Azimio la kikao cha CCM Juu ya Watumishi Serikalini

-Kinaaza mchakato wakuteua kila idara/units ya serikali popote tanzania mtu mmoja ambaye wenye mapenzi kweli ya chama chao
-majukumu yake nikufatili watumishi wote wanaopinga chama hicho au kuwa wanachama wa upinza kisha kuwashusha vyeo au kuwaamishia sehemu mbaya plus polini zaidi au kuwaulimboka....na n.k

kwani wametumia kila mbinu zinakwama... je kwani hivi jamani chama cha mzee wangu....???????
nawasilisha!

SOURCE: Mjumbe wa maazimio hayo.

Tuashuwashukuri nyie mnaolikisha habari za namna hii, endele kusaidia ukombozi. Wamepagawa kila wanaposoma taarifa za usalama wa taifa-hali ya siasa wapagawa
 
Hawa wanatumia propaganda kaka, hebu weka sawa hoja kaka Nnauye Jr, wanatupima. Nadhani ukweli ni kuwa CCM ndio mama wa propaganda, na tunajulikana kwa hili, tukiamua hapa, itakuwa kilio tu. Hebu tulia uwashushie hoja kwa kifupi tu, hakuna haja ya ku upuuzia upuuzi. Mfano, Chama cha CCM kina nia njema na watu wake, dhamana ya kuongoza si ya kuwaongoza wana CCM peke yao, bali ni ya watu wote pamoja na wale wenye itikadi tofauti na ya CCM ya "UJAMAA NA KUJITEGEMEA" (ambayo itikadi ya vyama vingine sijaijua vema ni ipi, ninajua propaganda za msimu tu). Tunawataka maafisa na viongozi wa Serikali tunaowaamini wafanye kazi zao kwa bidii bila kujali hoja hizi na uvumi huu unaoenezwa, kwakuwa serikali haikuwaingiza kazini kutokana na itikzadi zenu, ila ni kwa elimu na uwezo wenu wa kazi ambao CCM inauthamini sana. Si vema leo hii watu waliotuamini kutupa dhamana tukaanza kuwabagua kwakuwa tunaamini kuwa, sisi sote ni ndugu, na nchi hii ni yetu sote pamoja, hata kama tuna mawazo tofauti hayo yote ni katika kutafakari jinsi ya kuipeleka nchi hii mbali. Mungu Ibariki Tanzania Mungu Wabariki Watu wa Tanzania kwa itikadi zao Tofauti. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

Profesa, hivi bado CCM inatekeleza siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA? Hivi bado vijiji wa ujamaa vipo? Na vile viwanda vya kijamaa alivyoanzisha Mwalimu Nyerere bado vinamilikiwa na umma? Juzi nilipita pale kawe(Tanganyika Packers) palipokuwa na kiwanda cha kusindika nyama za ng'ombe toka NARCO(National Ranching Company) nikakuta siku hizi kuna kanisa la walokole. Hivi kile kiwanda bado kinaendeshwa na serikali ya CCM kwa njia ya kijamaa?
 
Ama kweli wahenga walisema: Wimbo MZURI hutoa nyoka pangoni.

Ni kweli usemi huu miaka yote huwa naufahamu, lakini kimsingi haukua matarajio yangu wala sikutegemea joka lenyewe lijitokeze ki-urahisi kiasi hiki. PROFESA, kumbe wewe humu Jukwaani huwa ni wetu????

Haya basi, kwa mpigo; kidumu chama cha mapinduzi.
Uwezo Tunao, bado sijashawishika kuamini chama kingine, ki-katiba, kimfumo, na kiitikadi, ila nateswa sana na tabia za viongozi wangu, hayo maumivu ni makubwa. Ila kuondoka CCM sio dawa, dawa ni kushiriki katika maboresho ya kweli, bila kuwa na hila, fitina, majungu, ubinafsi, upendeleo, wala chuki na mtu mwenye mawazo tofauti na chama cha CCM ninachokiamini. Hata ikichukua muda, bado tukiwa na imani, kwa pamoja tunaweza kufanikiwa. Vyama vingine vinapata wafuasi wengi kwasababu ya udhaifu wa viongozi wetu na si Chama cha Mapinduzi, la hasha. Wanatafuta matumaini yalipo, "wanajaribu". Ni tabia tu ziliingizwa katika chama na tulipokuja kujua tayari zinatugharimu, ila zitapita, kwanza wahusuika wenyewe ndio haooo wanazeeka, na natumaini vijana kama akina Nnauye Jr hawataiga mabaya, bali mazuri tu. Sasa kama unaamini haya, wewe nmi mwenzangu, ila kama unaamini kuwa mwenzako kama mwana CCM tu bila kuweka vigezo inaweza kuwa tabu kidogo. Maana ndani ya CCM wako wa aina nyingi tu, issemi huko kwenye vyama vingine hawamo, ila CCM kama chama kiongozi, ni rahisi kuonekana kwakuwa watu wengi wana matumaini makubwa na matarajio mengi, kama Chama Kiongozi lazima kiwe mfano mzuri, ndio mizania ya vyama vingine, so ubaya wa sasa unatokana na kutu ya mizania yenyewe, hebu tuungane kuweka mambo sawa, bila kelele. Washuhudie tu. Wakisema, na kutusema, tujibu kwa hoja na kuhakikisha hekima na busara mbele na kutenda yale mazuri tunayoyasema.
 
