Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lutayega, Jun 29, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,216
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 368"]
  [TR]
  [TD="width: 250"]

  Bibi Li Xiufeng baada ya kuzinduka toka kuzimu
  [/TD]
  [TD="width: 316"]Monday, March 12, 2012 1:09 AM
  Alitangazwa kuwa amefariki dunia, mwili wake uliwekwa kwenye jeneza, jeneza liliwekwa sehemu ya wazi ili watu waweze kuuaga mwili wake kwa siku sita watu waliendelea kuuaga mwili huo, siku ya sita watu walishangaa kukuta maiti haipo na bibi aliyekuwa kwenye jeneza alikutwa akiwa jikoni anapika.

  [/TD]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 491, bgcolor: transparent, colspan: 3"]Bibi mmoja wa nchini China amewashtua ndugu na majirani zake baada ya kutangazwa kuwa amefariki dunia na kupelekea maandalizi ya mazishi yake kufanyika lakini alizinduka na kurudi duniani siku ya sita akitoka ndani ya jeneza.

  Bibi Li Xiufeng mwenye umri wa miaka 95 aligunduliwa na majirani zake akiwa kitandani chumbani kwake akiwa hapumui na haonyeshi dalili yeyote ya kuwa hai.

  Tukio hilo lilitokea wiki mbili baada ya bibi Li kuteleza na kuanguka njiani na kupelekea kupata majeraha kichwani kwake.

  Baada ya majirani kumkuta chumbani kwake akiwa hapumui, walijaribu kumzindua lakini ilishindikana. Bi Li alikuwa hapumui na wala haonyeshi dalili yeyote ya uhai lakini mwili wake haukuwa wa baridi. Kwa fikira zao na majaribio machache waliyoyafanya, majirani walitangaza kuwa bibi Li amefariki dunia.

  Mwili wa bi Li ambaye alikuwa akiishi peke yake akipewa kampani na majirani, uliwekwa kwenye jeneza ndani ya nyumba yake na kwa kufuata taratibu za tamaduni za China, jeneza halifunikwa liliwachwa wazi juu ili kuwapa nafasi watu kuuaga mwili wa bi Li.

  Siku ya sita, majirani walipoenda kuuangalia mwili wa bi Li kabla ya kuuzika rasmi siku iliyofuatia, walishangazwa kukuta mwili haupo ndani ya jeneza.

  Msako mkali kijijini ulianza kuutafuta mwili wake na mazingira yanayoizunguka nyumba yake. Baada ya muda watu walishangazwa kumkuta bi Li akiwa jikoni anapika.

  "Nililala kwa muda mrefu sana, baada ya kuamka nilihisi njaa kali ikanibidi niingie jikoni kupika kitu cha kula", alisema bi Li alipohojiwa na majirani zake.

  Madaktari walisema kuwa kitaalamu bi Li alipatwa na "kifo cha bandia" 'artificial death', ambacho huelezewa kuwa mtu huwa hapumui lakini mwili wake huendelea kuwa wa moto.

  "Utamaduni wa kuhifadhi mwili ndani ya nyumba kwa siku kadhaa ndio uliookoa maisha ya bi Li, kama si utamaduni huo bi Li angekuwa ameishazikwa kweli zamani", alisema mmoja wa Madaktari waliomfanyia uchunguzi bi Li baada ya tukio hilo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. wehoodie

  wehoodie JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 784
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 80
  umesikia mara ngapi mtu yupo kwenye koma tanzania? Maana yake watu wengi tu huzikwa hai tz!
   
 3. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Duh.. bongo kuna watu hawalazi maiti.Na aliyepima hicho kifo aliangalia vigezo duni sana.Sijui kuwa wa baridi, sijui macho hayachezi, sijui moyo umesimama.
   
 4. roby2006

  roby2006 JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sio kosa lako
   
 5. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,995
  Likes Received: 1,566
  Trophy Points: 280
   
 6. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Jamaa yangu una agenda mbaya.Unapita kushambulia kila jina la Kikristu na kujaribu tumia Ukristu out of context.Na Biblia ipo right sana kuwa jamaa bado alichoma mkuki ili kuhakiki kuwa amekufa au hata kama hajafa basi lazima afe. Hili linapingana sana na theology uliyosoma kuwa hakufa.Sasa kazi kwako kuthibitishia uma alikwenda wapi?Na inabidi uje na maandiko ya Kihistoria au hata ya kidini yanayoonyesha kuwa hakufa na alikwenda wapi?Naomba usije na sababu ya kijinga kuwa wayahudi walisema kuwa hawakumuua.Kwani hata Biblia haijasema kuwa wao ndio walimuua,ila wao ndio walimshitaki kwa hila na uongo ili apate kufa, pia wakamweka kama sehemu ya zawadi ya pasaka iliyopaswa tolewa na mkuu wa wakoloni wao wa Kirumi.Myahudi aliyeshikwa akiua basi aliuwawa kikatili chini ya dola la Kirumi.
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nimecheka sana.Kwa hiyo bwana yesu alipata artificial death aise unaweza ukawa kweli
   
 10. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,995
  Likes Received: 1,566
  Trophy Points: 280
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Gavana hawa jamaa zetu hawaoni wala hawasikii, wanasoma lakini hawaelewi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. SIMBA mtoto

  SIMBA mtoto JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 208
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Toba !!!!! Tumswalieni mtume jamani.
   
 13. chuma cha reli

  chuma cha reli JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 1,794
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 280
  ....sio kila ki2 utakielewa kama ulishindwa kujua mwamedi ni mbakaji na jiwe la kaaba ni kipande cha nyota ambacho hata mbozi kipo na miaka flani kilipasuka mkakiuunga na madini ya shaba na kabla mwamedi hajatunga idea zaka kilikua kinatumika kwa ajiri ya ibada za kishetan za kabila yao huna sababu ya kuongea...u need to set ure mind free..hebu leo ruhusuni uko saudi arabia na nchi za kiarabu uhuru wa kuhabudu muaone matokeo...
   
 14. chuma cha reli

  chuma cha reli JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 1,794
  Likes Received: 579
  Trophy Points: 280
  ..wee ndo unaelewa....satanic verses
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe unaielewa Qur'an. Hakuna ubaya kwa hilo, ni vyema ukaisoma, inaeleweka bila kuwa na mfasiri.
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
   
 17. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,995
  Likes Received: 1,566
  Trophy Points: 280
  maneno yako haya ndiyo maneno ya bwana Yesu , ???? Jee maneno haya yalimfanya bwana yesu kufa???

  Ushahidi kutoka biblia Please


  Miguu yake haikuvunjwa na askari wa Kirumi: Yohana 19:32-33 "Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulubiwa pamoja naye.

  Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu.

  " Je, wewe unategemea madai ya askari hao kuwa Yesu alikuwa amekwishakufa, au walitaka kumwokoa kwa kuwa walikuwa wanaamini kuwa Yesu alikuwa hana kosa kabisa?

  Kama Yesu alifia msalabani, damu yake ingeganda na kwa hiyo kusingekuwa na damu ya kububujika kutoka mwilini mwake pale alipochomwa kitu cha ncha kali.

  Lakini Injili inaeleza kuwa damu na maji zilitoka: Yohana 19:34 "Lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu
  kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji."

  Mafarisayo walipomtaka Yesu athibitishe kazi yake ya kweli, alijibu: Matayo 12:40 "Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi."

  Bila kujali kipengele cha wakati, ambacho nacho hakikuwa michana mitatu na mausiku matatu bali ilikuwa ni mchana mmoja (Jumamosi, mchana tu) na mausiku mawili (usiku wa Ijumaa na wa jumamosi).

  Je, Yona alikuwa hai katika tumbo la nyangumi?

  Ni Ndiyo.

  Je, Yona aliendelea kuwa hai pale alipotemwa kutoka tumboni mwa nyangumi?

  Ni Ndiyo.

  Basi Yesu alikuwa bado yu hai, kama alivyotabiri
   
 18. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Kumbuka Yesu alijfananisha na Yona kwa kuwa ndani ya kitu na siku symbolically na si literally(ingekuwa literally basi naye pia ingebidi amezwe na huyo nyangumi).Kwanza Yona alimezwa na hivyo hakupata physical injuries ambazo zingeweza haribu sensitive organs.Ila Yesu alipigwa MKUKI na kilichotoka kinaonyesha kuwa kuwa aliumizwa kati ya ini ama bandama na utumbo mkubwa wenye maji.

  Yona angekumbwa na ukosefu wa hewa na kuanza sumbuliwa na digestive juices za huyo samaki.Ila inategemea huyo samaki alimeza nini tena kinachoweza kuwa more reactive/absoptive zaidi ya mwili wa Yona hivyo yona kuwa protected.Pia kuhusu Oxygen yona kam alizimia na kuwa ktk semi com auhitaji wa oxygen unakaribia zero au km si zero.Wapo watu wengi wameokolewa toka tumboni mwa chatu.Na wengi wao waliokolewa walipona kama chatu hakuwapiga meno ,na kuwapa backeria au virus.Ila wengi ngozi zao zilibanduka na kubaki kama wameungua kwa vile digestive juices zilishaanza washambulia.

  PIA SI SECURE SANA KWAKO KAMA MUUMINI WA UWEPO WA MUNGU MWEZA YOTE.KWANI KAMA MUNGU WAKO HAWEZI MORACLES KIDOGO KWA YONA,NA KWA YESU iweje Yesu afanye zaidi yake kwa kuokoa waliokwisha toa harufu?

  Umemezwa na propaganda kiasi huwezi angalia kitu kwa akili yako.Watu wengine pamoja na kuwa si wakufaulu sana,ila wanafeli mitihani kwa uzembe.Mfano teja anashindwa jibu madhara ya unga huku kila siku naowaona wenzie.Kuna ubishi mwingine waislam wanaendesha bila kuwa makini unawapeleka katika kufuru zaidi ya wema wanaoutafuta.
   
 19. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Warumi walikuwa na njia bora kwa kipindi kile za kutesa na ilikuwa ikiwaa furaha kama mchezo wakusisimua.Hawakuwa na haja ya kuvunja miguu ya mfu.Pia mari ya kiongozi wao haikuwa ya kuchezea kama unavyojaribu shawishi hapa.Na huna ushahidi kuwa hao askari hata kama walikuwa wakijua kuwa alikuwa hana hatia,bado wangeona sababu ya kumuokoa na si kuenjoy mauaji au hata kulinda uhai wao mbele ya kaisari.Pia unasahau wayahudi walikuwa na akili sana ndio maana waiweka taadhari.

  SO muwe mnasoam mistari n akuilewa huku mkiwa na reference nyingi.

  Acheni uongo nyie damu ina mazingira ya kuganda.Damu zipo hadi katika nyama za wanyama zilizotundikwa masaa kibao zikiwa exposed ktk hewa, ndio Yesu aliyekuwa chini ya masaa 3?Na ushahidi ni aliwahishwa kuzikwa mapema kabla ya sabato kwa taratibu za kiyahudi.

  Kutoa bandama au ini ni sehemu za mwili ambazo zenyewe tuu ni kama damu na zina damu nyingi,maji yapo ktk utumbo.Pia mjue kuwa alipewa siki alipoomba maji nayo pia inachange behavaious ya damu.
  unaelewaje 3(day+night)? na hii 3days and 3nights, na hii 1day+3nights?
  Kumbuka Yesu alijfananisha na Yona kwa kuwa ndani ya kitu na siku symbolically na si literally(ingekuwa literally basi naye pia ingebidi amezwe na huyo nyangumi).Kwanza Yona alimezwa na hivyo hakupata physical injuries ambazo zingeweza haribu sensitive organs.Ila Yesu alipigwa MKUKI na kilichotoka kinaonyesha kuwa kuwa aliumizwa kati ya ini ama bandama na utumbo mkubwa wenye maji.

  Yona angekumbwa na ukosefu wa hewa na kuanza sumbuliwa na digestive juices za huyo samaki.Ila inategemea huyo samaki alimeza nini tena kinachoweza kuwa more reactive/absoptive zaidi ya mwili wa Yona hivyo yona kuwa protected.Pia kuhusu Oxygen yona kam alizimia na kuwa ktk semi com auhitaji wa oxygen unakaribia zero au km si zero.Wapo watu wengi wameokolewa toka tumboni mwa chatu.Na wengi wao waliokolewa walipona kama chatu hakuwapiga meno ,na kuwapa backeria au virus.Ila wengi ngozi zao zilibanduka na kubaki kama wameungua kwa vile digestive juices zilishaanza washambulia.

  PIA SI SECURE SANA KWAKO KAMA MUUMINI WA UWEPO WA MUNGU MWEZA YOTE.KWANI KAMA MUNGU WAKO HAWEZI MORACLES KIDOGO KWA YONA,NA KWA YESU iweje Yesu afanye zaidi yake kwa kufufua waliokwisha toa harufu?Mnajikata mkia mkidhani mnakata wa mwingine

  Umemezwa na propaganda kiasi huwezi angalia kitu kwa akili yako.Watu wengine pamoja na kuwa si wakufaulu sana,ila wanafeli mitihani kwa uzembe.Mfano teja anashindwa jibu madhara ya unga huku kila siku naowaona wenzie.Kuna ubishi mwingine waislam wanaendesha bila kuwa makini unawapeleka katika kufuru zaidi ya wema wanaoutafuta.
   
 20. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  unajua nilikuwa nashangaa imekuweje tukatoka katika mada husika tukainga katika personal attacks.Kumbe ni udini wa watu humu ndani.Kila waongeacho watu wao wanawahi fananisha na dini huku wakiwa na mtazamo mbaya kuhusu dini yao wenyewe.Sasa kama nyie mnazika faster si mahlai pa kujifunza hapa?Na coincidences pia inabidi mhusika atumie busara.


  Sasa kama by coincidende nilikuwa naangalia mpira mpira ghafa messi akafunga goli nikashangilia halafu bahati mbaya na wewe ukajamba huku ukiwa na mwenzi wako.kwanini uanze nionyesha nisichokiona,ungepaswa subiri ili ujue kama nilikuwa nacheka hicho au lah.Then ndio utake ujue nimekuoaje au kusikiaje?Kwa chabo au wewe ulizidisha misifa.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...