Azimio la Hoteli Lakairo (Mwanza) na Dira ya Mpya ya Walalahoi Kuchagua Viongozi 2015

Uwezo Tunao

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
6,942
1,187
Wenye nyumba hamjambo???

Mwenzenu mie ndo kwanza nawasili hapa Ubungo nikitokea zangu Ku-Mafinga. Kwenu nimeleta salaam na ujumbe toka Jimboni kwangu Kinyanambo C Mkoani Iringa.

Basi letu la Matema Bichi ilichelewa kidogo pale Chalinze. WenSenu kule wameniagiza kuja hapa katika walichokiita 'Bunge la Jamii'. Huyu ndugu Indivisbo, Mzee wa Kaya, mwenzetu, na kiwakilishi cha sura halisi ya walalahoi Tanzania, kanikaribisha vizuri na kunipitisha pale ofisini kujiandikisha.

Ingawa hili Jengo la 'Jamii Forum Kompleksi' ilinipashida kidogo kupaona lakini kwa maelekezo mazuri wa Yosefu, Mzee wa Chai Tamu, sijapotea sana - tayari niko hapa jukwaani na maoni yao kede kede za kuwasilisha hapa jukwaani. Wenzetu, ingawaje Ratiba ya Uchaguzi Mkuu tayari umesemekana kupita lakini kule kwetu familia ya akina Mung'ong'o peke yao ndio waliopiga kura tena palepale nyumbani kwao lakini sie wengi waliamua kuturahishishia zoezi kutosumbuka kutembea sana kwenda kupiga kura. Mwenyekiti wetu wa Kijiji alitufahamisha kwamba 'AZIMIO LA HOTELI LAKAIRO (MWANZA) peke yake inatosha kupatikana viongozi wote kwetu.

Miongoni mwa mambo ambayo kule jimboni wameniagiza nikayasemee hapa ni pamoja na kushiriki kwa misingi ya kaulimbiu wa 'Walalahoi Tunauwezo kutokomesha kabisa Ufisadi na Matawi yake yote na kupata MFUMO mpya unaotufaa zaidi':

(1) kufanya taathmini ya kina juu ya 'Uchaguzi Mkuu 2010 Tanzania na Maana yake kwa Walalahoi',

(2) 'Mambo gani Yafanyike Tangu Sasa ili Chaguzi zijazo Zisijechukua Mimba ya Kifisadi',

(3) kuanisha 'Mambo ya MSINGI ambayo sisi VIJANA Tunataka Bunge la Kumi Sharti Lifanye katika siku 1800 zijaazo'.

(4) Tujadili na kuamua juu ya 'Changamoto za Mafisadi ambao Tayari Wanajulikana lakini kwa KINGA za nguvu za VIJISENTI vyao bado wanaendelea kuvinjari kila kona ya nchi na Hata Kutununulia Bakhshishi lukuki wa aina ya Viongozi ambao Wapendezewa Kutuongoza', na

(5) kubwa zaidi wameniagiza wananchi hawa nikawakilishe kwenu KAMA AMBAVYO walivyoniagiza ili yapate kujadiliwa kwa kina mapendekezo juu ya 'MIONGOZO KUMI YA WALALAHOI KUCHAGUA VIONGOZI WOTE TANZANIA 2015.'

'AMRI KUMI ZA WALALAHOI KUCHAGUA VIONGOZI WOTE TANZANIA 2015.'

1. Utetezi wa Maslahi ya Umma/Taifa kwa gharama yoyote ile: (40Marks)

Mtu yeyote ambaye anaonyesha uwezo wa dhati wa kuweza kufikiri, kuamua, na kutenda jambo nje ya itikadi za kichama, kidini, kimikoa na nyinginezo, kwa maslahi ya taifa na Umma wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania (JMT).

Awe na uwezo utakaoonekana ama ndani ya Bunge au hata kwa wale ambao kwa sasa sio Wabunge, Madiwani wa hata Wakuu wa Mashirika mbalimbali kuonyesha UDHATI kabisa bila ya UNAFIKI Kutetezi wa 'Maslahi ya Umma / Taifa' walau kwa 75 % na zile za kiitikadi nyinginezo kwa kiwango kisichozidi 20% ya muda wako kwa kipindi cha siku 1800 tangu ratiba ya uchaguzi kukamilika.

2. Mcha Mungu mwenye Maadili Mema kwa Jamii: (20 Marks)

Tutatazama zaidi mtu na mapenzi yake kumuabudu Mwenyezi Mungu kwa dhati kabisa, kuzingatia maadili mema machoni mwa yamii wakati wote na kwa kila alitendalo LAKINI asieacha ulevi wa imani yake kupanda kichwani na na kuanza kuathiri wengine walioko nje ya imani husika.

Asiwe mtu mwenye ama kuhonga au kuhongwa donari 30, cheo, mwili au maslahi nyinginezo ambazo sisi wananchi tunaweza kuzing'amua kwa kipindi husika au hata baadaye. Pindi anapokaribia kuingia MKATABA WOWOTE kwa niaba na kwa jina letu na basi kwanza afikirie sura zetu, shida zetu kama taifa, ajiulize zaidi na zaidi kwamba hata akiaaga dunia dakika inayofuatia je wenzake katuacha penye salama na maslahi inayovuka mipaka ya familia yake????????

Mtu huyu ni sharti asiwe na harufu yoyote ya ufisadi, kushiriki kwa namna yoyote ile au hata kuruhusu ufisadi utokee, bila ya kuchukua hatua stahili za haraka kulizuia, na hasa katika mazingira ambayo mtu yeyote atakayewekwa kwa nafasi yake hiyo inadhihirika wazi kwamba angeliweza kuzuia hiyo hali kabisa. Vile vile awe mbele zaidi katika kutafuta majibu ya kuandika upya sheria za uchaguzi, na katiba mpya.

3. Mbunifu na wa Kuzalisha miradi na Ajira zaidi Kwetu sie VIJANA: (25 Marks)

Ni lazima awe kiongozi mbunifu mwenye kuchangia zaidi hoja za kuzalisha nafasi za ajira zaidi na tija zaidi kwetu sisi vijana na kwa njia za wazi zaidi.

Awe kiongozi wa kampuni, shirika la umma, au Asasi za Kirai zinazotumikia wananchi walio katika dhiki ya maisha na wala kutoendesha mambo kiitikadi za kichama cha siasa, kikundi au kujiruhusu akili yako kutumika kama TAWI LA MAFISADI pa kupigia ramli namna gani kutuibia na kutusokomeza zaidi katika lindi la umasikini wa kutisha.

4. Nguvu ya Umma kushika Hatamu: (15 Marks)

Awe ni kiongozi ambaye anawashirikisha zaidi wanachi katika maendeleo anayoinua kutufanya nasie tukayapate, hoja zake bungeni mara kwa mara zitoke kwetu moja kwa moja kwa njia ya kukutana nasisi mashinani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom