Azinduka Toka Kwenye Koma na Kuanza Kuzungumza Kijerumani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azinduka Toka Kwenye Koma na Kuanza Kuzungumza Kijerumani

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wednesday, April 14, 2010 9:03 PM
  Msichana mmoja wa nchini Croatia amewashangaza watu wengi baada ya kuzinduka toka kwenye koma baada ya kupoteza fahamu kwa masaa kadhaa akiwa ameisahau kabisa lugha yake halisi na kuanza kubonga kijerumani kama vile alizaliwa nacho. Msichana huyo ambaye alipoteza fahamu kwa masaa 24 wiki mbili zilizopita, amewaacha madaktari wakiumiza vichwa kutokana na hali aliyo nayo.

  Msichana huyo alizinduka akiwa ameisahau kabisa lugha yake ya Croatia na kuanza kuzungumza kijerumani fasaha kama vile alizaliwa nacho.

  Wazazi wake walisema kuwa msichana huyo alikuwa akijifunza kijerumani shuleni na pia akiangalia shoo za kijerumani kwenye luninga lakini kijerumani kilikuwa hakipandi kabisa akishindwa hata kuziunga sentesi kifasaha.

  "Huwezi kujua ukizinduka toka kwenye koma ubongo utakuwa katika hali gani", alinukuliwa mkurugenzi wa hospitali ya KB Hospital ambayo msichana huyo alikuwa amelazwa.

  Madaktari kadhaa wamejaribu kumfanyia uchunguzi msichana huyo lakini wameshindwa kujua chanzo cha hali iliyomtokea.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4353426&&Cat=2
   
 2. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndo maajabu ya dunia hayo.
   
 3. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh kazi kwelikweli!
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,992
  Trophy Points: 280
  haya sometimes ni mambo yasiyo na mashiko, huo ni uongo uliodhahiri, kama huyo mama alikuwa hajuhi Kijerumani kabisa amewezaji kukuongea?
   
 5. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  hii mada ungeiweka tarehe 01/04 ndo siku muafaka
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Naona haya ndo maajabu ya Musa
   
 7. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hiyo, mpya kabisa.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,256
  Likes Received: 21,956
  Trophy Points: 280
  Hiyo kweli kabisa.
  Kuna ndugu yangu alipoteza fahamu kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya ajali iliyomuuza vibaya kichwa chake.
  Alipozinduka akapoteza kabisa kumbukumbu zake binafsi ikiwa ni pamoja na kusahau jina lake.
  Lakini watu wengine wote aliweza kuwakumbuka na kukumbuka mambo yao.
   
 9. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakuna maajabu yoyote ya dunia ,.ni study ya ubongo tu ,.kuna seheme yenye uwezo wa kutunza kumbukumbu hata za utotoni,kama hakuzaliwa ujerumani basi wazazi wake walikuwa wanazungumnza kijerurumani,.zamani,...hiyyo mifano tumeiona mingi,...hakuna maajabu ya dunia hapo ni ubongo tu,...na sehemu zake za kumbukumbu huwa hauasahau kitu,..
  computer huwa ina Recovery program,....mafaili hata uliyoyasahau utkiwanayo yanakuja,....
   
 10. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hii labda ni medium phenomena,watu wanaotumika kama simu kutoka kuzimu.
   
 11. upele

  upele JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna lolote kila kitu wao tu hivi why wao basi kuna jamaa mmoja nae alizimia ila alipo zinguka tu akataka pombe inakuwaje jamani,huyo alikuwa mjeru ila ni homa tu mbona wabongo wengi wanatamani sana language fulani ila hata azimie vipi akiamka kama kawa lugha ya madafu ile wao
  chanaga la macho
  conquest-utamu wa sukari tunaipenda ila ni homa
   
Loading...