Azimio la Msasani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Azimio la Msasani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Jul 28, 2008.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Jul 28, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wakulu hivi ni kweli Mwalimu aliwaita G55 pale nyumbani kwake Msasani na kuwaasa wajitoe CCM Nambari Wani ili waunde CCM Nambari Mbili itakayoleta upinzani wa kweli Tanzania? Na je ni kweli Mzee wa Butiama alijitoa kwa muda katika CCM A na alikuwa tayari kujiunga na CCM B ndio maana akasema CCM sio mama yake? Kama haya yote ni kweli ina maana huu mpasuko ndani ya CCM MTANDAO ndio utekelezaji wa Azimio la Msasani?
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Be specific please....
   
 3. C

  Chuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  udaku.....ihamishie ktk udaku au maswali...
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Jul 28, 2008
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Katika medani ya siasa sio kila kitu kiko wazi kwa mwananchi wa kawaida, hivyo ni kazi ya wakulu na wachambuzi kutufungua macho. Hili suala la Azimio la Msasani ni suala tete na nyeti sana ambalo inabidi tuliangalie kwa undani kama tunataka kuelewa hali halisi ya chama tawala. Ndio suala pekee lililomliza Mwalimu mbele ya kadamnasi. Ngoja nimnukuu Mwalimu mwenyewe kutoka katika ukurasa wa 20 wa kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania:

  "Sina kawaida ya kulizwa na mambo ya siasa, lakini katika kikao hicho nilishindwa kujizuia kulia. Sikupata maelezo ya maana ya kuwafanya watu wazima wafanye walivyofanya. Nilipouliza kwa nini hawakupinga hoja ya Serikali Tatu, kama tulivyokuwa tumekubaliana, majibu ya Viongozi wetu Wakuu yalikuwa ni ya ajabu kabisa. Ati Wabunge wenye hoja, baada ya kuonana nami Msasani, walikwenda bungeni wakiwa wakali kama mbogo"

  Sasa hapa inabidi tujiulize waliteta nini Msasani kilichowapa ujasiri wa ajabu wabunge hawa wa G55 wageuke nyati bungeni? Iweje Mwalimu ambaye alikuwa anapingana kabisa na hoja yao ya Utanganyika awaite chemba pale Msasani na awape ujasiri huu wa ajabu katika enzi za zidumu fikra sahihi za mwenyeketi wa zamani wa chama na zama za chama kuendelea tu kushika hatamu hata wakati wa mageuzi? Na iweje baada ya tukio hilo Mwalimu asisitize sana katika kitabu chake cha Tanzania!Tanzania! kuwa sera ya Utanganyika sio sera ya chama tawala na kuwa wanaounga mkono sera hiyo watoke waanzishe chama chao? Kama muasisi mwenyewe wa chama tawala alisema upinzani wa kweli utatoka CCM nini kinawazuia G55 wa leo wenye hoja za msingi dhidi ya Richmond, Kiwira na EPA wasijitoe katika mitandao ya chama tawala na kuanzisha chama kitakacholeta upinzani wa kweli?
   
 5. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu hapa. Mwalimu alikuwa akiongelea CCM A akiwa na maana iliyokuwepo ambayo imeasi misingi ya chama hicho na CCM ambayo itaweza kurudisha misingi hiyo ama vice versa.

  Sasa huu ujinga unaoendela sasa wala hauna uhusiano wa kimisingi wala kifalsafa...Ni POWER STRUGGLE and POLITICAL SURVIVAL per se....nothing more. Hakuna cha maana kitakachotokea hapo endapo watafukuzana hawa ukitilia maanani kuwa hata upande wa pili bado HAWAJATULIA.....

  CCM B aliyodhania mwalimu haitatoka kwa hawa wazee....

  Tanzanianjema
   
Loading...