Aziz Cargo wa Facebook mwenye namba 0719639731 ni mwizi na tapeli wa kwenye mtandao

kemi2011

JF-Expert Member
Dec 25, 2013
735
290
Kuna MTU yuko Facebook anajiita Aziz Cargo, anatangaza kuuza bidhaa kwa bei ya chini sana na kwamba anampelekea mteja mzigo wake popote alipo Tanzania.

Jamani MTU huyu ni tapeli na mwizi mkubwa namba anayotumia ni 0719639731 Mimi nimeishaibiwa

Kama kuna MTU anajua namna ya kukamata matapeli na wezi wa mitandao plse saidia kabla hajawaliza wengi.

Akipokea pesa baada ya mda mfupi anakublock, kuweni makini
 
We acha tu, ni kweli Hata Mimi najishangaa!

Ni mwizi jamani tusaidiane akamatwe, wengi wamelizwa
 
Pole sana siwezi kukulaumu nadhani utakuwa mwalim kwa wengine watz bado sana kwenye biashara za mitandao
 
Mmmh mjini akili tu nguvu shamba endeleeni kutuita tu wanaume wa dar. Pole lakini mkuu
 
Watanzania wanapenda virahisi wanapenda slope,hawawapigaji wanatumia advantage hiyo hiyo...kuwakamata wapenda virahisi
Kuna jamaa unakuta anauza Mac Pro Book with retina display nikauliza shilling ngapi akaniambia Laki na nusu, nikamuuliza unajua unachouza akajibu hii ndio bei. Yaani product ya karibu Mill 3 anauza Laki na nusu na sie waswahili kwa kupenda be rahisi ndio maana tunapigwa na hawa vibaka uchwara.
 
Ukimshtaki lazima na wewe uwe makini
Usije kuwa ni miongoni mwa wakwepa Kodi

Halafu JF hasa vituko,yaani kwenye kufanya maamuzi upo kivyake ila ukiisha ibiwa ndio unakuja humu mbiooooo
We mtu atakuwa Agent wakati hata Ofisi hana,usajili hana na wewe unatuma pesa kilainiiiii
 
We acha tu, ni kweli Hata Mimi najishangaa!

Ni mwizi jamani tusaidiane akamatwe, wengi wamelizwa

Wakati unataka kumtumia pesa ulitupa taarifa!? Ujinga huu peleka Facebook! Mlikokutania! Sio huku kwa GT.
 
Usinunue bidhaa bila kumuona na kuona bidhaa kama upo mbali mtumie hata mtu unae mfahamu SITAKI KUSIKIA MAMBO YA KUIBIWA TENA KWA UZEMBE UZEMBE
 
Wakati unataka kumtumia pesa ulitupa taarifa!? Ujinga huu peleka Facebook! Mlikokutania! Sio huku kwa GT.

Kila siku tunawausia humu ila wakishaibiwa ndo wanakuja kulialia e Commerce ipo ulaya pekeyake huku ni utapeli tu eti mtu unamtumia hela hajawahi kumuona kama si wenda wazimu ni nini
 
Ustaarabu wa e-commerce upo ulaya kwa BINADAMU. Lkn siyo huku afrika tunakoishi WATU.
 
Sasa kwann umlipe pesa kabla ya kupokea mzigo

Uzembe ,muache apige pesa Aziz wa watu
 
Ukimshtaki lazima na wewe uwe makini
Usije kuwa ni miongoni mwa wakwepa Kodi

Halafu JF hasa vituko,yaani kwenye kufanya maamuzi upo kivyake ila ukiisha ibiwa ndio unakuja humu mbiooooo
We mtu atakuwa Agent wakati hata Ofisi hana,usajili hana na wewe unatuma pesa kilainiiiii
Maamuzi yenyewe wanafanya Facebook , wakishadhulumiwa wanakumbuka jf
 
Wewe wa mikoani ulianzaje kumtumia pesa mtu ambaye humjui? Wacha mkome mnapenda vya dezo mno!! Sasa unashitaki JF ili tufanyeje? Hata kama unatupa tahadhari hapa hawapati kitu maana ni kwa great thinkers ndo maana wanakimbilia kwa mazombie ya facebook!
 
Ukweli ulio wazi ni kwamba matapeli jinsi wanavyo fanikiwa kutapeli,ndio chachu ya kutafuta njia nyingine mbadala ya kutapeli. Kamwe utapeli hautaisha mpaka wenye nia,na hamu ya kutapeliwa watakapo pungua au kuisha.
 
Back
Top Bottom