Profesa, hivi bado CCM inatekeleza siasa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA? Hivi bado vijiji wa ujamaa vipo? Na vile viwanda vya kijamaa alivyoanzisha Mwalimu Nyerere bado vinamilikiwa na umma? Juzi nilipita pale kawe(Tanganyika Packers) palipokuwa na kiwanda cha kusindika nyama za ng'ombe toka NARCO(National Ranching Company) nikakuta siku hizi kuna kanisa la walokole. Hivi kile kiwanda bado kinaendeshwa na serikali ya CCM kwa njia ya kijamaa?
tubadilike-sasa ukiangalia makala yangu niliyomjibu Uwezo Tunao hapo, utaona msimamo wangu. Kwa chama chochote kile cha siasa, hata vyama vingine vya hiyari, kuwepo kwwa Katiba na Muongozo ni jambo moja kulitekeleza ni jambo lingine. Katiba ya CCM ni nzuri sana kwa kweli (siemi nyingine ni mbaya), ila ninamashaka makubwa mno na utekelezaji wake. Kuna mambo mengi kwa makusudi waliopewa dhamana ya kukoongoza chama wameyapotosha ili kujinufaisha wao na kujipatia mali kwa haraka bila kujuali wengine. Hili ndilo Tatizo kubwa. Je wajua kuwa nchi kama Sweden walijifunza kutoka kwetu na kuiga na kutekeleza sera za ujamaa na kujitegemea? Unafahamu kuhusu uchumi wa nchi hii ya Sweden? Haya tutayaongea siku nyingine. Nchi nyingi tu Venezuela, Rwanda nk wamejifunza mengi kutoka katika mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea (Kujitegemea Kiuchumi, Kisiasa na Kiutamaduni).

Hebu angalia mwenyewe, achilia mbali itikadi ya mtu, mana ni vema kussoma hivi vitu ukikosoa hoja yako inakuwa nzito kwa kuwa na ushahidi tosha: http://www.ccm.or.tz/images/upload/katiba.pdf
 
Kweli chadema mko taabani mmeanzisha majungu mengine kama kawaida yenu manake nyie chadema ndiyo washawishi wa migomo na maandamano yote hapa nchini mnataka muigombanishe serikali ya CCM na watumishi wake,katika hilo mmefeli watanzania wanawajua sasa hivi acheni majungu nendeni mkamjulie hali mbunge wenu aliyepata ajali Mh Selasini mnamtenga kwa sababu ni msema kweli anakosoa maovu na madudu ya viongozi wa chadema basi mnamtenga,chadema haifahi kupewa madaraka ata kidogo kama leo tu mnamajungu kiasi hicho je mkipewa madaraka?chadema ni chama cha kidini,undugu na ukabila hawafahi ata kidogo watavuruga Amani ,Umoja na Mshikamano wetu watanzania!
 
Huu ni upuuzi mwingine unaothibitisha ni jinsi gani watani wako taabani na kifo chao hakiepukiki!

Hakuna upuuzi hapa, Ni ukweli usiopingika kuwa wakuu wengi wa idara ktk taasisi za serikali ni makada wa CCM. Mtumishi asiye-mwanachama wa chama cha mapinduzi hata kama ni mchapakazi hawezi pewa ukuu wa idara. Wakati wa uchaguzi mkuu CCM ruksa kufanya siasa maeneo ya kazi; vyama vingine vinatakiwa kufuata sheria ya kutofanya siasa ktk maeneo hayo.

Ole wenu mpindishao sheria kwa maslahi yenu binafsi
 
Victims wengi zaidi watatokea Arusha Arusha MBeya Moshi Iringa Kilomanjaro Mara Bukoba etc.
Waharakishe mpango huo ili nimfahamu mtu ofisini kwangu ambaye anaweza kuwa ccm hadi miaka hii!

Watu wengi wana kadi za chama twawala lakini imani na mapenzi yao yapo upinzani; sijui watachambuaje mchele na pumba...Most of wenye ofisi kubwa wana vyeti vya ndoa (makaratasi) lakini mapenzi yako zaidi nyumba ndogo....Hata siku moja visible things (i.e kadi) hazijawahi kuwa superior to invisible things (i.e mapenzi, akili etc)...

Uwiiiii sijui kwanini hawa watu wanashindwa kuelewa kamba wanazotengeneza kunyonga wengine zitawanyonga wenyewe. Atleast preacher nimekuwa kama sauti nyikani lakini yaonekana wana macho yasiyo ona, hisia zisizo hisi, masikio yasiosikia na wako mbio kuelekea shimoni.....Haya we waandaeni simba wawe na njaa kali ili wamtafune 'Daniel' tuone kati ya huyo na ninyi wafitini nani atakuwa mboga ya hao simba!
 
siku hizi kazi za kuineza cdm tunazifanya kama za kitume,ikiwezekana hata kwa gharama zetu.acha watupeleke huko maporini tukamwage sumu ili kifo cha nyinyiem kiwe mapema haraka iwezekanavyo.pipooooooooooooozz

Wewe ni mmojawapo katika wale vijana waliowekwa pale makao makuu ya chadema kazi yao ni kuichafua CCM na serikali yake ili wananchi waone hawafahi kuwa madarakani waichague chadema uchaguzi ujao,vijana hawa wanapewa posho kwa kazi hiyo chafu ya kuichafua CCM na serikali yake ,Ewe mtanzania mzalendo popote ulipo hawa chadema ndiyo wachochezi wa migomo,maandamano na fujo zote hapa nchini hivi sasa wanachochea mgomo wa madaktari na sasa wanataka kuichonganisha serikali na watumishi wa umma kama uonazo jumbe zao kataa chadema hawafahi ata kidogo kuongoza taifa hili ni wabaguzi,wadini,undugu na ubinafsi umewajaa ,waroho wa madaraka ndiyo maana wanashawishi fujo ili nchi isitawalike waonekane wao bora,kataa chadema kwa nguvu zako zote hapo ulipo elimisha jamii iliyokuzunguka kuwa chadema hawafahi kupewa madaraka ya kuongoza taifa hili ili kulinda Amani,Umoja na Mshikamano wa watanzania!
 
Hakuna upuuzi hapa, Ni ukweli usiopingika kuwa wakuu wengi wa idara ktk taasisi za serikali ni makada wa CCM. Mtumishi asiye-mwanachama wa chama cha mapinduzi hata kama ni mchapakazi hawezi pewa ukuu wa idara. Wakati wa uchaguzi mkuu CCM ruksa kufanya siasa maeneo ya kazi; vyama vingine vinatakiwa kufuata sheria ya kutofanya siasa ktk maeneo hayo.

Ole wenu mpindishao sheria kwa maslahi yenu binafsi

Kinacho sikitisha zaidi hao ambao wanaonekana wanamapenzi sana huwa mara nyingi hayo mapenzi hayamo mioyoni mwao ila maslahi binafsi ndiyo yamejaza vyumba vya mioyo yao. Kwakua wengi wako kimaslahi basi pale ambapo maslahi yao yanakuwa hatarini hawakawii kumwaga mboga ili kutishia nyau wahusika bila kujali maslahi mapana ya nchi na raia wake.

Time has come and now is of the manifestation of the true sons of Tanzania! I am prety sure that the whole creation has been groaning as in the pains of childbirth right up to the present time and has been awaiting for the manifestation of these servants of the most high. For the creation was subjected to frustration, not by its own choice, but by the will of the one who subjected it, in hope! Gwajima kanena; Rose Mhando kaimba; Ame kaweka muhuri kabisaaaa kwakuwa anajua amebeba ufalme mabegani mwake. The best is yet to come kwa maana injili/habari njema tuihubiriyo siyo kwa maneno ya ufundi wa kibinadamu bali yenye nguvu na yenye kuleta matokeo! Ufisadi na kabila lake lote karibu linafika katikati ya bahari ili tuyaruhusu maji yarudiye hali yake ya kwanza nasi tuanze safari ya kuiteka caana! Kwa jina la Yesu tunavunja..tuna bomoa...lazima tushindeeeeee!
 
Watu wengi wana kadi za chama twawala lakini imani na mapenzi yao yapo upinzani; sijui watachambuaje mchele na pumba...Most of wenye ofisi kubwa wana vyeti vya ndoa (makaratasi) lakini mapenzi yako zaidi nyumba ndogo....Hata siku moja visible things (i.e kadi) hazijawahi kuwa superior to invisible things (i.e mapenzi, akili etc)...

Uwiiiii sijui kwanini hawa watu wanashindwa kuelewa kamba wanazotengeneza kunyonga wengine zitawanyonga wenyewe. Atleast preacher nimekuwa kama sauti nyikani lakini yaonekana wana macho yasiyo ona, hisia zisizo hisi, masikio yasiosikia na wako mbio kuelekea shimoni.....Haya we waandaeni simba wawe na njaa kali ili wamtafune 'Daniel' tuone kati ya huyo na ninyi wafitini nani atakuwa mboga ya hao simba!

wewe ni kijana wa chadema unapewa posho na chama chako cha kibaguzi ili kuisema vibaya CCM na serikali yake ndiyo nyie washawishi wa migomo yote na wachochezi wa fujo zote hapa nchini leo ngugu xetu wengi wanapata tabu mahospitalini na wengine kufariki kwa sababu ya chadema kuwachochea madaktari kugoma,kataa chadema ili kulinda Umoja wetu, na Mshikamano wa watanzania!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kweli chadema mko taabani mmeanzisha majungu mengine kama kawaida yenu manake nyie chadema ndiyo washawishi wa migomo na maandamano yote hapa nchini mnataka muigombanishe serikali ya CCM na watumishi wake,katika hilo mmefeli watanzania wanawajua sasa hivi acheni majungu nendeni mkamjulie hali mbunge wenu aliyepata ajali Mh Selasini mnamtenga kwa sababu ni msema kweli anakosoa maovu na madudu ya viongozi wa chadema basi mnamtenga,chadema haifahi kupewa madaraka ata kidogo kama leo tu mnamajungu kiasi hicho je mkipewa madaraka?chadema ni chama cha kidini,undugu na ukabila hawafahi ata kidogo watavuruga Amani ,Umoja na Mshikamano wetu watanzania!

mwigulu acha izo banaa!
 
Nape, vipi kuhusu hatima ya wale Magamba 3 na wafuasi wao? Maana kumbukumbu zinaonesha wewe ndio ulikuwa uko mstari wa mbele kuwashighulikia. Kuna maendeleo yoyote kuhusu hatima yao?

Hatima hana manake Magamba matatu hayo yamekiua chama na wali wa hitima tayari umeshaliwa na M4C.
 
A: Mnamkataa shetatani?
Wote: Namkataa
A: Na mambo yake yote?
Wote: Namkataa
A: Na fahari zake zote?
Wote: Nazikataa
 
Wakitumia njio hiyo inabidi sisi tutumie Peoples Power ndio itakuwa dawa yao nguvu ya uma haishindwi
 
wafanyakazi wengi wako mijini na familia zao katika chaguzi za mwisho vyama vya upinzani ndivyo vilivyopata kura nyingi ktk chaguzi hizo
 
Huu ni upuuzi mwingine unaothibitisha ni jinsi gani watani wako taabani na kifo chao hakiepukiki!
Wewe mtu ni taahira!!! Si ulikwishabatizwa kwa jina la "kansa ndani ya ccm"?? Sasa unajipendekeza nini tena??? Hebu tuambie ile kasi yako ya kuwavua magamba wezi wenzako iliishia wapi!!!?

Utaratibu huo ulikuwepo miaka ya nyuma na hata makada hawa kufikia kufilisi mashirika mengi ya umma. Utaratibu huu ulikufa naturala death 1991 baada ya vyombo vya juu vya CCM kupitisha azimio la Zenji ambapo wajumbe wa vikoa hivyo walirejea kimya kimya na kuanza kutumia vyeo vyo kuhamishia raslimali za taifa katika miliki zao binafsi. Kilele cha ufisadi huu ni kujibinafsishia nyumba za serikali. Kuona hivyo watendaji wa serikali ambapo weni ndio huwapatia wananchi huduma muhimu kama vile amaji, afya, elimu n.k nao wakajiunga na wananasiasa kutafuna raslimali za nchi na hivyo kuwaacha wananchi bila ya huduma. Ni wazi kutokana na ulafi unaoendela hivi sasa hapa nchini watajitikeza watu wenye malengo ya kujinufaisha kujifanya wakereketwa wa CCM kama vile Wassira na taarifa zote atakazopeleka zitakuw za uongo na mpango mzima hautafanikiwa.
 
Back
Top Bottom