Aziz P. Mlima.. Almost ambassador?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,987
Nimepokea habari hizi za unyeti wa ndugu yetu Dr. Aziz Ponary Mlima ambaye nusura aukwae ubalozi wetu kwenye mojawapo ya nchi za Scandinavia. Bahati mbaya (sijui ni kwake au kwa nchi) ni kuwa wenye nchi yao kule walimkataa kwa sababu ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wetu!

Labda hili suala la dual citizenship inabidi tulifikiria jinsi litakavyofanya kazi kwa public servants wetu isije kutokea yale ya Fujimori kule Peru!

Thanks ka nzi!
 
Mimi na wewe hatujui labda kadri siku zinzvyokwenda ndio tunaweza kuona akateuliwa kuwa Balozi
 
Ubalozi katika nchi za Scandinavia ni mmoja tu. Balozi aliye Stockholm anawakilisha nchi za Scandinavia na Baltic. Hivi inawezekana kweli dual citizenship ikawa ni tatizo au kuna lingine?

Huyu Aziz ni nani lakini?

Amandla......
 
Fundi Mchundo,
Sijui kwa nini Mwanakijiji ameamua kutomwaga mtama wote ukumbini. Hakuna lingine zaidi ya dual citizenship. Namwachia Mwanakijiji atujuze zaidi.
 
Kama amekataliwa na wenyeji wetu, ni jambo la kushukuru maana hastahili hii kazi.

Yeye ni mchumi, anahitajika nyumbani sio ubalozini. Kuna career diplomats kibao wenye uwezo ambao JK hawataki maana sio wapambe wake.

JK aache kutoa kazi kwa kujuana bali azitoe kulingana na mahitaji yetu na uwezo wa wahusika.
 
Mwanakijiji,

..isije ikawa wamependekeza jina la Dr.Mlima kwa nchi ambayo wanajua atakataliwa.

..kuna jamaa aliniambia Dr.Sherrif alishaukana uraia wa Tz, lakini akateuliwa balozi wa Tanzania Saudia, na hakuwekewa kikwazo chochote.

..labda kwa huyu Dr.Mlima wangeanza na kumpeleka nchi kama Saudia,Oman,au UAE, ambako hawaulizi maswali mengi.

NB:

..haya mambo yalishamkuta Balozi Bandora[alikuwa balozi wetu Lagos] baada ya Rwanda kumteua kuwa mwakilishi wao Ujerumani.
 
inadaiwa yeye ni raia wa huko huko tayari.. sasa nchi inampendekezaje raia wa nchi nyingine kuwa balozi wake?
 
Mzee Mwanakijiji,

..nahisi jamaa yako kaingizwa mjini huyo.

.kama anautaka ubalozi aombe na ang'ang'anie apelekwe Middle East ambako hawana longolongo/hawachunguzi kama wanavyofanya jamaa wa European Union.
 
hapa ndiyo tatizo la uraia wa nchi mbili labda pia litaonekana. Je, tuko tayari rais wetu awe ni raia wa Tanzania na Kenya at the same time? au wa Rwanda na TZ at the same time au nchi nyingine yoyote? Vipi kuhusu Ubunge, Uwaziri, Ukuu wa Jeshi, vyombo vya usalama n.k?
 
Kuna watu mahala flani wanaolipwa kufanya vetting yanapojitokeza mapendekezo ya teuzi kama za huyo Mscandinavia mwenye asili ya Tanzania.Sasa sijui tatizo ni uzembe wa hawa jamaa wa vetting,kupuuzwa kwa mapendekezo/ushauri wao (kama wanafanya hivyo at all) au ni mlolongo wa ubabaishaji uliotawala takriban kila korido la utawala wa JK na CCM yake.

Kwa mwenendo huu I wouldn't be surprised Mullah Omar akapendekezwa kuwa Balozi wetu somewhere.

As to dual citizenship,encouraging news is Membe looks to be in favour of the idea,na hilo lina umuhimu wa kipekee katika nchi inayoendeshwa na matakwa ya watawala
 
hapa ndiyo tatizo la uraia wa nchi mbili labda pia litaonekana. Je, tuko tayari rais wetu awe ni raia wa Tanzania na Kenya at the same time? au wa Rwanda na TZ at the same time au nchi nyingine yoyote? Vipi kuhusu Ubunge, Uwaziri, Ukuu wa Jeshi, vyombo vya usalama n.k?

Hakuna tatizo na uraia wa nchi mbili. Cha muhimu ni kuandika sheria zinazoweka bayana kuhusu watu wenye uraia wa nchi mbili na kazi na nafasi wanazoweza kushika ktk serikali yetu. Mbona sheria za Marekani ziko wazi kuhusiana na hilo ingawa wao ktk baadhi ya ngazi za nafasi za zerikali nadhani mtu anaweza akawa na huo uraia wa nchi mbili isipokuwa uraisi.

Tusichukulie visingizo kama hivi kunyima watu uraia wa nchi mbili.
 
Mwanakijiji,

..mbona tumeshawahi kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania wakati wa utawala wa Mwalimu?

..Herbert Chitepo, raia wa Rhodesia, na Raisi mwanzilishi wa Zanu-PF, aliwahi kuwa DPP.

..kuna jamaa mwingine anaitwa Akena alikuwa DCI sina hakika kama alikuwa raia wa Tanzania.
 
Ooh jamani,ameukosa hivi hivi!sasa kama sababu ni hizo hilo pemdekezo lilitokaje wakati hakuwa na sifa?
 
Ooh jamani,ameukosa hivi hivi!sasa kama sababu ni hizo hilo pemdekezo lilitokaje wakati hakuwa na sifa?

Tatizo la kutokuwa na sifa haliko kwa hao wascandnavia,tatizo liko kwetu,na unaweza kuona wasacandnavia bado wanatufundisha namna ya kufuata sheria zetu sisi wenyewe.
Unless serikali iwe either imefanya utumbo kwa kutokuwa makini,ama 'Ilidhani" kuwa imesha pitisha sheria ya uraia wa nchi mbili.
 
Mwanakijiji,

..mbona tumeshawahi kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania wakati wa utawala wa Mwalimu?

..Herbert Chitepo, raia wa Rhodesia, na Raisi mwanzilishi wa Zanu-PF, aliwahi kuwa DPP.

..kuna jamaa mwingine anaitwa Akena alikuwa DCI sina hakika kama alikuwa raia wa Tanzania.

kwa hiyo unafikiri tunaweza kuwa na Rais ambaye si Mtanzania? sijazungumzia tatizo la kuwa na mtu ambaye si Mtanzania kushika nafasi mbalimbali hata Zanzibar waliwahi kukopa Jaji Mkuu kutoka Nigeria???

Marekani haina uraia wa nchi mbili kama watu wanavyoamini; Marekani inatambua uraia wake tu.
 
Tatizo hapa si uraia wa nchi mbili bali Scandinavia wamemkataa wakisema raia wao hawezi kuwa balozi katika nchi yake mwenyewe. Hata kama Tz tungekuwa na uraia wa nchi mbili bado ingekuwa kikwazo kwa Dr Azziz. Tatizo Dr Azziz hakuwa mkweli kwa serikali ya JK, alitakiwa aseme kwamba yeye kisheria ni raia wa (nchi kapuni) Scandinavia kabla JK hajapeleka maombi....usiri ndio umeumbua serikali.
 
Mwanakijiji,

..mbona tumeshawahi kuwa na Jaji Mkuu ambaye siyo Mtanzania wakati wa utawala wa Mwalimu?

..Herbert Chitepo, raia wa Rhodesia, na Raisi mwanzilishi wa Zanu-PF, aliwahi kuwa DPP.

..kuna jamaa mwingine anaitwa Akena alikuwa DCI sina hakika kama alikuwa raia wa Tanzania.
jokaKuu,
Akena alitoka Uganda. Na hiyo ilifahamika. Hakimu Mkuu Georges ambaye alitoka Trinidad and Tobago aliajiriwa ikifahamika kuwa si raia lakini baada ya uhuru hatukuwa na wanasheria wa kutosha kujaza nafasi muhimu kwa hiyo wengi walichukuliwa kutoka nchi za Commonwealth wakiwemo Waghana na Wanigeria. Katika suala hili tofauti ni kwamba huyu ni Mtanzania aliyekwishachukua uraia wa kigeni na kwa bahati mbaya akateuliwa kuwa balozi wa nchi hiyo hiyo ya kigeni. Inavyoonekana Watanzania walikuwa hawajui kuwa mwenzetu kishajilipua na alipopewa uteuzi huo hakusema kuwa tayari ni raia wa kule. Sasa wenyeji wakastukia wakasema hatuwezi kumchukua raia wetu awe balozi wa nchi yenu wakampa ofa ya kukana uraia ule akakataa. Hapo ndipo utamu ulipo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom