Azimio la Mwanza lililotolewa leo . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimio la Mwanza lililotolewa leo .

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Dec 5, 2008.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  AZIMIO LA MWANZA
  Sisi wananchi wa mkoa wa Mwanza tuliokutana hapa jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa Chama cha CHADEMA leo tarehe 5 Disemba 2008, na baada ya kupata taarifa ya ziara ya Operesheni Sangara ya viongozi wa CHADEMA kutoka katika majimbo manane ya Mkoa wa Mwanza, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma Ndugu Kabwe Zuberi Zitto (Mb), tunapenda kuazimia yafuatayo;
  TUNASIKITISHWA sana na kiwango cha Ufisadi katika Taifa letu na hivyo kulifanya taifa kupoteza rasilimali fedha nyingi ambazo zingeweza kusaidia maendeleo ya wananchi na kutuondoa katika dimbwi la umasikini; Ufisadi ambao sasa umeanza kuleta nyufa katika misingi ya uhai wa taifa letu;
  KWA KUTAJA tu baadhi ya mabilioni ya shilingi ambayo yamefujwa kutokana na wizi, ufisadi, mikataba mibovu na ubadhirifu wa rasilimali fedha za Watanzania ni pamoja na;
  - Akaunti ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania 133bn
  - Kampuni ya Meremeta na Tangold 155bn
  - Kampuni ya Deep Green 10bn
  - Mapato ya kikodi kutoka makampuni ya Madini kwa miaka 10
  (15% allowance clause kutoka sheria ya kodi ya mapato ya
  mwaka 2004 baada ya marekebisho ya sheria ya fedha 1997) 883bn
  - Misamaha ya kodi ya mafuta kwa makampuni ya Madini
  kuanzia 2005 170bn
  - Mkataba wa IPTL (3bn kwa mwezi) 168bn
  - Mkataba wa Richmond (wabunge na vyombo
  vya habari viliokoa) 172bn
  TUNATAMBUA hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa kutokana na baadhi ya tuhuma ambazo tumezitaja hapo juu kwa baadhi ya wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa kufikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa mujibu wa sheria; Hata hivyo tunahisi na tunasisitiza kuwa hatua hizi haziwezi kumaliza tatizo la rushwa kubwa hapa nchini ama ufisadi kwani hatua za aina hii zimewahi kuchukuliwa huko nyuma na zinawaacha watuhumiwa wengi ambao wana makosa ya aina hiyo hiyo kwa kutokana tu na misingi ya kisheria na kikatiba;
  Kwa mfano, TUNAKUMBUSHA kuwa katika kipindi cha utawala wa Rais Benjamin Mkapa, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Katibu Mkuu wake wakati wa utawala wa Rais Mwinyi (Nalaila Kiula na Dkt. Mlingwa) walifikishwa mahakamani kwa kosa la rushwa wakiwa viongozi wa umma na hatimae wote walisafishwa kimahakama. Hii ni dhahiri kwamba hata kesi za sasa zinaweza kuishia katika mazingira ya aina hiyo hiyo. Aidha ikumbukwe kuwa baada ya hatua hiyo, vitendo vya rushwa na ufisadi viliendelea kukithiri katika utawala wa Rais Mkapa. Kwa hiyo hofu yetu ni kuwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa zinaelekea kuisafisha tu serikali na sio kuvunja misingi ya ufisadi ndani ya mfumo wa utawala wa nchi yetu;
  TUNATAKA Taifa letu lirudi kwenye misingi ya umoja, haki, usawa mbele ya sheria na mshikamano wa kitaifa. Ufisadi umeanza kubomoa kabisa misingi imara ya Taifa letu. Hivyo, hatua madhubuti zapaswa kuchukuliwa kuhusu ufisadi ili kumaliza kabisa mianya ya ufisadi wa kimfumo ulioshamiri (Institutional corruption);
  TUNAJUA kuwa, kwa mfano, katika ufisadi uliofanyika katika akaunti ya madeni ya Nje (EPA) Benki Kuu ya Tanzania, kampuni moja ya KAGODA AGRICULTURAL LIMITED ilichota takribani 40bn wakati wa kampeni za uchaguzi na tunaamini kuwa fedha hizo zilitumiwa na Chama Cha Mapinduzi kufanyia kampeni zake na kufanikiwa kushinda Urais, Wabunge na Madiwani kwa kishindo. Ndio maana serikali imepata kigugumizi kutaja wamiliki wa kampuni ya KAGODA. Vilevile misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ilitolewa katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kwa hiyo tuna mashaka kuwa makampuni haya yaliisaidia CCM; Hivyo hivyo kwa fedha kupitia kampuni ya Deep Green.
  Kwa hiyo TUNASISITIZA kuwa serikali ambayo imeingia madarakani kwa kutumia fedha za kifisadi kamwe haiwezi kusafisha ufisadi; Vilevile chama kilichochukuwa utawala kwa kutumia fedha za ufisadi hakiwezi kudhibiti serikali yake wala kuunda serikali ambayo haitokani na ufisadi.
  Hivyo basi, tunatoa matamko yafuatayo;
  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete atangaze kipindi cha mpito (transition period), aivunje serikali yake na kuunda utawala wa mpito ambao utawezesha kuanza kwa mchakato wa kujenga misingi mipya na ya mwafaka wa kitaifa kwa masuala yafuatayo;
  - Mfumo na muundo wa Muungano,
  - nafasi ya dini katika mfumo wa utawala,
  - Misingi imara ya kusimamia masuala ya kijamii kama haki ya kupata elimu, huduma za afya nk.
  - Kuainisha tunu za Taifa ambazo zitaongoza mienendo ya uongozi wa nchi, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla.
  2. Kuandika Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo mbali na matakwa ya tamko namba 1 hapo juu itaweka misingi ya utawala wa maadili ya Taifa na Utaifa, mfumo wa uchaguzi na kuweka sheria mpya ya uchaguzi itakayokidhi misingi ya demokrasia ya vyama vingi na itakayodhibiti matumizi ya fedha katika kampeni.
  3. Iundwe mahakama maalumu (Special Tribunal) kwa sheria ya Bunge itakayofanya kazi ya kupitia masuala yote ya rushwa kubwa kubwa zinazotajwa na zisizotajwa, itakayotoa nafasi kujua ukweli mtupu kuhusu ufisadi na kujenga maridhiano ya Taifa.
  4. Mapendekezo ya Taarifa ya Bomani kuhusu sekta ya madini itekelezwe mara moja ili taifa lianze kunufaika na rasilimali zake za Madini.
  TUNAOMBA watanzania wa mikoa mingine yote watuunge mkono katika maudhui ya Azimio hili ambalo sisi wananchi wa Mwanza tunaona linaweza kuliokoa Taifa letu na kulirejesha katika misingi ya uanzishwaji wake na waasisi wetu;

  AZIMIO hili la MWANZA limefikiwa leo tarehe 5 Disemba 2008 katika viwanja vya SAHARA hapa jijini Mwanza.
   
 2. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Azimio hili limesomwa na mzee Sylivester Kanyansi Masinde kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa leo jioni.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Chadema you are still cruising kwenye kanda hiyo ? Safi sana lakini naomba kujua mipango yenu ya kunyakua Jimbo la kule wapi huku Mbeya.Watu wa Mbeya wanaweza kuwa kama Tarime ?Hebu longeni nisikie
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu mie nilidhani na wewe "umeenda" kwenye operesheni Sangara. How comes u missed out on this one ngosha?
   
Loading...