Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,913
- 30,254
- Thread starter
- #401
Njiwa,hakuna
hakuna anayekuchagulia , bali weye ndiye unajarobu kuwachagulia watu waamini kipi na kuacha kipi! weye kama unaona hizi hekaya ! tuache na hekaya zetu! wewe chapa lapa tu! .. haina haja ya kufanya vurugu ndani ya thread
Ndugu yangu Njiwa historia hii niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes
imeumiza wengi.
Sababu kubwa ni kuwa kwa wale ambao walikuwa wageni wa historia ya
TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, sahihisho lile la historia
iliyozoeleka iliwapiga kama dhoruba inayokuja ghafla tena usiiku watu wote
wamelala.
Jinsi walivyodhani na kuaminishwa ikaja kuwa ni kinyume sana tena sana.
Katika blog yangu www.mohammedsaid.com kuna makala zinazohusu gazeti
la Africa Events (London) gazeti ambalo lilichapa kwa mara ya kwanza makala
yangu iliyoeleza vipi TANU iliundwa na watu gani walikuwa washiriki wakuu.
Kupitia gazeti hili niliweza kupata uwanja huru wa kuandika historia ya TANU
kama nilivyoifahamu.
Atakae kujua yaliyopitikana miaka ile na aingie kwenye blog afanya search,
''Africa Events,'' makala hizo zote atazipata hapo.
Naweka link ya baadhi ya niliyoandika kuhusu AE na mengi yapo hapa JF:
- Mohamed Said: KUTOKA JF: AFRICA EVENTS LILIPOCHAPA KUMBUKUMBU YA ABDUL SYKES 1988
- Mohamed Said: KUTOKA JF: AFRICA EVENTS NA HISTORIA YA TANU 1988
- Mohamed Said: KUTOKA JF: AFRICA EVENTS NA MISUKOSUKO YAKE
- Mohamed Said: KUTOKA JF: GAZETI LA AFRICA EVENTS TOLEO LA MARCH/APRIL 1988 LILIPOKUSANYWA NA KUTIWA MOTO
kama wengi mfano wa yeye, historia hii inawataabisha.
Lakini katika wote ambao waliumia khasa na kwa kweli kwa yale mapya yaliyokuwa
katika kitabu cha Abdul Sykes ni mwalimu wangu Prof. Haroub Othman.
Prof. Haroub alimuomba Mwalimu Nyerere na yeye aandike kitabu kiwe jibu
la kitabu changu.
Wanamajlis,
Hekaya sikuandika mimi.
Hekaya iliandikwa na Chuo Cha Kivukoni walipochapa kitabu cha Historia ya TANU
1954 - 1977 na ndani ya kitabu kile wakafuta wazalendo wote waliopigania uhuru
wa Tanganyika wakabaki na Mwalimu Nyerere peke yake.