540 kwa siku.

Nini maoni yenu watanzania wenzetu watumiaji wa rununu?

Chanzo Nipashe.
 
yan watu wanaona kulipwa hela nyingi za hapo bungeni wameridhika na hali hawajue huku tunateseka na maisha sisi tulio wachagua wanatukandamiza tu mimi naomba serekali ipunguze mishaara ya wabunge ili wawe na mawazo chanya kwa jamii.
 
Kapumbavu sana haka kazee
Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu ametaka kuwepo na kodi ya uzalendo itakayokatwa katika mitandao ya simu kwa kila Mtanzania kwa siku kama chanzo kipya cha mapato kwa Serikali.

Amesema kiasi hicho kikikatwa kwa Watanzania milioni 30 kati ya wote waliopo nchini huweza kufikisha shilingi bilioni 540 kwa kila siku.

View attachment 1758510
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom