Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Mar 12, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  <tbody>[TR]
  [TD="colspan: 3"]Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  Bibi Li Xiufeng baada ya kuzinduka toka kuzimu[/TD]
  [TD]
  Alitangazwa kuwa amefariki dunia, mwili wake uliwekwa kwenye jeneza, jeneza liliwekwa sehemu ya wazi ili watu waweze kuuaga mwili wake kwa siku sita watu waliendelea kuuaga mwili huo, siku ya sita watu walishangaa kukuta maiti haipo na bibi aliyekuwa kwenye jeneza alikutwa akiwa jikoni anapika.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Bibi mmoja wa nchini China amewashtua ndugu na majirani zake baada ya kutangazwa kuwa amefariki dunia na kupelekea maandalizi ya mazishi yake kufanyika lakini alizinduka na kurudi duniani siku ya sita akitoka ndani ya jeneza.

  Bibi Li Xiufeng mwenye umri wa miaka 95 aligunduliwa na majirani zake akiwa kitandani chumbani kwake akiwa hapumui na haonyeshi dalili yeyote ya kuwa hai.

  Tukio hilo lilitokea wiki mbili baada ya bibi Li kuteleza na kuanguka njiani na kupelekea kupata majeraha kichwani kwake.

  Baada ya majirani kumkuta chumbani kwake akiwa hapumui, walijaribu kumzindua lakini ilishindikana. Bi Li alikuwa hapumui na wala haonyeshi dalili yeyote ya uhai lakini mwili wake haukuwa wa baridi. Kwa fikira zao na majaribio machache waliyoyafanya, majirani walitangaza kuwa bibi Li amefariki dunia.

  Mwili wa bi Li ambaye alikuwa akiishi peke yake akipewa kampani na majirani, uliwekwa kwenye jeneza ndani ya nyumba yake na kwa kufuata taratibu za tamaduni za China, jeneza halifunikwa liliwachwa wazi juu ili kuwapa nafasi watu kuuaga mwili wa bi Li.

  Siku ya sita, majirani walipoenda kuuangalia mwili wa bi Li kabla ya kuuzika rasmi siku iliyofuatia, walishangazwa kukuta mwili haupo ndani ya jeneza.

  Msako mkali kijijini ulianza kuutafuta mwili wake na mazingira yanayoizunguka nyumba yake. Baada ya muda watu walishangazwa kumkuta bi Li akiwa jikoni anapika.

  "Nililala kwa muda mrefu sana, baada ya kuamka nilihisi njaa kali ikanibidi niingie jikoni kupika kitu cha kula", alisema bi Li alipohojiwa na majirani zake.

  Madaktari walisema kuwa kitaalamu bi Li alipatwa na "kifo cha bandia" 'artificial death', ambacho huelezewa kuwa mtu huwa hapumui lakini mwili wake huendelea kuwa wa moto.

  "Utamaduni wa kuhifadhi mwili ndani ya nyumba kwa siku kadhaa ndio uliookoa maisha ya bi Li, kama si utamaduni huo bi Li angekuwa ameishazikwa kweli zamani", alisema mmoja wa Madaktari waliomfanyia uchunguzi bi Li baada ya tukio hilo.

  [/TD]
  [/TR]
  </tbody>[/TABLE]
  chanzo. Azinduka Toka Kwenye Jeneza Siku Sita Baada ya Kufariki
   
 2. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kinawezekana China...
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  China mwisho wa Dunia Mkuu umebadilisha picha yako? Nimeipenda picha mpya mwahhhhhhhhhhh
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  sipati picha angekuwa tz yani tumesha msahau
   
 5. Mchochezi

  Mchochezi JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 6,953
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  ingekuwa tz watu wangekuwa wanazungumzia habari za msukule
   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mzizi walimuona hana nyama wakaamua wamrudishe
   
 7. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,485
  Likes Received: 4,757
  Trophy Points: 280
  Hayo ni majaribio tu wakifuzu wanakuja Bongo, na huku watatumia mizizi mikavu tu!!!
   
 8. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Alikuwa hajafafa huyo
   
 9. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hili dili angelipata TB Joshua!
   
Loading...